Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 19,484
- 38,416
Na mitaala yetu ya elimu inawakaririsha watoto wetu jambo la kijinga kama hili kama vile ni kitu chenye mantiki kinachoweza kuwasaidia wanetu kubuni rockets za kwenda Mars.Ni maajabu sana. Kulingana na machapisho mbalimbali mlima maarufu unaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 3 million iliyopita hakuna mkazi yeyote wa aliwahi kujua kuna mlima mrefu kaskazini mwa Tanganyika hata wale wakazi wenyewe hawakujua š.
Johannes Rebmann.
Mlima Kilimanjaro uligunduliwa na bwana Johannes rebmann ambaye alikuwa mmissionary kutoka Ujerumani mnamo 1848.
Kutokana na bwana huyo aliyekuwa na mwenzake aitwaye Johann Lidwig Krapf, habari ziliweza kusambaa maeneo mengi ya ulaya kuwa kuna mlima wenye kilele cha barafu karibu sana na ikweta. Lakini habari hizo hazikuaminika kwa watu mpaka miaka kadhaa baadae.
Ujinga kama huu unapaswa kuondolewa kwenye mitaala yetu.