Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #41
Tabby,Hii makala inagusa moyo sana na inafungua ufahamu mkubwa kabisa juu ya changamoto za maisha, uadilifu, malengo, uvumilivu lakini pia masuala ya uzazi na ulezi wa watoto, na changamoto mbali mbali ambazo binadamu zinamkuta na namna ambavyo hatakiwi kukatishwa tamaa.
Major General Walden, pengnie maisha ya kutengwa na wazazi akiwa mtoto mdogo, yalimjgengea tabia ya kujitegemea akiwa katika umri mdogo na kufahamu kwamba ili mtu apate anachokihitaji katika maisha ni lazima afight. Bila hivyo, kitendo cha kubaguliwa na kutiliwa mashaka uzalendo na uaminifu wake kwa jeshi, kulingana na rangi yake au tabia za mzee wake, tayari kungemvujna moyo na pengine hata angeamua kufuta mkondo mwingine wa maisha. Huyu kijana anafundisha mengi mno kwa jina za matendo.
Hata hivo, ninatamani sana habari kama hizi, zingefuatiliwa na kuandikwa kabla hajafariki ili kumsikia kwa upande wake anasema nini. Yako masuala mengi sana ya kujinfunza kutoka kwa atu kama hawa. Si kwa Watanzania ama binadamu wa kawaida, bali pia upande wa serikali namna ya kuwaenzi kwa dhati badla ya kisiasa.
Major General nimeongea naye mara kadhaa nyumbani kwake Iwambi. Nilikuwa nikipitia nyumbani kwake mara nyingi nikitokea Lusaka kwa gari na alikuwa mkarimu na mwenye ushirikiano na watu sana. Penginge historia yake hii ndiyo imepelekea kumfanya awe mtu wa kuthamini watu, asiyejibagua na mwenye upendo.
Kuna mengi ambayo kama yangeandikwa pia kwa kumhoji yeye, hii habari ingelikuwa na upande wa pili ambapo pengine umma ungelifahamu Serikali yetu inawaenzi vipi mashujaa wetu wanapokuwa hai baada ya kumaliza majukumu yao. Kwa kugusa mioyo na fikira, ninahakika maisha ya Major General huyu, yangetoa mwelekeo mpya na makini juu ya kuenzi wataafu wetu wanaoishi maisha ya majuto.
Ahsante kwa makala nzuri. Karibu na zingine utushirikishe.
Ahsante sana.
Mimi nataka kupata jina la mtu aliyeandika taazia/makala hii lakini bado sijafanikiwa.