Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kiukweli kabisa hata kwa macho ya nyama tu, John Heche hana haiba, muonekano, hekima wala busara ya kuwa kiongozi wa ngazi ya juu mathalani kuwa makamu mwenyekiti wa chadema Taifa.
Si mtaratibu wala mstaarabu mwenye subra, ni mtu wa vurugu na fujo, huenda ni zaidi ya kelele na mdomo wa anaemuunga mkono nafasi ya uenyekiti wa chadema Taifa.
Katika kujieleza kwake, kinachojidhihirisha mwanzo kabisaa wa maelezo yake ni kiburi, kisasi na ujeuri wa kiwango cha juu sana dhidi ya viongozi wa sasa wa chadema hususan mwenyekiti wa chadema Taifa. John Heche anajaribu kujieleza na kujipambanua kwa kufokafoka kwa hisia kali, akadhani eti ndio ataonekana jasiri au kwamba yeye ndie mwenye uchungu sana na chadema kuliko wengine, kumbe waerevu wenye hekima na busara wana muona kama mtu anaetumia vitu vya kusisimua akili na kumpa ujasiri wa kujieleza bila woga au kujali macho ya hadhira inayomskiliza.
Kisiasa
Maelezo, mtazamo na muonekano wa Heche vinatia shaka na vinamfanya aonekane kama vile anapitia changamoto au wakati fulani mgumu, na hivyo anaonekana kama mtu ambae si mwema na asie na dhamira au nia njema kwa chadema.
Siasa, hulka na tabia ya uzungumzaji wa John Heche, unashabihiana na unaendana na ule wa Tundu Lisu, na kwahiyo kuna uwezekano mkubwa wagombea hawa wakaungwa mkono na watu wa vurugu mithili ya majambazi wa kisiasa, na kusababisha wenye hekima na busara walazimike kuhama kambi kukwepa au kukimbia vurugu za Lisu na Heche uongozini.
Kwa kifupi
John Heche ameshusha hadhi na kiwango cha kuaminika kwa Lisu miongni mwa wanao muunga mkono.
Lakini pia chemistry ya Heche na Lisu ni kitisho kwa demokrasia, msingi wa kuanzishwa kwa chadema na uhai wa chadema kwenye medani za siasa za Tanzania.🐒
Mungu Ibarki Tanzania