Kwa jitihada zilizotumika CCM waliamini upinzani upinzani umekwisha, baada ya huu uchaguzi kuna watafukuzwa kazi kutokana na kutoa ushauri batili wa kuuzima upinzani hapa nchini.
[/QUOT
Mimi wasiwasi wangu ni endapo CCM itashinda tena ,patakua na ukiukwaji mkubwa sana wa haki za watu mara dufu ya awamu ya kwanza.
Kama wamesema wazi kuwa hawatanii kwa maeneo yote yatakayowanyima kura hawatapewa hata maji ya kunywa achilia mbali huduma zingine kama tiba n.k.
Tumuombe Mungu yasije yakatokea yale ya Kule Iraq kwa maeneo ya wapinzani wa Sadam enzi hizo.
Sijasikia popote mgombea wa CCM akizungumzia suala la haki na usawa. Hii ni hatari sana.
Vijana wengi wanaweza wakafungwa na kupotea kama sisimizi mana wanaonekana kuwa wanaunga mkono upinzani. Maendeleo ni ya walipa kodi wa CCM tuu. Wapinzani hata mvua kama sio Mungu hawatapata. Kama jua lingekuwa ni mali ya CCM au lingekuwa limetengenezwa kwa juhudi za Mkubwa wa nchi basi wapinzani wangepewa jua la saa nane mchana masaa yote ili wakome kupinga pinga maendeleo.
Hivyo ni vyema wapinzani wamshukuru sana Mungu anayetoa mvua na jua kama anavyopanga yeye mwenyewe.