Pre GE2025 John Heche kumuunga mkono Lissu asema Lissu ni mkweli, muwazi na muadilifu sana

Pre GE2025 John Heche kumuunga mkono Lissu asema Lissu ni mkweli, muwazi na muadilifu sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hiyo ni too low even for somebody like you.Hoja kama hizo zilitolewa wakati Zitto Kabwe anafukuzwa.Vijana wengi walitishia nyau kwamba watahama Chadema hakuna cha maana kilichotokea.Huwezi kutoa Ultimatum kwenye uchaguzi kwamba asipopita ninayemtaka nahama Chama ni hoja ya kitoto sana.
Uchaguzi ni mchakato sio udikteta.Usipopata unachotaka ujue demokrasia ndio ilivyo.You win or you lose ndio siasa sio mikwara mbuzi.
Hapana sio kweli, enzi za zitto zaidi ya 70% ya chadema tuliside na Mbowe. Angalia humu hard-core chadema wote tulikua Team Mbowe ila kwa sasa sisi tuliokuwa kiherehere kuisemea chadema tumesema "inatosha".

Nakuhakikishia Mbowe akichaguliwa utakuja kuniambia kama kuna chadema ataenda mkutanoni au kupiga kura. Take it from me
 
==
Mhe John Heche anasema yeye waziwazi anamuunga mkono Mhe Tundu Lissu kwa sababu ni mtu mkweli sana ni muadilifu sana na anachukia rushwa kwa moyo na nguvu zake zote.

Mhe John Heche ilitarajiwa na wengi kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa lakini baada ya Mhe Tundu Lissu kuamua kugombea yeye ameamua kumpisha Tundu Lissu kwani anaamini nafasi hiyo ya Uenyekiti anaiweza zaidi na ndio sababu ya kumuunga mkono.

Mpaka sasa haijafahamika kama John Heche atagombea nafasi yoyote ndani ya chama au atabaki pembeni kumuunga mkono Tundu Lissu,

Tusubiri tuone mpaka hiyo tarehe 05.01.2025 ambae ndio mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu Kwa mujibu wa kalenda ya Uchaguzi ya chama.

View attachment 3189380

==
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (@ChademaTz), @HecheJohn, ameonesha dhamira yake ya kuendelea kupigania mustakabali wa chama hicho na Taifa kwa ujumla.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) leo Jumanne Desemba 31, 2024,
Heche ameandika ujumbe mzito akisisitiza umuhimu wa CHADEMA kama taasisi muhimu kwa maslahi ya taifa na wananchi wa Tanzania.

"Tuna taasisi ya kuilinda, tuna nchi ya kutetea, tuna Watanzania wa kupigania. CHADEMA ikifa madhara yake ni makubwa mno kwa nchi yetu," aliandika Heche.

Katika ujumbe huo, Heche amemuelezea mwanasiasa mashuhuri na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara @TunduALissu, kama kiongozi mwadilifu, mkweli, na mwenye uwazi wa hali ya juu.

"Lissu sio muongo ni mkweli, muadilifu na muwazi," aliandika, akionesha imani yake kubwa kwa Lissu.

Lissu, ambaye kwa sasa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, ameendelea kuungwa mkono na viongozi na wafuasi wa chama hicho.

Uchaguzi wa nafasi hiyo unatarajiwa kufanyika tarehe 21.02.2025.
Safi sana
 
Tarime tamka kama anavyotamka wakurya! 🤣
 
Back
Top Bottom