Tetesi: John Heche kahujumiwa na chama chake CHADEMA

Tetesi: John Heche kahujumiwa na chama chake CHADEMA

Zote mbwembwe, tunataka utuhabarishe yafuatayo:-
Je ni wanachama wangapi walizuiwa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura?
Je kulikuwa na rushwa zilizotembezwa ili kuhakikisha Heche anaangukia Pua, je Heche aliwahi kuwajulisha TAKUKURU ama Police?
Je tangu zoezi la kujinadi, Upigaji kura, Kuhesabu kura na kutangaza matokeo - mazoezi yote haya yalikuwa na figisu ama yalikuwa ya haki? Je Mh. Heche alilalamika popote - chama kina ngazi za rufaa..nk
Je Mh. Henche ndiyo kakutuma kwa niamba yake uje kutuhabarisha? yeye hana uwezo wa kuitisha press?
Kama Salum na Matiko wanatoka wewe inakuhusu nini? au ulitaka Salum atoke na wewe amwache Matiko? yaani mantiki yako ilikuwa nini tufafanulie...wivu ama?

Kama huna majibu ya haya basi ni MAJUNGU tu kama kawaida ya Lumumba - kiwanda cha kutengeneza majungu & fitna.
 
Wewe ccm una maslahi gani na uchaguzi wa Chadema, haya basi mwambieni huyo msajili kibaraka chenu. It's nothing but another rubbish for a trashcan.
Nyie mkawasumbue akina Davutwa tu ndio size yenu.
 
Hivi ni lini ilikua mara ya mwisho kwetu CCM kufanya uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa Chama ngazi taifa?
Kuna mwana CCM anayekumbuka karatasi ya kura ya kumchagua mwenyekiti wa Chama taifa inavyo fanana?
Kwamba unataka kusema mwenyekiti hapigiwi kura?
 
Uwezo wa Mvowe mkubwa wakati CHADEMA Inamfia mkononi mwake
Nilitaka sana Mbowe asigombee ili wengine wachukue nafasi yake, ila kwa kuwa kila anayeshindwa katika uchaguzi ndani ya CHADEMA lawama zinaelekezwa kwa MBOWE basi dhahiri kwamba huyu Jamaa si mtu wa kawaida na uwezo wake ni mkubwa sana na hivyo, kuanzia hivi sasa natangaza rasmi kumuunga mkono Mbowe aendeee kuwa Mwenyekiti.
 
Hizo ni siasa tu asikudanganye
Hata baada ya uchaguzi huo, Heche wakati wa kutoa shukrani, alisema kuwa, yeye Heche alikuwa mstari wa mbele kumshawishi Mbowe agombee hiyo nafasi ya Uenyekiti.
 
Wenye akili na wajanja tunakubaliana na hili andiko
Kama ushahidi pekee ulionao ndio huu, ni wajinga tu watakaokubaliana nawe.
Eleza kunagaubaga jinsi wajumbe zaidi ya 70 waliopiga kura walivyolazimishwa kumchagua Matiko.

Wakati mwingine, mnapoleta mada za kipumbavu kama hizi hapa ni kudharau uwezo wa wanaosoma maandishi yenu.

Hapa unatudharau sisi watu wa JF kwa kudhani hatuwezi kutumia akili zetu, na hapo hapo unawadharau wajumbe waliopiga kura na kufanya nasi tuwaone kama hawana akili kichwani.
 
Lazima Mbiwe ajadiliwe ni Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.
Upuuzi wote huu unaandikia wageni wa nchi gani?
Sisi tupo tuna macho wewe endelea kutumika hadi hapo utakapo tupwa kama kondom. Ujinga huu kawadanganye hao wageni wako na familia yako kama unayo!

Mbowe amekukaa utafikiri alikuchukulia mke!
Kwa taarifa yako Mbowe ni mkiti wa CDM ajaye, nyie ccm wasio na mkia hangaikeni na yenu
 
Naona hapa ni Ant-Mbowe Syndrome inavyoitesa CCM na Serikali yake.
 
"Mbowe akaamuru
kuwa wajumbe na Msimamizi wa uchaguzi kuwa
wahakikishe Heche aangushwe kwa gharama
yoyote ile."
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
tapatalk_1575284580897.jpeg
 
HUJUMA ALIZOFANYIWA HECHE NI AIBU KWA CHAMA KINACHOJIITA CHA DEMOKRASIA:

Uchaguzi wa Mwenyekiti Kanda ya Serengeti umetamatika huku Heche akifanyiwa hujuma, rafu na figisu za kila namna kuhakikisha kuwa anaangushwa na Esther Matiko.

Ni bahati mbaya sana kuwa chaguzi hizi za Kanda zimetawaliwa na hujuma za kila aina, rushwa za kila aina kuanzia za pesa hadi zile za ngono. Naamini Msajili wa Vyama vya Siasa nchini atashirikisha vyombo husika kuchunguza hujuma hizi.

Watu wananiuliza imekuwaje shujaa Heche aangushwe? Bahati nzuri Mimi niko jikoni na leo nitawaeleza peupe, Heche hajaangushwa kidemokrasia iko hivi:

1. Urafiki wa Heche na wapinzani wa Mbowe:

Kwa wale msiojua ni kwamba Heche ni rafiki mkubwa wa Cecil Mwambe, Joseph Selasini Saed Kubenea na Anthony Komu. Mbowe amekuwa akimuona Heche kama kitisho (threat) katika utawala wake hususani kutokana na misimamo mikali isiyoyumba ya Heche ambapo amekuwa akimkosoa Mbowe kwenye vikao vya chama bila woga. Mbowe akaamuru kuwa wajumbe na Msimamizi wa uchaguzi kuwa wahakikishe Heche aangushwe kwa gharama yoyote ile.

