John Heche: CHADEMA ina wanachama milioni nane

John Heche: CHADEMA ina wanachama milioni nane

Mbunge wa zamani wa Chadema jimbo la Tarime amesema hivi sasa chama hicho kimepata mafanikio makubwa kutokana na kampeni ya Chadema digito inayoendelea. Amesema hayo leo tarehe 4 Disemba 2021 kupitia kipindi cha Medani ya Siasa cha Star TV kinachoendeshwa na Odemba. Amesema kupitia kampeni hiyo chama hicho kimesajili wanachama milioni nane.

Aidha amesema kutokana na kuwa na wanachama hao milioni nane ambao wanachangia Shs. 500/= kwa mwezi kila mmoja, Chama kinapata Shs. Bilioni nne kwa mwezi.

Fedha hizo zitakiwezesha Chadema kuendesha shughuli za kiofisi na kujenga ofisi mpya katika majimbo mbalimbali.
Chadema is next level, ujumbe ukamfikie kingai,Mahita, Good lack, Juma nne, kamati ya siasa TOKA magogoni, mwenyekiti wa ccm,katibu mkuu, na mwenezi, wanaccm wote, na kamati zote za roho mbaya,

Watujua wanajua kumbe hawajui,
 
Hivi wanaccm kama kina lowasa, sumaye, nyalandu na wengine walivyohamia chadema nao walinunuliwa na chadema mbona wanachadema wanaohamia ccm wanaonekana wamenunuliwa ila wanaccm wakienda chadema hawaonekani wakinunuliwa hizi propaganda za kinafiki
 
Wanachana milioni 8 lakini ajabu walipoitisha maandamano baada ya uchaguzi hakutoka ata mtu mmoja., ata Tundulisu kiongozi wa upinzani hakuwa jasiri., hakutokeza mahali popote siku ile lakini pia sasa Mwenyekiti wa Chama yupo jela kwa kile wanachodai kabambikiziwa lakini hakuna chochote kinachotokea kwa hao wanachama milioni 8 kwa Mwenyekiti wao ana anaendelea kusota jela.,
Hata Zambia utawala na wafia tumbo walibeza Sana Rais wao mpya, leo wanajitekenya na kucheka wenyewe, hakuna jipya chin ya jua
 
Hivi wanaccm kama kina lowasa, sumaye, nyalandu na wengine walivyohamia chadema nao walinunuliwa na chadema mbona wanachadema wanaohamia ccm wanaonekana wamenunuliwa ila wanaccm wakienda chadema hawaonekani wakinunuliwa hizi propaganda za kinafiki
Kama wewe ni mchumia tumbo utaonekana umenunuliwa tu kwa sababu utapewa nafasi ya kulipwa mshahara, lakini kwa wanaojiweza wananunua nafasi za uongozi!
 
Billioni 4 kwa mwezi ni fedha nyingi sana wajenge ofisi ya makao makuu sasa kama kweli.


lakini je; wanachama watalipia hiyo ada ya uanachama?
Tunajenga kwenye bongo za wamachama kwanza. Achana na majengo
 
Mtekwe na nani nyie na nani awaibie kura chadema imekosa sera na mvuto kwa wananchi mmebakia kutafuta huruma za wananchi na mataifa ya mabeberu hizi za kutekwa, kuibiwa kura, kuuawa ni propaganda za chadema baada ya kushindwa uchaguzi
Akili yako haina akili
 
Nyumbu millioni 8
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Dah!
tapatalk_1555146678239.jpg
 
Polepole anaulizwa mikutano ya siasa imezuiwa kwa sheria ipi anasema nchi haiongozwi kwa katiba na sheria tu bali pamoja na matamko, amri na utamaduni!

Pole pole hana jipya ndiyo maana hata sikutaka kumsikiliza ,sasa nchi haingozwi kwa sheria bali matamko sasa kila kiongozi akitoa matamko itakuwaje? Pole pole ni KANJUNJU.
 
Back
Top Bottom