Joe Biden achaguliwa kuwa rais wa 46 wa Marekani

Joe Biden achaguliwa kuwa rais wa 46 wa Marekani

Afu wanalazimisha waafrica katika uongozi tuwe na 50...50 kwenye uongozi, wao wenyewe na demokrasia yao ndio mara ya kwanza mwanamke anakuwa kwenye ngazi ya juu kabisa. Nafikiri africa tutafute mfumo wetu sio kila kitu kulazimishwa
 
Mgombea wako alikuwa na character flaws nyingi mno!

Kapata kura zaidi ya milioni 70 na bado kashindwa!

Hakuna mgombea mwingine wa urais aliyewahi kupata kura nyingi namna hiyo na akashindwa.

Biden kapata kura milioni 74.

Nyingi ya hizo kura si za Biden. Ni kura dhidi ya Trump.

Trump angerekebisha tabia yake na kuachana na beef za Twitter na kuacha kutoa kauli za ajabu ajabu, naamini wananchi wangemsamehe licha hata ya janga Corona maana hakulisababisha yeye.

Watu walichoka na drama zake na tabia zake zisizo za ki presidential.
Ila alijitahidi jizuia na vita.
Alijitahidi wakazia China
Alijiweka mbali na North Korea
 
Joe Biden ashinda uchaguzi wa Marekani na kuwa rais mteule wa Marekani baada ya kumshinda Donald Trump.

Bw. Biden ameshinda katika jimbo muhimu la Pennsylvania, akijizolea kura zaidi ya 270 zilizohitajika ili kunyakua kiti cha White House.

Kampeni ya Trump imeonesha mgombea wao hana mpango wa kukubali matokeo ya uchaguzi huo.

Matokeo hayo yanamfanya Trump kuwa rais wa kwanza kutumikia awamu moja madarakani tangu miaka ya 1990.

Uchaguzi huu umeshuhudia watu wengi wakijitokeza kupiga kura tangu miaka ya 1900. Bwana Biden ameshinda zaidi ya kura milioni 73 mpaka sasa, idadi ya juu kuwahi kutokea kwa mgombea yoyote yule Marekani. Trump akipata kura zaidi ya milioni 70 akishika nafasi ya pili kwa idadi kubwa katika historia ya Marekani.

Rais Trump alijitangaza mshindi wa uchaguzi wakati kura zikiendelea kuhesabiwa. Wakati wote amedai kuwa zoezi la kuhesabu kura limekuwa na dosari, lakini hajawasilisha ushahidi wowote kuhusu madai yake.

Kampeni yake imefungua kesi katika majimbo mbalimbali mapema Ijumaa, wakati Biden alipokuwa akikaribia kunyakua ushindi, alisema : ''uchaguzi huu haujakwisha.''

Mchuano ulikuwa ukiendelea huku idadi ya maambukizi ya virusi vya corona na vifo vikiongezeka, huku Rais Trump akisema kuwa kwa Biden madarakani kutasababisha watu kubaki majumbani hali itakayosababisha uchumi kudorora.

Biden amemshutumu Trump kushindwa kuchukua hatua madhubuti kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19.

Joe Biden sasa anajiandaa kurejea Ikulu ya White House, ambako alipatumikia kwa miaka minane akiwa makamu wa rais, msaidizi wa Barack Obama. Akiwa na miaka 78, atakuwa rais mwenye umri mkuba kuwahi kutokea katika historia ya Marekani, rekodi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Trump ambaye ana miaka 74.
 
24, mnataka Trump asimame tena, au someone else?!

Kama mnamtarajia Trump tena, then tell that old man to stop being too arrogant!! Arrogance yake towards anyone else imem-cost huku matokeo yake anaelekea kupoteza hata senate majority!
Republican mwingine, mwaka huu Democrats wametuweza ila hawataperform kama sisi
 
Finally Twitter itapumzika kuziba tweets za Trump

Na mipasho ya Trump twitter itapungua
 
Finally Twitter itapumzika kuziba tweets za Trump

Na mipasho ya Trump twitter itapungua
IMG_20201107_205719.jpg
IMG_20201107_205716.jpg
 
Republican mwingine, mwaka huu Democrats wametuweza ila hawataperform kama sisi
1.Ron DeSantis 2024. My preference.

2. Josh Hawley

3. Doug Ducey

4. Nikki Haley

5. Tom Cotton
 
Bora kina pompeo waondoke zao na balozi wao
Democratic wanakuja kuinyoosha CCM hatari,mtawakumbuka wakina Pompeo kwa kutoingilia kivile mambo ya Africa.
 
1.Ron DeSantis 2024. My preference.

2. Josh Hawley

3. Doug Ducey

4. Nikki Haley

5. Tom Cotton
Harley hataweza.
Ila miaka 4 mingi ngoja tuone.
Performance ya Biden on foreign policy itamsaidia mno kufuta nyayo za Trump.
 
Ntamkumbuka Trump kama mzungu asiekubali kuwajibika kwa makosa yake. Kwa wazungu wengi hii sio tabia ya kawaida. Pole sana mzee ni muda muafaka wa kuanza kupromote mieleka Iran
 
Harley hataweza.
Ila miaka 4 mingi ngoja tuone.
Performance ya Biden on foreign policy itamsaidia mno kufuta nyayo za Trump.
Nikki Haley is solid.

Rock solid.

But I’m still riding with Ron DeSantis.
 
Back
Top Bottom