2. Ni Kuhusu uhusiano nyeti sana wa kimapenzi baina ya Matiko na Salum Mwalimu. Hili naliweka kiporo ila figisu zikiendelea nitapasua mbarika. Ila kiufupi tu ni kwamba Mwalimu ana Mtoto na Matiko waliozaa naye. Hivyo licha ya Mwalimu kupewa maagizo mazito na Mbowe ili aende Serengeti kuhakikisha Heche anachinjiwa baharini ni kwamba pia Mwalimu ambaye ni NKM-Zanzibar alitumia mwanya huo kuhakikisha mpenzi wake au ukipenda kimada kinapata ulaji. It was a win win situation kutwkeleza maagizo ya Mbowe ya kumchinjia mbali Heche lakini wakati huo huo akihakikisha anatumia fursa hiyo kuhakikisha anamfurahisha Matiko.

Na tayari Mbowe alishatoa amri kuhakikisha kuwa endapo Heche atajaribu kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa adhibitiwe mapema hata kabla ya Uchaguzi wenyewe.

Hivyo urafiki wa Heche na mahasimu wa Mbowe ndani ya chama ndio uliomponza na kupelekea kuadhibiwa kwa amri ya Mwenyekiti.

Heche ni miongoni mwa Wabunge wanaomuunga mkono Cecil Mwambe kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa na hapo ndipo uhasama zaidi kati yake na Mbowe ulipoongezeka.

Na kwa taarifa tu ni kwamba tayari Mbowe ameshasuka mkakati kuhakikisha kuwa akifanikiwa kufanya uchakachuz na kuwa Mwenyekiti kwa awamu ya tano basi John Heche, Joseph Selasini, Anthony Komu, Cecil Mwambe na Saed Kubenea watakatwa kwenye mchakato wa Kura za maoni.

Hii inasikitisha sana, sijawahi kuona Uchaguzi wa kipumbavu na kijinga kama huu. Yani hata CCM kwa sasa wana ahueni ya kidemokrasia kuliko sisi CHADEMA.

Misingi ya demokrasia haipo tena ndani ya CHADEMA, Mbowe ndiye amri, yeye ndiye Katiba na lolote atakalo anahakikisha linafanyika. Watu waejeruhiwa ndani ya CHADEMA wengine wameamua kunyamaza tu.

Ukiongea vizuri na watu walioamua kuondoka CHADEMA unaweza kuwaomba msamaha kama uliwatukana. Mbowe huyu ambaye baadhi ya vijana wameamua kumuabudu na kumsujudia huku wakilamba viatu vyake ili MATUMBO yao yashibishwe ndiye anaenda kuizika CHADEMA. Amini usiamini 2020 CHADEMA hii chini ya Mbowe itakuwa DHAIFU sana kuliko hata TLP ya Mrema.

Mbowe amegeuza CHADEMA kuwa mali yake. Mali za chama amegeuza ni zake. Anyway nikipata wasaa nitaeleza namna Mbowe anavyokifisadi chama na kujineemesha huku akitutumia vijana kama greda lake la umchimbia barabara ili aendelee kuneemeka.

Kama ulikuwa unajiuliza imekuwaje shujaa Heche aangushwe Serengeti basi UKWELI MCHUNGU ndio huo kuwa nguvu ya ngono na na urafiki wake na kina Selasini, Mwambe, Kubenea na Komu ndivyo vilivyo mgharimu.

Level ya udikteta wa Mbowe aliyofikia ndani ya CHADEMA hana legitimacy ya kumuita mtu yeyote yule kuwa ni Dikteta.

Kwa upuuzi huu tunaoufanya CHADEMA hatuna legitimacy ya aina yoyote ile ya kukashifu hujuma za uchaguzi wa Serikali za mitaa. Hivi kwa upumbavu huu unapata wapi ujasiri wa kumkashifu Waziri Jafo na Mwita katika uchaguzi wa SM?

Dawa chungu ndiyo inayoponesha, UKWELI MCHUNGU unauma lakini UKWELI hauna mbadala.

Baadae nitaanika hujuma alizofanyiwa Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini katika uchaguzi wa Mwenyekiti Kanda ya Kaskazini dhidi ya Godbless Lema.

Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
Ukiwa kwenye heat unachachawa saaaaana.
 
mimi sina hasara, hata akinipiga risasi kama alivyompiga Lissu haina shida kabisa

Dah! Your sensational narrative had some hint of plausibility, but this? Kweli wewe ni mtengeneza propaganda wa kulipwa wa awamu ya 5 (sio CCM). Jitahidi tu upunguze jazba kwenye hoja/maelezo yako. Nilianza kuona kitu (substance) ndani ya bandiko lako, lakini ulichoandika hapa kimefuta kila kitu.
 
Remmy Cameroon!

Kuna mambo huyafahamu Heche Si Team KKs Heche ni team Mbowe,

Mbowe ni miongoni mwa watu walioumia kwa Heche kushindwa Uchaguzi,

Kwa Haya machache angalia ulipokwama
 
Back
Top Bottom