Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada...
Mwendesha mnada ni yeye! Anashindwa nini kuzuia? Aungane tu na wanaodai katiba mpya ili aujue wajibu wake na ausimamie!
 
Kama huu mwak mmoja tu amekopa hivi je, itakuaje kama atakapewa mitano mingine si atauza nchi huyu aende kwao.
 
Hangaya akiendelea kuwepo na kutaka kutawaka si ajabu akawepo na rais hajaye baada ya Hangaya akawa Mzanzibar wakaendelea kulithishana, watakuja kustuka sekta zote za juu wamejaa wazanzibar
Acha wendawazimu,kwani wazenji wanatatizo gani ilihali tanzania ni moja?
 
Hakuna nchi inapigwa mnada,, marekani ndo nchi inaongoza kwa deni kubwa, mpaka serikali huwa inafungwa kwa mda,, lakini haijawahi kuuzwa,,,, [emoji1787][emoji1787]
Hahahaaaa mkuu, nimependa comment yako hiyo saaana kuhusu Marekani.

Lakini limenizulia swali hili: Unaweza kumuuza babako au yeye ndiyo anaweza kukuuza?

Risk ya Tz kuuzwa ni kubwa kuliko risk ya Marekani kuuzwa maana Marekani ni baba na Tz ni mtoto.

Ila ni kweli Marekani ina deni kubwa mno lililokuzwa na Reagan & Bush Jr kupitia vita nje ya nchi & Trump kupitia C-19.
 
By that time mwendazake anakopa kimya kimya huku anaongopea kuwa anajenga kwa pesa za ndan ya nchi si alikua anajua huyu ndugai,why hakuzungumza sasa
 
nimwelewe Nini hapa ? Kwani kipindi Cha jiwe madini hayakuwepo, lakini alikopa , alidhibiti madini wakati hana hata ujuzi wowote wa hayo madini kuyatumia au kuyaprocess. Siwezi mwelewa mtu anaye msifu na kumwadu jiwe.
We kweli jinga!

Soma tena!
 
Umeandika ujinga mtupu na kishabiki, Jiwe kakopa sana , na hatujui pesa zote kapeleka wapi, alikuwa hatoi ajira, alifukuza wafanyakazi hewa, na alisema tunajenga kwa pesa zetu wenyewe huku akikopa kwa Siri kwa Nini?
Tena alikuwa mtu wa hovyo sn japo ni kama aliyepo pia naye ni yale yale
 
Alikuwa anatudanganya hakopi kumbe anakopa kisirisiri bila kuweka Mambo wazi halafu anatudanganya nchi hii Ni tajiri wakati anatembeza bakuri. Jk mpaka anatoka kaa si zaidi ya trillion 40 tu. Hiyo nyingine ni jpm. Na vyombo vya habari vilikuwa vinaogopa Mana wangeuuawa.

Sema mama anachokosea ni kuweka wazi Sana kila kitu na kuwapa Uhuru kila mtu.
Katiba mbovu sn hii
 
kwamba siutetei upande wowote kwa ushabiki holela bali kwa hoja zenye kujibu naomba ieleweke,

Kusherehekea pesa kama wendawazimu bila kuelewa msingi wake ni utoto na mnaambiwa ukweli taka msitake!!!

Mwendazake alikuwa na plan zake na lkwa hili la leo wenue akili wote tumeelewa kuwa blue paper ya aliyoyafanya ilijulikana na the the top 5 of national authority akiwemo huyo job. Plan iliyokuwa na utaratibu wa kurejesha pesa kwa kupitia maliasili za madini haraka sana , ila hakuweza kisimamia plan hiyo mpaka mwisho kwa yaliyotokea.

Waliokuja, hawana uwezo wa kutembelea kiatu kile kwani uwezo wa kudhibiti maliasili na kuwabana mabebeeu ili kuingiza pesa hawana. Lakini bado tunawataka watekeleze maendeleo waliyoyarithi , hapo ndio kizungumkuti!
Wametapatapahuku na huko, mara tozo mara luku n.k lakini hela haitoshi kuendeleza miradi! Ikabidi wafuate masharti ya mabeberu ili wapate fedha , wananchi muone fly over na ndege mpya lkn njia ya kupatia fedha ilisha badirika.
Kwakuwa waliokuwepo wanajua ilivyokuwa na ilivyosasa, wanaona jinsi picha sasa linavyotisha . Kwa kupata maendeleo yale yale kimikopo bila uwezo wa kudhibiti madini ili kulipa mikopo hiyo jibu lake ni wazi kuwa hiyo ni disaster inakuja.

Hata ukiamgalia lile jiwe lilikuwa halisafiri kwenda magharibi na lilikuwa linajisifu kuwa linaandaa donor country, na mziki ule ilifikia dunia ikauelewa vizuri sana, kwani jiwe linakuambia Nickel ya kagera inatumika kutengeneza ndege na Tz ni ya 3/2 duniani , hellium ni gesi muhimu na Tz ni ya 1 au 2 duniani, bila kutaja madini mengine mengi tuliyonayo kwa wingi. Ukiweza kiyadhiniti vema hata ukope unakuwa na kiburi cha kulipa maana hata matajiri wanaweka akiba ya dhahabu sio minoti tu sasa kama una dhahabu ardhini maana yake unauhakika kuwa wewe una pesa na hakuna mtu mwenye akili anaejua nafasi ya dhahabu katika teknolojia ya uzalishaji na katika matumizi yake kama fedha atakunyima mkopo wowote akijua dhahabu ipo.
Tatizo linakuja kwa wattawala dhaifu ambao ubeberu wanauruhuau tena urudi, hawana udhibiti tena wa madini yetu( pesa yetu) , sasa hata wakikopa deni linakosa uhakika wa kulipwa , nchi ni lazima itapogwa mnada. Hawana jeuri ya kusema tena ," Tanzania ni tajiri".
Kazi iendelee mkuu. JPM 1959 - 2021.
 
Spika Ndugai kiukweli ametoa tahadhari nzuri tu, hebu fikiria ingekuwa ni Tundu Lisu ndio kaiponda mikopo ya mabeberu hakika hapa Jf pasingetosha pongezi za makamanda.

Ila kwa sababu aliyeshauri ni mgogo watu mnadharau hoja yake.

Maendeleo hayana vyama!
 
Of course tunashangaa sana kuona ombaomba maarufu tz anapinga mikopo. Hata yeye analijua ndio maana alijihami kwa kutaja kabila lake kwanza ili wasimshambulie imekuaje matonya anapinga mikopo aka uombaomba.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom