Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Ndani ya serikali ya JPM hawa watu wamejifunza mengi pia wamejifunza kuipenda nchi. Zaidi wamejua kuwa kumbe viongozi wakiamua nchi inaweza kupiga hatua.

Maendeleo yale yamenufaisha majimbo yao na ndugu zao wakiwemo mashangazi, baba wadogo na wengine.

Mfano; zahanati na vituo vya afya, huduma rafiki kwenye taasisi za serikali zilizokuwa zinapatikana kwa wakati huo sio sasa, umeme kila kijiji tena wa uhakika usiokatikakatika, miundombinu ya uhakika hadi kuunda tarura, mifumo ya maji safi hadi vijijini. Hii hata wao wabunge iliwarahisishia kiutendaji.
 
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada amenena maneno hayo baada ya kusema kwamba tozo zote zamiamala ya simu zilizopitishwa na bunge zilipitishwa kwa lazima kwani wananchi hawakuridhia kama inavyosema na baadhi ya wanasiasa.

Kwa maneno hayo naona kuna mambo yanaendelea huko Lumumba yapo mambo hayajakaa sawa ukiona spika anaanza kulalamikalalamika! Alianza kuhusiana na serikali kuhamia Dodoma kuwa kwa sasa kazi zote za serikali na makongamano zimerudishwa Dar-es-Salaam.

Mheshimiwa Ndugai popote ulipo nakwambia hivi wewe na viongozi wako mnaifanyia nini hii nchi mbona mnakaa mnalalamika lalamika wakati chama ni cha kwenu na chama chenu ndicho kimeunda serikali.?

=====

UPDATES;

=====

=> Watu wengi wanatulaumu sana, ninyi ndio Wasomi. Hebu fikiria, Juzi mama kaenda kukopa 1.3 Trilioni deni.

=> Na tuna majengo hivi sasa ya Madarasa, ya Vituo vya afya, ambayo yanajengwa kwa tozo. Hivi ipi bora? Sisi Watanzania wa miaka 60 ya Uhuru tuendelee kukopa na Madeni au tubanane banane hapa tujenge wenyewe bila madeni Makubwa yasiyoeleweka? Ni lini tutajenga wenyewe?

=> Tutembeze bakuri ndo heshima? na tukishakopa tunapiga makofi! Sisi wa kukopa kila siku?

=> Tukasema pitisha Tozo, anayetaka asiyetaka, pitisha Tozo. Lazima tuanze kujenga wenyewe. Nani atatufanyia? Yupo wapi huyo Mjomba? Tukapitisha Tozo.

=> Sasa 2025 itaamua. Mkitoa waliopo sawa. Waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa endepo hiyo ndo namna ya kuendesha Nchi.

=> Hivi sasa deni letu ni 70 Trilioni. Hivi ninyi si Wasomi? Is that healthy? Kuna siku nyi itapigwa mnada hii. Madeni Madeni Madeni

=> Bajeti yetu Trilioni 30, Trilioni 10 kati ya hizo kwa Mwaka tunalipa Madeni.

=> Tumeenda Kukopa 1.3 Trilioni, Tunapiga Makofi. Tunawapa Wazungu Trilioni 10 Mariba Matupu. Wanatufanya Sisi Mazezeta. Hela yako Mwenyewe. Anachukua hela yako, halafu anakupa Kidogo Unashangilia.

=> Toza fanya hivi, tujitegemee, Tusimame wenyewe. Kuna ubaya gani? Hata msomi anatupinga.
View attachment 2060338

Zaidi, soma: Thread 'Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏' News Alert: - Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏
😭😭😭😭😭😭😭😭✊
 
Hakika uliona mbali kitega uchumi kikuu Cha nchi kinauzwa kukodisha bandari kwa miaka 100 ni sawa na kuuza mali hiyo ya nchi

Miaka 100 si Samia wala mimi atakayekuwepo duniani

Hakika Magufuli aliposema makaburi yetu yatacharazwa bakora na wajukuu zetu wala hakukosea

TISS kazi yenu kuwafuatilia wapinzani na si uchumi wa nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika uliona mbali kitega uchumi kikuu Cha nchi kinauzwa kukodisha bandari kwa miaka 100 n sawa na kuuza Mali hyo ya nchi

Miaka 100 si samia Wala mm atakayekuepo dunian

Hakika magufuli aliposema magufuli makaburi yetu yatacharazwa bakora na wajukuu zetu Wala hakukosea

TISS Kaz yenu kuwafuatilia wapinzan n s uchumi wa nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
TISS wapo bize lutafuta kinga ya kutoshtakiwa.

Sisi wananchi ni takataka mbele yao. Wanalinda maslahi ya CCM
 
Nchi haina mwenyewe sasa tiss wanataka kinga ili wawe watekelezaji wa atakayo Rais na CCM.....wana siasa wana kinga kuuza rasilimali zote. N.a. hawataguswaaa ....jeshi wanaona ila watasema hawafanyi siasa lakini nani hasa kusimamia radilimali kubwa kama bandari kuuzwa? Kwakweli hapa Hapana Hapana tujadili kwa mapana yake
 
Back
Top Bottom