Anacho maanisha ndugai ni kuwa hawa jamaa wa kambi mizoga wao ni vibaraka wa mabeberu na hawana uwezo wa kudhibiti maliasili za taifa hili dhidi ya mabeberu.
Tunapoongelea kitu kinachoitwa "mkopo" kila mtu anajua kwamba nyuma ya mkopo kuna jambo linaitwa " dhamana", kama wewe huna ujasiri wa kukinga kifua mbele ya mabeberu kuidhibiti maliasili yako basi wewe dhamana ya mikopo yako inakuwa ni tofauti kabisa, ni masharti magumu , yanayoweza kusababisha nchi ikauzwa.
Kama nina dhahabu ndani na nimeishiwa chakuka nikikopa mchelle dukani halafu wewe up kanicheka eti najitamba kuwa nina hela, wakati nimekopa , ni ujinga wako tu ndio Unakusumbua.
Kabla ya kuanza kutumika haya makaratasi dhahabu ndio ilitumika kubadirishana kama fedha duniani. Na hata leo mabenki wanahifadhi dhahabu pia sio manoti peke yake, matajiri unaowajua awe mo, mengi, bakhresa n.k wote huweka akiba ya dhahabu sio minoti tu. Hii ni dunia nzima.
Ni majuha sisi watz, kwamba tuna dhahabu ardhini ya kutosha lakini bado tunajiona sisi ni maskini, hili ndio alikuwa analisema magufuli , marehemu. Maana inakuwaje benki za ulaya , matajiri wote mpaka wafalme wote wahesabu dhahabu zao katika utajiri wao halafu wewe uwe na dhahabu nyumbani kisha ujiite wewe ni maskini, huo ni ujuha aliokuwa anaushangaa magufuli, ni akili ya kurogwa na mabeberu na kundi lao la mizoga.
Hivyo mru mwenye uwezo wa kudhibiti madini, huyo ana pesa,huyo ni tajiri, usimuige wewe kibaraka wa mabeberu unaejiuza utashi wako kwa kujipendekeza kwao kila uchao utatumia vipi madini Yako kama dhamana , lazima nchi itauzwa tu,