John Bocco huwa anaingizwa kufanya nini kwenye mechi za kimataifa?

John Bocco huwa anaingizwa kufanya nini kwenye mechi za kimataifa?

Kuna washabiki hawajui mpira wanafuata mkumbo tu..wamesahau kule Malawi alichokifanya.
Mkuu malawi alifanya nini? Maana nakumbuka alikutana na mpira akafunga. Game za cafcl zinataka mapambano ambayo bocco hayawezi tena.
 
Kuna issue nyingine zinahitaji uzoefu wakuu,Bocco ni mzoefu huwezi mlinganisha na hao madogo wa juzi!
 
Boko anabidi ajitambue na astaafu sasa kwa heshima, kuliko anavyong'ang'ania kuendelea kucheza atakuja kuachwa kwa aibu.
Aliyoyafanya yanatosha ajikite kwenye kusomea ukocha kama bado anataka kuwa kwenye familia ya mpira.
 
Kweli kabisa. Anaweza kufanya kosa moja akapoteza heshima yake maana mashabiki hawatabiriki.
 
Simba inatakiwa isajili washambuliaji, vinginevyo bocco ataendelea Tu kucheza. Nadhan viongozi wamsaidie mwalimu. Ila Kwa sasa options za mwalim ni ndogo Sana. Akikosa kitu anachotaka Kwa kiyombo anabakia na bocco Tu.
 
Amefunga baada ya kukutana na mpira kwenye njia. Game za sasa zinahitaji mwili flexible na wenye nguvu. Magoli rahisi kama yale hayatakuwepo huko mbele tunakoenda.
Magoli mangapi ya Haland sio ya kukutana na mpira?
 
Mkuu malawi alifanya nini? Maana nakumbuka alikutana na mpira akafunga. Game za cafcl zinataka mapambano ambayo bocco hayawezi tena.
Nani mwingine alikutana na mpira kati ya Wachezaji wote kumi?.

Mashabiki tuache tabia ya kusimanga, Bocco ni Mfungaji na ameshapruvu hilo....ni jukumu lao hao wengine nao waoneshe kama anavyofanya Firi.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Nani mwingine alikutana na mpira kati ya Wachezaji wote kumi?.

Mashabiki tuache tabia ya kusimanga, Bocco ni Mfungaji na ameshapruvu hilo....ni jukumu lao hao wengine nao waoneshe kama anavyofanya Firi.
Mkuu mechi za cafcl ni nadra sana kupata magoli kwa staili hiyo. Vijana waliopo wapewe nafasi.
 
Simba inatakiwa isajili washambuliaji, vinginevyo bocco ataendelea Tu kucheza. Nadhan viongozi wamsaidie mwalimu. Ila Kwa sasa options za mwalim ni ndogo Sana. Akikosa kitu anachotaka Kwa kiyombo anabakia na bocco Tu.
Bora kyombo apewe nafasi apate uzoefu kuliko kumweka bocco anayepoteza mipira na hata kukaba hawezi.

January inatakiwa watafute striker, beki wa kati na kiungo mkabaji.
 
Bocco anayo rekodi nzuri pale Simba na hakika mchango wake ndani na nje ya uwanja hauwezi kusahaulika.

Ila kwasasa ni vizuri uhalisia ukazingatiwa, John umri umemtupa mkono. Mechi za kimataifa zinataka kasi na umakini mkubwa.

Leo amepoteza mipira mingi sana kwa dakika chache alizocheza. Atumike kwenye michuano mingine lakini sio CAFCL.
Simba ushkaji mwingi,,,,Kila nabii na zama zake...zama za bocco zmekwsha
 
Tatizo lenu mnaongea bila kujua ukweli wa mambo. Pale Simba Boko ataendelea kucheza mpaka anaondoka au kustaafu. Sio kila mchezaji anaweza kubeba hirizi, hawa majasiri wapeni kongole ..

Boko asipocheza, makaburini utalala wewe? 😅
 
Utopolo embu mtuache...hangaikeni na Li timu lenu.

Li timu lenu Lina Miaka 24 Halijaingia Makundi CAF Champion.....!

Kuna Mizee pale inakula Pensheni Ya Bure kbs MNAIFUGA.. !
Juma Shabani.
Kisinda
Aucho
Bangala
Yanga ikitaka mafanikio Hawa wote timua Leta damu Changa.....!
Mizee hii bado ukikutana nayo inakubandua, means michezaji yako ni Mizee zaidi yao
 
Back
Top Bottom