Joh Makini, sitokusamehe kwa kutuharibia mziki wetu Nako 2 Nako Soldiers

Joh Makini, sitokusamehe kwa kutuharibia mziki wetu Nako 2 Nako Soldiers

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Salamu zikufikie,

Unajiita Mwamba, ni kwa ujanja wa nje uliofanikisha kumzima mpinzani baada ya kuangushwa vibaya ulingoni.

Wadau na walio timamu watakumbuka hili, Joh Makini na timu yake River Camp Soldiers. Si ajabu usikumbuke ngoma yoyote kali kutoka kwenye kundi hili, kama ipo tusaidiane.

River Camp Soldiers ikiongozwa na Joh Makini, na mdogo wake Nikki, Bonta na wengine kama wapo (wasiojulikana), haikuwa na maajabu kama kundi.

Sana sana ilitumika kumbeba Joh kwa kiasi kikubwa, huku akiibatiza majina mbalimbali kwa vipindi tofauti (Mfano Good Music Family ‘GMF’ hadi Ngumu Nyeusi ‘WEUSI’) lakini yote haikufua dafu.

Wakati huo akichezea ‘vitasa’ vikali kutoka kundi hasimu Nako 2 Nako Soldiers, likiongozwa na Lord Eyez, G Nako, Bou Nako na Ibra da Hustler.

Kama kundi walikuwa wakitamba kwa kila ngoma waliyoachia, walitamba na hakika walikosa upinzani, labda kwa mbaaali Kikosi Cha Mizinga ya Kalapina.

Kwa uchache tu nikukumbushe ngoma kali kama Ndo Zetu, Mchizi Wangu, Hawatuwezi, Bang! Hapo sijasahau Mchizi Wangu Remix, ni kwa vile nimeahidi kutaja mawe kwa uchache.

Joh Makini aliona kabisa mazishi haya hapa, ikabidi atumie ujanja na akili kubwa ili kujipatia ushindi wa mezani, nje ya uwanja.

If you can’t beat them, join them. Ndiyo turufu aliyotumia Joh Makini.

Akavizia kipindi Lord Eyez yupo ‘high’ kwa mihadarati, akamsajili kiungo wake mchezeshaji G Nako. Na kwa fitina nyingi kuhakikisha timu zinaungana ili awe kiongozi.

Hebu fikiria, Nako 2 Nako imesambaratika kipindi ambacho imepata ‘lebo’ Bongo Records kwa Godfather Majani, hii inawezekenaje!

Na hapo tayari wamesharekodi album nzima, wimbo pekee uliosikika kutoka album hiyo ni HAWATUWEZI, fikiria ngoma kali kiasi gani zimefia studio kwa Majani!

Sasa we jamaa Joh Makini, Mwamba, umeua ushindani kisha ufurahie tu kuwa kiongozi wa kundi lisilo na maana!

Hizi nyimbo zenu uchwara Wapoloo sijui Gere sijui Arosto kabisa unaona ni hadhi ya Lord Eyez au unamkomesha kijanja!

Nako 2 Nako tunawadai ngoma kali, lawama zote ni kwako Mwamba, binafsi sitokusamehe!

Bring back our NAKO SOLDIERS!
 
Kwani Lord izy si ameshapona? Shida ikowapi Sasa kuanza kuporomosha mangoma Kama solo arist?

Nako ilijijenga na kupata nguvu kama kundi, solo projects zao hazina moto... Joh na wenzake walikuwa vizuri kwenye solo, ila kama kundi ni kinyume!
 
Mkuu fatilia vizuri mziki wa Chuga. Joh aka Rapture hajahusika kuiua Nako. Mtu alieharibu Nako ni Ibra da Husler.
Mziki anausikiliza tuu kwenye radio. Hajui zaidi ya hapo.

River camp soldiers halikuwa kundi rasmi la muziki bali kijiwe ambacho joh alikuwa anapenda kukaa. Kiko chini ya ras omega.

N2N ilipotea baada ya Ibra na Eyz kuwa mateja. Gnako ndio ikabidi awe kwenye kampani ya Weusi.
 
Hebu elezea kiundani, vinginevyo tutajua tu umetumwa kumtetea Mwamba!

Kwanini nimtetee? na ili iweje?

Mziki wa Chuga huujui vizuri historia yake. Ibra alijitoa N2N mapema tu wakiwa kwenye harakati za kuzindua album ya Hawahemi street huslers vol 2. Baada ya kujitoa ndio utata ukaanzia hapo. Mnako Lord akakolea kwa Ray C na kwa stress akafundishwa kula kiariri na Ray C (Japo wengi wanasemaga Lord ndio kamfunza Ray C unga) Baada ya hapo ndio Joh akaingilia kati kumchukua G na mwishowe kuunda weusi.
 
Mziki anausikiliza tuu kwenye radio. Hajui zaidi ya hapo.

River camp soldiers halikuwa kundi rasmi la muziki bali kijiwe ambacho joh alikuwa anapenda kukaa. Kiko chini ya ras omega.

N2N ilipotea baada ya Ibra na Eyz kuwa mateja. Gnako ndio ikabidi awe kwenye kampani ya Weusi.

Ukisema historia hata Nako 2 Nako halikuanza kama kundi rasmi, ilikuwa dojo la wapiga nondo (mazoezi).... lakini baadae likawa kundi la mziki.

Ni kweli nasikiliza mziki redioni tu, nina haki ya kupenda kizuri bila kujali huko jikoni kuna niaje!

Si ukweli kuwa Joh alichezea kila raundi.?
 
Kwanini nimtetee? na ili iweje?

Mziki wa Chuga huujui vizuri historia yake. Ibra alijitoa N2N mapema tu wakiwa kwenye harakati za kuzindua album ya Hawahemi street huslers vol 2. Baada ya kujitoa ndio utata ukaanzia hapo. Mnako Lord akakolea kwa Ray C na kwa stress akafundishwa kula kiariri na Ray C (Japo wengi wanasemaga Lord ndio kamfunza Ray C unga) Baada ya hapo ndio Joh akaingilia kati kumchukua G na mwishowe kuunda weusi.

Umechambua vema, lakini hapa hatuongelei mziki wa chuga... hawa walishafika kwetu huku mjini.

Mziki wa chuga achia kina Chindo, Umbwa na wale mamong’o ya ara!
 
Back
Top Bottom