Joe Biden achaguliwa kuwa rais wa 46 wa Marekani

Kwa mujibu wa matokeo yanayoendelea kutangazwa huko USA inaonesha tayari Serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Donald Trump imeangushwa.

Bado hakuna uhakika kama Rais Trump ataridhia matokeo na hivyo kumuachia ofisi Mshindi Joe Biden.

Ikumbukwe kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mara kwa mara umekuwa ukitoa matamko ya mwenendo wa uchaguzi uliokwisha nchini Tanzania ukihoji juu ya matukio ya ukandamizwaji wa demomrasia kwa kusikiliza madai potofu ya wapinzani.

Ikumbukwe kuwa Rais Trump amenukuliwa mara kadhaa akihoji mwenendo usioridhisha wa upigaji kura na utangazaji matokeo katika uchaguzi wa Marekani.

Lakini Tanzania iliendelea kuheshimu demokrasia ya Marekani kwa kukaa kimya bila kutoa matamko yanayohoji uchaguzi uliogubikwa na malalamiko yanayohusu wizi wa kura.

Kwangu mimi naona kuwa ni aibu na laana kwa Serikali ya Marekani ambayo imeondolewa madarakani ...kwani imekuwa ikifuatafuata mambo ya nchi nyingine bila sababu za msingi.
 
Bila shaka wapigakura wa US wanaongezeka kila baada ya miaka 4. Miaka ijayo kunaweza kuwa na mgombea ambaye atapata kura mil 100 na atashindwa, kulingana na population ya wapigakura ya mwaka huo.
Turnout ya mwaka huu ilikuwa juu kidogo.

Na moja ya sababu ni chuki dhidi ya Trump.

Niliwahi kuandika uzi humu kuhusu akili ya Trump....huenda ndo Rais zuzu kuliko marais wote wa Marekani kuwahi kutokea.
 
Ulisemaga hiki kibabu Biden kinapoteza muda we kiazi leo unasema nini?
 
Wako mbali sana hawa jamaa
Acha kabisa hawa jamaa!! Ajabu eti Lumumba wameumia kuona yaliyotokea manake walitarajia kusikia uhuni waliofanya wao ukifanyika US ili wapate cha kusema!!

Yalitamani kuona wale waliokuwa wakifanay protest waanze kupigwa mabomu ili yaseme hata kwa mabeberu ukiandamana unapigwa mabomu!!!
 
Bila shaka wapigakura wa US wanaongezeka kila baada ya miaka 4. Miaka ijayo kunaweza kuwa na mgombea ambaye atapata kura mil 100 na atashindwa, kulingana na population ya wapigakura ya mwaka huo.
Hili ndo lakuzingatia. Kitu cha kusema hapa ilikuwa ni idadi ya waliopiga kura dhidi ya waliosajiriwa. Hiyo kupigiwa kura na idadi nyongeza ya watu inatarajiwa ikue kila uchaguzi.
 
sitashangaa kama jiwe atatuma salamu za pongezi kwa Biden
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…