Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Taratibu watu wataanza kumwelewa magufuli. Alikua nania tujitegemee wenyewe. Ñdio kisa cha kuchukiwa na wenye nia mbaya ndio wamekumbatiwa na Awamu ya 6
Duh wakati yeye pekee amekopa 22trilioni tena akatupiga kamba kua ni pesa za ndani.
 
Ni bahati mbaya sana kwa Taifa letu kuwa na subwoofer huyu tuliyenaye. Huyu ni sehemu ya matatizo ya kiutawala kwa nchi hii.
 
Iuzwe tu, Tanzania na watu wake tuuzwe tukalipie mkopo.

Hata hayo yanachosha.

Hizo hela mnafanyia nn, huku ki dispensary ni kile kile, soko hakuna, kituo cha polisi hakuna, kisekondari hicho hapo kina darasa moja, air port hakuna.

ni hapa mkoa wa pwani tu hapa.

Naungana na Job nchi iuzwe.
 
Spika wa Bunge ameonya kitendo cha serikali kuendelea kutegemea mikopo kutoka nje kuendesha nchi kitu ambacho kimefanya deni la taifa kuwa kubwa maradufu "Ipo siku hii nchi itapigwa mnada,kopeni tu".

View attachment 2060343
Yeye pamoja na Wabunge wenzake ndio wanasababisha deni la taifa linaongezeka kwa sababu hakuna wanachozalisha pale bungeni zaidi ya matumizi makubwa yasiyo ya lazima. Mfano posho wanazolipwa hata kama mbunge ameenda kusinzia bungeni kama yule mzee wa Bunda, magari ya kifahari badala ya kununua Vitz, mishahara isiyokatwa kodi, kupitisha sheria kandamizi dhidi ya wanyonge, kuvunja katiba kwa kuingiza wabunge wasiokuwa na chama mfano wale COVID19(wanaolipwa kodi za wanyonge kwa kuingizwa bungeni na Ndugai wakati hawana vyama kinyume na utaratibu wa kikatiba)
 
Duh wakati yeye pekee amekopa 22trilioni tena akatupiga kamba kua ni pesa za ndani.

Kukopa kujenga SGR, Maji ya uhakika, miundombinu ya barabara. la umeme, umeme nafuu wa uhakika kwa viwanda, biashara na binadamu ni kitu kizuri kama mikopo ni ya masharti nafuu.

Ina maana itajilipa yenyewe ndani. Tatizo hapa usimamizi na matumizi na wasimamizi sahihi wa hii mikopo. Kuna wapiga dili, wala rushwa, mafisadi. umeme, maji sio vitu vya uhakika tena.
 
Tumsikilize Rais Au Tumsikilize Spika wa Bunge?

Rais Samia Anapata Upinzani mkali sanaa Ndani Ya Chama Bila Kujijua… Ana Deal Na Kina PolePole, Gwajima na Jerry ambao hata sio
 
Rais Magufuli yule mwamba tuache tu apumzike kwa amani, ipo siku itatengwa siku itatengwa kwa ajili yake. Kipindi chake hatukuwahi kusikia wala kuona kiongozi anayemlipa mshahara anamkosoa
 
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada amenena maneno hayo baada ya kusema kwamba tozo zote zamiamala ya simu zilizopitishwa na bunge zilipitishwa kwa lazima kwani wananchi hawakuridhia kama inavyosema na baadhi ya wanasiasa.

Kwa maneno hayo naona kuna mambo yanaendelea huko Lumumba yapo mambo hayajakaa sawa ukiona spika anaanza kulalamikalalamika! Alianza kuhusiana na serikali kuhamia Dodoma kuwa kwa sasa kazi zote za serikali na makongamano zimerudishwa Dar-es-Salaam.

Mheshimiwa Ndugai popote ulipo nakwambia hivi wewe na viongozi wako mnaifanyia nini hii nchi mbona mnakaa mnalalamika lalamika wakati chama ni cha kwenu na chama chenu ndicho kimeunda serikali.?

=====

UPDATES;

=====

=> Watu wengi wanatulaumu sana, ninyi ndio Wasomi. Hebu fikiria, Juzi mama kaenda kukopa 1.3 Trilioni deni.

=> Na tuna majengo hivi sasa ya Madarasa, ya Vituo vya afya, ambayo yanajengwa kwa tozo. Hivi ipi bora? Sisi Watanzania wa miaka 60 ya Uhuru tuendelee kukopa na Madeni au tubanane banane hapa tujenge wenyewe bila madeni Makubwa yasiyoeleweka? Ni lini tutajenga wenyewe?

=> Tutembeze bakuri ndo heshima? na tukishakopa tunapiga makofi! Sisi wa kukopa kila siku?

=> Tukasema pitisha Tozo, anayetaka asiyetaka, pitisha Tozo. Lazima tuanze kujenga wenyewe. Nani atatufanyia? Yupo wapi huyo Mjomba? Tukapitisha Tozo.

=> Sasa 2025 itaamua. Mkitoa waliopo sawa. Waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa endepo hiyo ndo namna ya kuendesha Nchi.

=> Hivi sasa deni letu ni 70 Trilioni. Hivi ninyi si Wasomi? Is that healthy? Kuna siku nyi itapigwa mnada hii. Madeni Madeni Madeni

=> Bajeti yetu Trilioni 30, Trilioni 10 kati ya hizo kwa Mwaka tunalipa Madeni.

=> Tumeenda Kukopa 1.3 Trilioni, Tunapiga Makofi. Tunawapa Wazungu Trilioni 10 Mariba Matupu. Wanatufanya Sisi Mazezeta. Hela yako Mwenyewe. Anachukua hela yako, halafu anakupa Kidogo Unashangilia.

=> Toza fanya hivi, tujitegemee, Tusimame wenyewe. Kuna ubaya gani? Hata msomi anatupinga.
View attachment 2060338

"Wapinzani walituchelewesha sana." Alisikika yule shujaa.
 
Back
Top Bottom