Tetesi: John Heche kahujumiwa na chama chake CHADEMA

Mathayo Fungo

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2018
Posts
319
Reaction score
511
HUJUMA ALIZOFANYIWA HECHE NI AIBU KWA CHAMA KINACHOJIITA CHA DEMOKRASIA:

Uchaguzi wa Mwenyekiti Kanda ya Serengeti umetamatika huku Heche akifanyiwa hujuma, rafu na figisu za kila namna kuhakikisha kuwa anaangushwa na Esther Matiko.

Ni bahati mbaya sana kuwa chaguzi hizi za Kanda zimetawaliwa na hujuma za kila aina, rushwa za kila aina kuanzia za pesa hadi zile za ngono. Naamini Msajili wa Vyama vya Siasa nchini atashirikisha vyombo husika kuchunguza hujuma hizi.

Watu wananiuliza imekuwaje shujaa Heche aangushwe? Bahati nzuri Mimi niko jikoni na leo nitawaeleza peupe, Heche hajaangushwa kidemokrasia iko hivi:

1. Urafiki wa Heche na wapinzani wa Mbowe:

Kwa wale msiojua ni kwamba Heche ni rafiki mkubwa wa Cecil Mwambe, Joseph Selasini Saed Kubenea na Anthony Komu. Mbowe amekuwa akimuona Heche kama kitisho (threat) katika utawala wake hususani kutokana na misimamo mikali isiyoyumba ya Heche ambapo amekuwa akimkosoa Mbowe kwenye vikao vya chama bila woga. Mbowe akaamuru kuwa wajumbe na Msimamizi wa uchaguzi kuwa wahakikishe Heche aangushwe kwa gharama yoyote ile.

2. Ni Kuhusu uhusiano nyeti sana wa kimapenzi baina ya Matiko na Salum Mwalimu. Hili naliweka kiporo ila figisu zikiendelea nitapasua mbarika. Ila kiufupi tu ni kwamba Mwalimu ana Mtoto na Matiko waliozaa naye. Hivyo licha ya Mwalimu kupewa maagizo mazito na Mbowe ili aende Serengeti kuhakikisha Heche anachinjiwa baharini ni kwamba pia Mwalimu ambaye ni NKM-Zanzibar alitumia mwanya huo kuhakikisha mpenzi wake au ukipenda kimada kinapata ulaji. It was a win win situation kutwkeleza maagizo ya Mbowe ya kumchinjia mbali Heche lakini wakati huo huo akihakikisha anatumia fursa hiyo kuhakikisha anamfurahisha Matiko.

Na tayari Mbowe alishatoa amri kuhakikisha kuwa endapo Heche atajaribu kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa adhibitiwe mapema hata kabla ya Uchaguzi wenyewe.

Hivyo urafiki wa Heche na mahasimu wa Mbowe ndani ya chama ndio uliomponza na kupelekea kuadhibiwa kwa amri ya Mwenyekiti.

Heche ni miongoni mwa Wabunge wanaomuunga mkono Cecil Mwambe kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa na hapo ndipo uhasama zaidi kati yake na Mbowe ulipoongezeka.

Na kwa taarifa tu ni kwamba tayari Mbowe ameshasuka mkakati kuhakikisha kuwa akifanikiwa kufanya uchakachuz na kuwa Mwenyekiti kwa awamu ya tano basi John Heche, Joseph Selasini, Anthony Komu, Cecil Mwambe na Saed Kubenea watakatwa kwenye mchakato wa Kura za maoni.

Hii inasikitisha sana, sijawahi kuona Uchaguzi wa kipumbavu na kijinga kama huu. Yani hata CCM kwa sasa wana ahueni ya kidemokrasia kuliko sisi CHADEMA.

Misingi ya demokrasia haipo tena ndani ya CHADEMA, Mbowe ndiye amri, yeye ndiye Katiba na lolote atakalo anahakikisha linafanyika. Watu waejeruhiwa ndani ya CHADEMA wengine wameamua kunyamaza tu.

Ukiongea vizuri na watu walioamua kuondoka CHADEMA unaweza kuwaomba msamaha kama uliwatukana. Mbowe huyu ambaye baadhi ya vijana wameamua kumuabudu na kumsujudia huku wakilamba viatu vyake ili MATUMBO yao yashibishwe ndiye anaenda kuizika CHADEMA. Amini usiamini 2020 CHADEMA hii chini ya Mbowe itakuwa DHAIFU sana kuliko hata TLP ya Mrema.

Mbowe amegeuza CHADEMA kuwa mali yake. Mali za chama amegeuza ni zake. Anyway nikipata wasaa nitaeleza namna Mbowe anavyokifisadi chama na kujineemesha huku akitutumia vijana kama greda lake la umchimbia barabara ili aendelee kuneemeka.

Kama ulikuwa unajiuliza imekuwaje shujaa Heche aangushwe Serengeti basi UKWELI MCHUNGU ndio huo kuwa nguvu ya ngono na na urafiki wake na kina Selasini, Mwambe, Kubenea na Komu ndivyo vilivyo mgharimu.

Level ya udikteta wa Mbowe aliyofikia ndani ya CHADEMA hana legitimacy ya kumuita mtu yeyote yule kuwa ni Dikteta.

Kwa upuuzi huu tunaoufanya CHADEMA hatuna legitimacy ya aina yoyote ile ya kukashifu hujuma za uchaguzi wa Serikali za mitaa. Hivi kwa upumbavu huu unapata wapi ujasiri wa kumkashifu Waziri Jafo na Mwita katika uchaguzi wa SM?

