Licha ya kupewa kibali cha kufanyia mikutano ya hadhara kwa sharti la kulinda amani, lakini Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA ameonekana kushindwa kutumia uhuru aliopewa na sasa ameanza kuamuru vijana wake kuanza kuwapiga wananchi wanaokwenda kuwasikiliza ajenda zao mfu za No Reforms No Election.
Kwanza hali ya hatari ya ilianza kuonekana kwenye mkutano uliofanyika Singida, ambapo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Heche aliwatishia wananchi waliokua na mawazo kinzani kuhusu Hoja yao ya No Reforms No Election na Heche alitamka kauli ambayo ingeweza kuleta maafa makubwa mno kama Jeshi la Polisi lisingekuwepo maeneo ya karibu pale.
Heche alitamka maneno yafutayo "Nyie vijana hapo mnajifanya mnapinga No Reforms No Election, nitawatuma vijana wetu wawafinye hadi mpotee"
Kauli yake hii ilizua taharuki kubwa kwenye mkutano wake wa Singida ambao kwa asilimia kubwa wananchi walikua hawataki ajenda ya No Reforms No Election mpaka pale Polisi walipoingilia kati kunusuru zahma kutokea.
Lakini Chizi huwa hasahau jalala lake, leo tena akiwa mkoani Tabora John Heche ameamuru vijana wake, kuwapiga wananchi waliokwenda kusikiliza hoja zisizo na uhalisia za kuzuia Uchaguzi Mkuu, akaagiza vijana wake kuwarushia mawe wananchi, ambapo mpaka muda huu kuna wananchi zaidi 25 wamejeruhiwa kwa sababu ya kupokea kichapo kwa sababu ya amri ya John Heche.
Umefika muda John Heche aseme wao kama CHADEMA hawawataki Watanzania waende kusikiliza hoja zao zilizokufa, ili waepukane na vichapo kwa sababu ya amri anazozitoa maana kama ni hivyo sasa kila anayekwenda kwenye huo mkutano hana uhakika kama atarudi na Ngeu au kupata ulemavu.
Umesikiliza hii, Samia anatafuta watu KWA NGUVU wakuhudhuria mikutano yake huko Simiyu. HAUZIKI, HAKUBALIKI ni huzuni kwa kweli.
SAUTI INAYOSIKIKA KWENYE HIZI VIDEO NI SAUTI YA MKUU WA WILAYA YA MASWA.
"Idd Amin Mama anatarajia kuwa na ziara Mkoa wa Simiyu kuanzia June 16, 2025 sasa hapa Mkuu wa Wilaya alikuwa kwenye kikao na watumishi wa umma akiwaelekeza maagizo aliyopewa na Mkuu wa Mkoa Simiyu Kenan Kiongosi ili kufanikisha ziara ya Idd Amin Mama kwenye Mkoa wao.
Kenan Kihongosi ameamuru kila Wilaya iliyopo ndani ya Mkoa wa Simiyu ichangie Ng'ombe 136, magunia ya mchele,maharage na fedha taslimu.
Kenan Kawaambia maDC kwamba wanaotakiwa kutoa izo Ng'ombe, magunia ya michele, maharage na fedha taslimu ni WADC yani Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu, Watendaji Kata, Maofisa wa Kata, Maafisa Ugavi, Waganga Wafawidhi n.k
Halafu kila Wilaya ya Mkoa wa Simiyu wameambiwa wakusanye Vijana 15,000 na kuwaweka kambini kusubiri mikutano ya Idd Amin Mama wakajaze viwanja vya mikutano,
hizo pesa Taslimu ndo zitakuwa zinatumika kukodisha mafuso ya kuwabebea hao vijana 15,000.
Na kwenye izo kambini ndo watakuwa wanakula hao ngo'mbe na hiyo michele na mandondo halafu hao Vijana watakuwa wanazunguka kila wilaya atakakokuwa anaenda Idd Amini Mama lengo ni mikutano isikose watu wanataka ionekane iko na nyomi ya kutosha.
Ukisikiliza Mkuu wa Wilaya ya Maswa anaelezea jinsi ambavyo waliwahi kukosa watu kwenye moja ya mikutano yao sasa anasema hawataki aibu ijirudie, anawaambia kwamba kipindi chote ambacho Idd Amin Mama atakuwa Simiyu ofisi zote za Serikali kazi zitasimama na watumishi wa Umma wote lazima waende kwenye Ziara ya Idd Amini Mama eti wao ndo wanapaswa kuwa walinzi wa kwanza wa Idd Amin Mama.
Hii ni dalili ya kwamba Idd Amin Mama hakubaliki kabisa kwa Wananchi ndo maana Serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wanatumia nguvu mpaka kulazimisha watumishi kutoa michango ili kupata watu wakujaza Mikutano yao maana wanajua wakisubiri watu waende uwanjani kwa hiyari yao hawatotokea".
CCM ipo kwenye haatua za mwisho kabisa kupotea kama ilivyokuwa kwa KANU huko Kenya. NO REFORMS, NO ELECTION 2025.