Joe Biden achaguliwa kuwa rais wa 46 wa Marekani

Joe Biden achaguliwa kuwa rais wa 46 wa Marekani

Afu wanalazimisha waafrica katika uongozi tuwe na 50...50 kwenye uongozi, wao wenyewe na demokrasia yao ndio mara ya kwanza mwanamke anakuwa kwenye ngazi ya juu kabisa. Nafikiri africa tutafute mfumo wetu sio kila kitu kulazimishwa
Subiri uone Democratic wanavyoenda kuinyoosha CCM&serikali yake,mtamkumbuka sana Trump maana hakua na time na Africa zaidi ya kuwaachia wakina Pompeo wa-tweet tu.
 
Ushindi wake unakuja baada ya kushinda kwa kishindo jimbo la Pennsylvania

Anakuwa Rais wa kwanza kuingia Madarakani akiwa na umri mkubwa (miaka 78). Pia, Marekani imepata Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke, Kamala Harris

View attachment 1621542
View attachment 1621578
BIDEN: NITAWATUMIKIA WALIONIPIGIA NA WASIONIPIGIA KURA

Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Marekani katika Nafasi ya Urais, Joe Biden amewashukuru wamarekani kwa kumpa dhamana ya kuongoza taifa hilo

Katika tweet yake amesema atawatumikia wote bila kujali kama walimpigia kura au ambao hawakumpigia kura

Ameahidi kutowaangusha kwa imani ya uongozi ambayo Wananchi wamempa kwa kipindi hiki
View attachment 1621579
Rais Mteule wa Marekani Joe Biden
View attachment 1621544
Kamala Harris Mwana Mama wa kwanza katika Historia ya Marekani kuwa Makamu wa Rais.

Mama ametulia sana aisee!
 
Turnout ya mwaka huu ilikuwa juu kidogo.

Na moja ya sababu ni chuki dhidi ya Trump.

Niliwahi kuandika uzi humu kuhusu akili ya Trump....huenda ndo Rais zuzu kuliko marais wote wa Marekani kuwahi kutokea.
Wewe ulikuwa upande wake ..acha kumkana sasa.
 
Trump sa hii anakusanya mabegi na masufuria aondoke zake jumba jeupe.

Ila nitamiss sana mipasho yake huyu babu ana maneno. Yani alishaleta chokochoko hadi kwa wazungu wenzie wa ulaya huko[emoji3]
 
Subiri uone Democratic wanavyoenda kuinyoosha CCM&serikali yake,mtamkumbuka sana Trump maana hakua na time na Africa zaidi ya kuwaachia wakina Pompeo wa-tweet tu.
Hana lolote la kufanya, zipo nchi km uganda, rwanda ambazo hata kubadilisha viongozi tu hawajabadili lakini kila wakati inabaki mikwara tu. Sio rahisi km unavyofikiri
 
Hapo kwenye makamu wa rais mwanamke wametuiga Tz
 
Hana lolote la kufanya, zipo nchi km uganda, rwanda ambazo hata kubadilisha viongozi tu hawajabadili lakini kila wakati inabaki mikwara tu. Sio rahisi km unavyofikiri
Hizo nchi zimepitia mititi ya vita ya kutosha na zinajulikana ni 'volatile' wanazipotezea kwa misingi hio.

Bongo yenyewe ilipitia vita vya wenyewe kwa wenyewe lini na ni 'volatile'?
 
Wewe ulikuwa upande wake ..acha kumkana sasa.
Mimi niliyeandika huu uzi miezi kadhaa kabla ya uchaguzi ndo nilikuwa upande wake?

Ninaweza kuandika uzi kama huu kama niko upande wake?

Seriously???

Hahah na umesema ukweli mzee baba.
Mimi niliyeandika hivi mwezi June ndo nilikuwa upande wake??

Turnout ya mwaka huu ilikuwa juu kidogo.

Na moja ya sababu ni chuki dhidi ya Trump.

Niliwahi kuandika uzi humu kuhusu akili ya Trump....huenda ndo Rais zuzu kuliko marais wote wa Marekani kuwahi kutokea.
Mnafiki wewe...Si ulisena Kibabu Biden kinapoteza muda??? Au sio wewe
 
Back
Top Bottom