Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Huyu ndugai ndo alikuwa mstari wa mbele kutufokea kuhusu tozo akimsaidia chifu na madelu huku akitunanga kwamba kama hatutaki tozo tutafute vyanzo mbadala.........halafu anakuja kulialia hapa wakati bunge la mazuzu ndo wenye mamlaka ya kuibana serikali.......
 
Dah! Hapo ndiyo mimi nachoka kabisa na viongozi wetu, Mh Spika kasema hivyo kweli! Sheria zote zinatungwa pale kwenye Bunge letu tukufu na yeye ndiye kiongozi wa huo mhimili……. this is it.
Yes it is it
 
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada amenena maneno hayo baada ya kusema kwamba tozo zote zamiamala ya simu zilizopitishwa na bunge zilipitishwa kwa lazima kwani wananchi hawakuridhia kama inavyosema na baadhi ya wanasiasa.

Kwa maneno hayo naona kuna mambo yanaendelea huko Lumumba yapo mambo hayajakaa sawa ukiona spika anaanza kulalamikalalamika! Alianza kuhusiana na serikali kuhamia Dodoma kuwa kwa sasa kazi zote za serikali na makongamano zimerudishwa Dar-es-Salaam.

Mheshimiwa Ndugai popote ulipo nakwambia hivi wewe na viongozi wako mnaifanyia nini hii nchi mbona mnakaa mnalalamika lalamika wakati chama ni cha kwenu na chama chenu ndicho kimeunda serikali.?
View attachment 2060237
Nafikiri Ndugai kapata karipio/vitisho baada ya malalamiko yake ya awali.
 
Next time tunahitaji Magufuli aingie bungeni sasa ili kuondoa upuuzi! Naimani Bunge likiwa na mtu strong hata raisi kufanya upuuzi ni ngumu
Ngumu, hawezi kwenda kinyume na matakwa ya atakayemuweka (m/kiti wa chama chake).
 
Screenshot_20211228-102304.png
 
Kipindi hayo yote yanafanyika ndungai alikuwa Bado hajawa spika wa bunge? Ccm ni wanafiki wazandiki maguluguja.uzuli ni kwamba bunge lote ni kijani wananchi tunajua Kila kitu.
Sawa ni bora kuwa Mnafiki ambaye mara moja moja unasema ukweli kuliko Wanafiki wanaopiga makofi tu mpaka wanakufa ili hali Nchi inaangamia.
 
Miongoni mwa mtu ambaye hana la maana nchi hii ni Job. Yeye akae kimya kabisa. Wakati wa mwendazake alishiriki jinai zote mpaka zingine ambazo hata mwendazake alishangaa. Job hajui kwamba yuko na wabunge ndani ya bunge lake ambao hawana chama? Hili kwake yeye anaona ni sawa? Job ni sehemu ya watu wa hivyo ambao wameliharibu sana taifa hili na uongozi wake.
Wewe spika washughulikie ndani ya bunge mimi nitawashughulikia nje ya Bunge. Ndipo akawa anawafukuza bungeni yule mwenzie anawatandika nje ya bunge. Anadhani tumesahau. Huyu akae kimya tu.
 
Back
Top Bottom