John Butler Walden (1939 - 2002) a.K.a ''Black Mamba''- A legend in the Tanzanian army (author unknown)

John Butler Walden (1939 - 2002) a.K.a ''Black Mamba''- A legend in the Tanzanian army (author unknown)

Wengi tunamkumbuka maj gen walden na kuenzi mchango wake. wala hakuna shaka hakika alikua askari bora kabisa.
 
Tanzania ni yetu sote. Tunapenda kusahau hilo. Hakuna dini wala race au kabila litakayoitaifisha mama Tanzania kama hodhi yake binafsi. Tuijenge Tanzania kwa watanzania
Tangawizi,
Tunatamani sote iwe hivyo lakini hali haipo hivyo.
 
Hivi kuna Fritsch aliyeoa/ kuolewa kwa Nyerere? Kuna mjukuu mmoja wa Nyerere alikuwa anaitwa Judith Fritsch.
 
Mi nilisoma na mwana hivi anaitwa Paulo john pale iyunga technical mbeya Ila alinitangulia madarasa kama mawili mbele alikuwa chotara chotara hivi .
Siku ya maafali mzee na mkewe walikuja
Mbona huyo Paul John simkumbuki katika watoto wake!au alikuwa wa mchepuko.
Watoto ninaowafahamu kama jirani akiwa Mwambata au Military Attache nchini Uingereza ni Elizabeth, Mary, Stella, Adolf na Stanley,nadhani Adolf ni marehemu ila hao wengine sijui wako wapi.
 
Ngongo,

Kiwelu si alikuwa Luteni Generali mpaka anastaafu hakuwahi kuwa Generali kamili kumbukumbu zangu zinaniambia.Ila nakumbuka utawala wa mkapa aliwapandisha vyeo vya U-Jenerali Sarakikya sikumbuki na nani wakiwa wameshastaafu!
 
Kiwelu si alikuwa Luteni Generali mpaka anastaafu hakuwahi kuwa Generali kamili kumbukumbu zangu zinaniambia.Ila nakumbuka utawala wa mkapa aliwapandisha vyeo vya U-Jenerali Sarakikya sikumbuki na nani wakiwa wameshastaafu!

Mkuu Jidu Kiwelu ni General sawa na wakuu wa majeshi (CDF) General Mirisho Sarakikya, Lt General Abdallah Twalipo,General David Musuguri,Genaral Mwita Kyaro,General Robert Mboma,General Mwita Waitara & General Davis Mwamunyange.

Ukiitazama wakuu wote wa majeshi wastaafu na wa sasa ni majeneral kasoro Lt Gen Abdallah Twalipo.Kabla ya vita ya Uganda wakuu wa majeshi hawakuwa full General.Wakati General Mirisho anaondoka kama CDF alikuwa Brigadier alikujapandishwa cheo na Mkapa tena akiwa Balozi kashaondoka jeshini nadhani madhumuni yalikuwa kumlinganisha na wakuu wa majeshi wa kipindi hicho ambao walikuwa full General au four star general ukipenda.

Issue ya General Kiwelu ni tofauti kidogo,yeye ni full General au four star General pekee katika historia ya JWTZ ambaye hakuwahi kuwa mkuu wa majeshi CDF.
 
John Barton Walden
1466586669101.jpg
 
Tabby,

Nakumbuka kituo cha ITV walifanya safari ya kumtembelea Generali Walden Mkoani Mbeya na kufanya naye mahojiano. Tafadhali waweza kutafuta clip/video ile kwa hifadhi ya historia ya Mhe. huyu.

Mimi binafsi wakati nikisoma secondary pale Tabora, tulikuwa tunatabia ya kwenda kucheza music pale 'Muungano Mess', hall hili lilikuwa linamilikiwa na JWTZ na maafisa wengi walipenda sana kustarehe pale ndipo nilikuja kumfaham General Walden.
 
Nalikuwa namkubali sana huyu commander JB Walden,nilikuwa nawafahamu watoto wake Margreth,Mary,Stella,Stanley na Adolf na mama yao, Sijui wako wapi kwa sasa.
Stanley na Adolf pamoja na dada yao wa mwisho Chuchu wapo Uingereza sister wao mkubwa Mariam alikuwa anaishi Tabora akahamia Mwanza, sijui kama bado yupo huko.

Hii familia nimeifahamu kupitia kwa marehemu Mzee Adolf, babu yao hawa kuna baadhi ya watoto wa mzee Adolf ni rafiki zangu Tony na Steve.
 
Aka kastori nakatamani sana kukajua ila hii lugha kidogo inanipotezea mudi ya kusoma ivi akuna alionayo kwa kiswahili
 
Such a great history... Walden, one among great historic figure of our nation
 
Nalikuwa namkubali sana huyu commander JB Walden,nilikuwa nawafahamu watoto wake Margreth,Mary,Stella,Stanley na Adolf na mama yao, Sijui wako wapi kwa sasa.
Mjane wa JBW (Angel Adolf) yupo Dar.
 
Back
Top Bottom