Dawa chungu ndiyo inayoponesha, UKWELI MCHUNGU unauma lakini UKWELI hauna mbadala.

Baadae nitaanika hujuma alizofanyiwa Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini katika uchaguzi wa Mwenyekiti Kanda ya Kaskazini dhidi ya Godbless Lema.

Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
 
Kuna equal chances za hii makala kua kweli au isiwe kweli!

Yaani 50% yaweza kua kweli au 50% hii kitu ikawa ni pumba plus pumba!

Maneno haya ni common sana kwenye mahali panapokua na power struggle!

Tushayazoea na ni kawaida!
 
Mleta mada umezungumzia zaidi mahusiano kati ya Mbowe na Heche bila kufanikiwa kueleza figisu zilizofanywa. Nikutahadharishe, hapa watu wanataka kusikia kama kura zimeibwa au zina kasoro, Heche kaenguliwa kwa hujuma, hongo zimetolewa na Matiko au kambi yake kushawishi wapiga kura na mambo kama hayo.

Shughuli za siasa ni za ushawishi. Kama wajumbe wengi wako upande wa Matiko kupitia ushawishi wa Mbowe na Mwalimu - hakuna ubaya kisiasa.

Katika hili ulipaswa kuelezea jinai iliyofanywa na au Matiko, au Mwalimu au Mbowe. Kama hutaweza kusema hayo - jaribio lako la kuonesha Heche kafanyiwa hujuma litabaki kuwa unsubstantiated allegations. Na kama wewe uliye jikoni ndio una uelewa huu - vipi walio mbali??
 
Kwanini mna viherehere sana wakati Heche mwenyewe jana/juzi ile ile alikubali matokeo na kumpongeza mshindi?, kama pangekuwa na tatizo lolote nilitegemea Heche ndio awe wa kwanza kulizungumzia, sio wewe mleta mada na wenzio mliotumwa kuivuruga CDM kupitia kwa msajili.

Halafu ulivyokosa akili unamwambia msajili wenu aiangalie CDM eti atume watu wake kuichunguza, na kwakufuata matakwa yenu mabosi wake kweli katoa tamko, eti anafuatilia uchaguzi wa CDM!

Hivi nikuulize wewe mleta mada na wenzio hapo Lumumba, kama pamoja na askari mlionao wanaowasaidia kuiba kura, tume ya uchaguzi inawasaidia, wakurugenzi wa majiji na manispaa wanawasaidia, wakuu wa wilaya na mikoa wanawasaidia, kwanini bado mnawasiwasi na CDM? mbona mnakiogopa hivyo hicho chama kina nini?

Msichezee akili za wengine nyie, chezeaneni akili zenu wenyewe huko mliko, hizi propaganda zenu za kuingilia faragha za watu ni za kishamba sana, mapenzi ya watu waachiwe wenyewe, najua mtakuja na propaganda nyingine muda sio mrefu, kameanza kale kasichana, umefuata wewe, namsubiri mwingine, washamba kabisa!

Wish ningekuwa na uwezo wa kupiga kura huko CDM niwakomoe mazuzu!
 
Kama wewe siyo mwongo weka jina lako sahihi halafu kama unajua rushwa ya ngono imetumika ulipaswa kutoa taarifa TAKUKURU ili uchaguzi ufanyike kuliko kubwabwaja hapa, pole sana
 
Sasa umeandika nini? Nimesoma toka mwanzo mpaka mwisho sikuona chochote cha kuyathibitisha maneno hayo.

Bila uthibitisho, yote uliyoyaandika yanakuwa crap.

Kwa ujumla ni andiko la kijinga lililoandikwa kuwahadaa wajinga. Mwanzo mpaka mwisho ninujinga na upuuzi mtupu. Sijaona mahali popote ilipoelezwa Heche jinsi alivyohujumiwa.
 
Wacheni kubaka demokrasia
Kuna equal chances za hii makala kua kweli au isiwe kweli!

Yaani 50% yaweza kua kweli au 50% hii kitu ikawa ni pumba plus pumba!

Maneno haya ni common sana kwenye mahali panapokua na power struggle!

Tushayazoea na ni kawaida!
 
Na kwa kuwa hujui nikujuze kidogo tu Mh. HECHE na Mh. MBOWE ni watu wa karibu zaidi kuliko Heche na hao uliowataja!

Kama unaakili na kumbukumbu kumbuka uchaguzi wa Bavicha uliomuweka Heche Kuwa Mwenyekiti wao.
 
Nilitaka sana Mbowe asigombee ili wengine wachukue nafasi yake, ila kwa kuwa kila anayeshindwa katika uchaguzi ndani ya CHADEMA lawama zinaelekezwa kwa MBOWE basi dhahiri kwamba huyu Jamaa si mtu wa kawaida na uwezo wake ni mkubwa sana na hivyo, kuanzia hivi sasa natangaza rasmi kumuunga mkono Mbowe aendeee kuwa Mwenyekiti.
 
Haya nayaona kuwa majungu tu. Labda nikuulize swali hizo njama ama hujuma zinafanywaje? Kura zinaibiwa ama wajumbe wanapewa rushwa? Umepiga bla bla za uchonganishi tu. Na mimi nadhani kama wewe ni mwana CDM basi ulifuata maslahi ambayo umeyakosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…