Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Tafsiri ya malalamiko ya Spika ni kwamba Mhimili wa Bunge umeshindwa kufanya kazi yake ya kuisimamia serikali (inakopa hovyo hovyo). Hivyo basi, Mhe. Ndugai kwa kauli yake anathibitisha kuingia rasmi kwenye kundi la akina Polepole, Gwajima na Silaa.
Kwahiyo orodha ya watakaoitwa kuhojiwa na chama Ndugai aongezwemo.
 
Yani eti wanaona tuna option mbili japokuwa tuna kila aina ya rasilimali. Yani kwao option ni either tukope au tozo
Yaani ni ufinyo wa kufikiri kabisa ni sawa na daktari kumpa mgonjwa option either kumchoma sindano ya kusogeza mbele muda wa maumivu ama kumuamishia tatizo la jicho na alipelekee sikio.
 
Kwahiyo orodha ya watakaoitwa kuhojiwa na chama Ndugai aongezwemo.
Julai 23, 2021 Spika alisema hili:
Spika Ndugai amesema wabunge wameshapitisha tozo ya kizalendo kwenye miamala ya simu na sasa ni sheria hivyo asiyeitaka atupe njia mbadala ya kutufikisha 2025.

Disemba 28, 2021 Spika asema hili:
Spika wa Bunge ameonya kitendo cha serikali kuendelea kutegemea mikopo kutoka nje kuendesha nchi kitu ambacho kimefanya deni la taifa kuwa kubwa maradufu "Ipo siku hii nchi itapigwa mnada,kopeni tu".

Wananchi tushike lipi tuache lipi?
 
Spika wa Bunge ameonya kitendo cha serikali kuendelea kutegemea mikopo kutoka nje kuendesha nchi kitu ambacho kimefanya deni la taifa kuwa kubwa maradufu "Ipo siku hii nchi itapigwa mnada,kopeni tu".

View attachment 2060343
Kama tozo ni bora, basi pigeni tozo migodi yote iliyo chini ya mabeberu mtalipa hizo trillion 70. Au nasema uongo ndugu zangu !!
 
Watu wanakesha angani safari kila siku kwanini wasiishi kwa kukopa?
Matumizi makubwa kuliko mapato.
 
Isanga family Kauli yako haileweki. Swali lilikuwa lipi bora tozo au mikopo? dhambi ipo wapi kwenye kuhoji hilo?
Wao wakuishauri Serikali ndio wanahoji Nchi ina matumizi makubwa ya hovyo tuu nilishangaa kuona mji wa Brantyre bei ya mafuta ipo sawa na Mwanza Tanzania kuja kuangalia tuna kodi nyingi sana kwenye mafuta achilia hilo bei ya mafuta Malawi ni moja Nchi nzima sio sisi uwizi na uongo tuu Pepsi ina bei moja ila mafuta tunayawekea vipengele wapo wachache wananufaika na hili..
 
Leo nimeamini kwamba Tanzania kuna ombwe la uongozi. Hivi huyu si ni miongoni mwa viongozi wetu? Si huyu alikuwa kimya wakati wananchi wanadhalilishwa na yeye akafanya kejeli?Si huyu alimnyima mpinzani mmoja haki zake kwa kutetea umma? Si huyu alinyamaza kimya wakati serikali inakopa na tukidanganywa tunajenga na kumunua kila kitu kwa pesa taslimu hadi ndege! Si aseme tu kwamba hii ni kwasababu usukani uko mikononi kwa mama? Hivi siku hizi uko wapi uwajibikaji wa pamoja? Eti 2025 mchagueni tena tuone. Ila mama yupo na wala hakujiweka mwenyewe. Ni katiba iliyotungwa na watu kama Ndugai ambaye leo anajifanya amesahau. Watu wanamuona na wala hatoki ikiwa kuna lawama. Ni yeye na wenzake.
Huwaga hamuelewi hoja iliyopo mezani!!??
 
Julai 23, 2021 Spika alisema hili:
Spika Ndugai amesema wabunge wameshapitisha tozo ya kizalendo kwenye miamala ya simu na sasa ni sheria hivyo asiyeitaka atupe njia mbadala ya kutufikisha 2025.

Disemba 28, 2021 Spika asema hili:
Spika wa Bunge ameonya kitendo cha serikali kuendelea kutegemea mikopo kutoka nje kuendesha nchi kitu ambacho kimefanya deni la taifa kuwa kubwa maradufu "Ipo siku hii nchi itapigwa mnada,kopeni tu".

Wananchi tushike lipi tuache lipi?
Ndugai,
Mimi nafikiri bora tuendelee kukopa ili tuwe huru kusimamia miradi yetu itokanayo na mikopo hiyo kuliko kumpa Mchina 50% ya Bagamoyo ajenge mradi avune kwa miaka 100 bila sisi kupewa uhuru wa kujuwa kinachoendelea kwenye mradi huo.

Kwa staili hiyo hiyo Mchina anamiliki Terminal 2 ya Lusaka, Bandari ya Mombasa, SGR ya Kenya na sasa ameshika mali kibao za Singapore ughaibuni kufidia gharama za ujenzi na uendeshaji wa Bandari ya Singapore ambayo ndiyo role-model duniani kwa spidi ya port turn around ambayo ni 5 hrs; baada ya Singapore kushindwa kuvumilia miaka kibao ya mkataba wa Mchina kujenga, kuendesha na kukabidhi Bandari (BOT - Build, Operate Transfer).

1640696576676.png

Singapore Port, chini ya Mchina.

1640696658536.png

Kenneth Kaunda International Airport Terminal 2 chini ya Mchina, soma maandishi ya Kichina ukutani mwa jengo.

1640696756920.png

Mombasa Port chini ya Mchina.

1640697193326.png

Kenya SGR Train-Hostess. Miundombinu hii ya kimkakati iko chini ya Mchina.

Taswira zote kwa hisani ya google.
 
Katika mnada huo Gzinjabar haitahusika kabisa.

Wakenya, Waganda na Wanyarwanda waanze kuweka pesa kuna nchi ya bure huku wenye mamlaka wameanza kuota kuiuza kama shamba la urithi.

Kuna ombwe la uongozi kwa miaka mingi sana hapa duniani
Hakuna nchi inapigwa mnada,, marekani ndo nchi inaongoza kwa deni kubwa, mpaka serikali huwa inafungwa kwa mda,, lakini haijawahi kuuzwa,,,, [emoji1787][emoji1787]
 
Misingi ya nchi hii ni ujamaa na kujitegemea lakini pia baadae tukasema ni nchi isiyofungamana na upande wowote tuliamua Kua vuguvugu nadhani shida imeanzia hapa.
 
Back
Top Bottom