Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mambo ni bora liende tu tunakosa umakini kwenye mambo ya msingi.
Sasa kama tuna resources za kila lakini bado tunakimbilia mikopo kama Taifa tunafeli.
Lissu hajawahai kutetea wananchi au maslahi ya nchi yeye anateteta maslahi yake na mashoga wenzake.Je umewahi kumsikia akimtetea mwenyekiti wake hata huko aliko?
Kalamu ya Baba Askofu Benson Lwakalinda Bagonza
UMOJA au UHURU WA MIHIMILI?!
Spika kakosoa.
Rais kajibu.
Nani yuko sahihi?
Ugumu uko hapa:
1. Ukiishakuwa kiongozi unapoteza haki ya kulalamika. Rais kaonyesha uongozi kwa kukopa. Spika kapoteza uongozi kwa kulalamika.
2. Tunahitaji uhuru wa mihimili siyo Umoja wa mihimili. Maslahi ya walipa Kodi yapo katika uhuru wa mihimili si Umoja wa mihimili.
3. Watawala wasipigane vijembe. Simba akinguruma anamsaidia mwindaji ajue mahali Simba alipo. Rais azingatie moyoni.
4. Spika kapatia kutujulisha hatari za mikopo. Atujulishe na hatari ya kulipa mishahara wasio wabunge. Amalizie kutujulisha uhalali wa sheria zinazotungwa na wasio wabunge.
5. Mikopo ikisababisha nchi ipigwe mnada, bunge na mahakama watakosa uhalali wa kutumia sheria zilizotungwa na wasio wabunge.
6. Spika anashabikia tozo kuliko mikopo. Tozo ni maumivu yetu. Zimeua matumaini ya kuishi ili tuweze kwenda madarasa yanayojengwa na tozo.
6. Tukumbushane: Wakikosekana wapinzani wa kweli, CCM itatengeneza wake wa ndani. Tumempata Kiongozi Mkuu wa upinzani bungeni. Mmemwona? Vaeni miwani.
CCM imara inahitaji Upinzani Imara siyo upinzani wa ndani.
Kazi Iendelee.
Yeleuwii na bado mradi wa bwagamoyo asalalee hii nchi yetu nani wa kuiokoa jamani.
Kwanini takwimu za makusanyo ya tozo haziwekwi wazi?Baada ya tafakari ya muda mrefu sana nimelazimika kuyaelewa maneno ya Spika Job Ndugai. Naungana nae.
Ni wazi kuwa maneno yake yamekuja wakati sahihi. Ameongea kama mwananchi wa kawaida kabisa... Na kwa vile yupo ndani ndani huko kuna mengi anayajua!
Cha ajabu sisi wananchi wa kawaida ndo wale wale tunaompiga vita na kumkashifu. Tulipaswa tuwe na harakati huru na endelevu za kutaka kujua matumizi ya fedha za mikopo na zile za tozo! Isije ikawa tunatumika kama dhamana ya mikopo ili wateule wachache wazidi kuneemeka.
Dalili za matumizi ya kufuru na anasa zipo wazi kabla hata ya SSH. Je, hatupaswi kwenda mbali zaidi kuhoji uhalali wa mikopo/tozo na matumizi yake?? Au tukishaambiwa na watawala basi tuufyate zaidi ya maandiko!
Mambo ni bora liende tu tunakosa umakini kwenye mambo ya msingi.
Sasa kama tuna resources za kila lakini bado tunakimbilia mikopo kama Taifa tunafeli.
ITA mkuu🤔🤔🤔 Tanzania Institute of Accountancy (TIA), ni chuo cha kodi mkuu???
Kile ni kichaka cha Mwigulu... anajichotea tu!!Kwanini takwimu za makusanyo ya tozo haziwekwi wazi?
Vodacom walitoa tathmini ya miamala wanayokamilisha kwa mwezi kufikia 10T transactions. Sasa pigia hesabu kila muamala serikali ile buku tu ni bei gani wanapata? Halafu ati makusanyo yalikuwa 48B tu 😅😅😅Kile ni kichaka cha Mwigulu... anajichotea tu!!
Achana na JPM, kalaumu ndugu na jamaa za familia yenu mnavyoparangana.Ndugai anapaswa kujua kwamba kama angesimama imara Magufuli asingethubutu kukopa fedha halafu akaendelea kuuhadaa umma kwamba tunatumia fedha zetu za ndani.
Udhaifu wa Ndugai ndiyo umepelekea taifa kufika hapa lilipo. Bunge chini ya Ndugai lilimuacha Magufuli akaongoza nchi kama vile anaongoza familia yake na sasa kila kitu kimeharibika.
Ndo vzr, kusema ukweli hatuelewi tulipo wala tunapopelekwa! Mama kaishiwa pumziNdungai ameamua kumkabili Hangaya uso kwa uso.
Unasumbuliwa na tatizo dogo Sana.....sukuma gang disorder.Achana na JPM, kalaumu ndugu na jamaa za familia yenu mnavyoparangana.
Sawa mkuuKuna wakati ni bora uungane na adui mdogo wa adui yako kupambana na adui mkubwa...