John Heche moments special thread

John Heche moments special thread

Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mh. John Heche, leo Oktoba 15, 2026, ametembelea Kata ya Kirua, Jimbo la Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo amezindua rasmi jiwe la msingi la Kijiji cha Lawate, ikiwa ni sehemu ya shughuli zake za ziara katika Kanda ya Kaskazini.
1792065427971.jpg
1792065421328.jpg
1792065417366.jpg
 
Mapenzi ya Mungu hayasemi watu wauwawe
Watu watekwe
Watu wasingiziwe

Inahitaji kutii kile Mungu anasema kwa mawazo

Kutoa mapenzi ya Mungu na kukubali kupambana na wanaokataa inahitaji kujikana nafsi
.tunapoweka kando matamanio yetu NI kwa sababu yenu
Tunapoona shida inayokuja tunajikana nafsi na kuamka upya
.
Kubalini katika nyakati hizi ngumu tujitoe sote kwa pamoja msituachie kazi hii wachache

Kama huna nguvu ya kusafiri changia mageuzi iepushe CHADEMA kuwa chama cha mfukoni ishikilie wewe kwa namna unavyoweza kama tunavyounga neno la Bwana mkono liende mbele kutuokoa nafsi zetu basi tupunguze sehemu nyingine sasa tuweke kwenye upiganiaji Haki NI wakati mgumu ...tujitoe sote twende sambamba ...mtu mmoja aseme sambamba na HAKI sambamba na HAKI ...

Na John Heche
1792431756724.jpg
1792431759824.jpg
1792431765071.jpg
 
Leo Oktoba 20, 2026 katika mwendelezo wa ziara ya Mhe. John Heche Kanda ya Kaskazini, Jimbo la Karatu, yamefanyika maombi ya kimila katika jamii ya Wairaqw yanayojulikana kama Firor’iraqw au Slufay, kwa ajili ya kuiombea Chadema na viongozi wake, hususan Mh. Tundu Lissu.
1792551371989.jpg
1792551367037.jpg
1792551362366.jpg
1792551357804.jpg
1792551352672.jpg
1792551347947.jpg
1792551343352.jpg
 
ANAANDIKA JOHN HECHE

Huyu mtoto anaitwa Sasha. Wakati nimetoka mahabusu mwaka jana, aliniomba simu kwa wawazi wake ili azungumze na mimi, kisha akanitumia zawadi.

Jana nimeonana naye kwa mara ya kwanza na akaniletea zawadi ya Biblia. Ameniambia furaha yake ilikuwa kubwa sana kuniona ana kwa ana, na mimi nilifurahi sana kukuona, Sasha.

Asante sana, Sasha. Mungu wetu aendelee kukutunza. Ninakutakia mema katika maisha yako. ❤️
1792691734234.jpg
1792691730330.jpg
1792691726793.jpg
 
Done @m
John Wegesa Heche ni mwanasiasa mashuhuri nchini Tanzania na sasa anahudumu kama Makamu Mwenyekiti (Bara) wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA.

Anajulikana sana kwa hotuba zake zenye ushawishi mkubwa, uwezo wa kuhamasisha wananchi kuanzia ngazi ya chini, na harakati zake za dhati za kupinga ukandamizaji wa serikali.

Katika safari yake ya kisiasa, amejenga matukio mengi ya kihistoria yaliyovuta hisia za wengi nchini na nje ya nchi.
Miongoni mwa matukio hayo ni hotuba yake kali aliyotoa hivi karibuni mwezi Agosti 2026 katika mkutano mkuu wa CHADEMA wilayani Temeke, Dar es Salaam. Katika mkutano huo, Heche aligonga vichwa vya habari baada ya kutangaza kuwa yeye na chama chake wanandamwa sana kwa sababu wanakataa kushiriki katika "siasa za udalali".

Alihamasisha umati wa watu kwa ujasiri mkubwa, akisisitiza kuwa serikali iliyopo madarakani haistahili kuendelea kuongoza. Aidha, mnamo Julai 2026, alijibu kampeni za kumchafulia jina zilizoratibiwa na wapinzani wake wa kisiasa huko Tarime Vijijini kwa msemo maarufu uliosambaa sana mtandaoni akisema, "Dhahabu haipotezi thamani kwa kupakwa matope", akiahidi kutorudi nyuma kisa vitisho.

Matukio ya Heche yanajumuisha pia misukosuko mikubwa ya kiusalama na kisheria. Mnamo Oktoba 2025, alikumbana na vurugu kubwa katika mpaka wa Sirari na Isibania alipozuiwa na maafisa wa uhamiaji kuvuka kwenda Kenya kumwakilisha Mwenyekiti wa CHADEMA kwenye msiba wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga.

Katika mzozo huo, gari lake lilipigwa risasi, pasipoti yake ikazuiliwa, na dereva wake alikamatwa. Baadaye mnamo Novemba 2025, kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliogubikwa na utata, Heche alikamatwa na kufunguliwa mashtaka mazito ya ugaidi, hatua iliyosababisha maandamano makubwa ya ndani na kulaaniwa vikali na mashirika ya kimataifa kama Amnesty International.
Nje ya harakati za kisheria, Heche amekuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa wa kihisia na kijamii.

Wakati wa kampeni zake huko Kahama mnamo Mei 2026, alitoa hotuba ya hisia kali kuhusu watu wanaopotea katika mazingira tatanishi na ukandamizaji wa wapinzani, hali iliyowafanya baadhi ya wananchi kwenye mkutano huo kububujikwa na machozi. Kijamii, Heche amekuwa akijihusisha na mijadala ya kitamaduni; mwezi Agosti 2026, alizua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii ya Afrika Mashariki baada ya kumshambulia hadharani msemaji maarufu Haji Manara, akimtaja kama "chawa" wa mfumo ambaye kiwango chake kiko chini sana kulinganishwa na siasa za Heche.


Done Mshana Jr hujaa cha hata punjeee ,kwa sasa Mwanasiasa Maarufu baada ya Mhe Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha siasa CDM Mh sana Mtukufu Tundu Antipasa Lissu ni Mhe sana john WEGESA HECHE MTOTO WA TARIME

Mwisho Yale mahojino alaiyofanyiwa na ITV alimaliza kila kituuuu Mshana Jr tuwasubiri Vikupe vije hapaa

uzi huu umekuja wakati muafakaa
 
Heche ni kiongozi mbinafsi na mlafi aliyekula hela za tone tone na kugoma kujiuzulu, aige mfano wa Nchimbi baada ya tuhuma kaamua kujiuzulu kupisha uchunguzi!!
Hili bomu lilotengenezwa na mfumo lilishindwa hata kfika hata nusu ya uwanjaaa ,na mshindwe mna roho mbaya sanaa ,hata hivyo akila kwani umechangiaa anakuuma nini
 
Back
Top Bottom