John Heche moments special thread

Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mh. John Heche, leo Oktoba 15, 2026, ametembelea Kata ya Kirua, Jimbo la Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo amezindua rasmi jiwe la msingi la Kijiji cha Lawate, ikiwa ni sehemu ya shughuli zake za ziara katika Kanda ya Kaskazini.
 
Mapenzi ya Mungu hayasemi watu wauwawe
Watu watekwe
Watu wasingiziwe

Inahitaji kutii kile Mungu anasema kwa mawazo

Kutoa mapenzi ya Mungu na kukubali kupambana na wanaokataa inahitaji kujikana nafsi
.tunapoweka kando matamanio yetu NI kwa sababu yenu
Tunapoona shida inayokuja tunajikana nafsi na kuamka upya
.
Kubalini katika nyakati hizi ngumu tujitoe sote kwa pamoja msituachie kazi hii wachache

Kama huna nguvu ya kusafiri changia mageuzi iepushe CHADEMA kuwa chama cha mfukoni ishikilie wewe kwa namna unavyoweza kama tunavyounga neno la Bwana mkono liende mbele kutuokoa nafsi zetu basi tupunguze sehemu nyingine sasa tuweke kwenye upiganiaji Haki NI wakati mgumu ...tujitoe sote twende sambamba ...mtu mmoja aseme sambamba na HAKI sambamba na HAKI ...

Na John Heche
 
Leo Oktoba 20, 2026 katika mwendelezo wa ziara ya Mhe. John Heche Kanda ya Kaskazini, Jimbo la Karatu, yamefanyika maombi ya kimila katika jamii ya Wairaqw yanayojulikana kama Firor’iraqw au Slufay, kwa ajili ya kuiombea Chadema na viongozi wake, hususan Mh. Tundu Lissu.
 
ANAANDIKA JOHN HECHE

Huyu mtoto anaitwa Sasha. Wakati nimetoka mahabusu mwaka jana, aliniomba simu kwa wawazi wake ili azungumze na mimi, kisha akanitumia zawadi.

Jana nimeonana naye kwa mara ya kwanza na akaniletea zawadi ya Biblia. Ameniambia furaha yake ilikuwa kubwa sana kuniona ana kwa ana, na mimi nilifurahi sana kukuona, Sasha.

Asante sana, Sasha. Mungu wetu aendelee kukutunza. Ninakutakia mema katika maisha yako. ❤️
 
Done @m
Done Mshana Jr hujaa cha hata punjeee ,kwa sasa Mwanasiasa Maarufu baada ya Mhe Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha siasa CDM Mh sana Mtukufu Tundu Antipasa Lissu ni Mhe sana john WEGESA HECHE MTOTO WA TARIME

Mwisho Yale mahojino alaiyofanyiwa na ITV alimaliza kila kituuuu Mshana Jr tuwasubiri Vikupe vije hapaa

uzi huu umekuja wakati muafakaa
 
Heche ni kiongozi mbinafsi na mlafi aliyekula hela za tone tone na kugoma kujiuzulu, aige mfano wa Nchimbi baada ya tuhuma kaamua kujiuzulu kupisha uchunguzi!!
Hili bomu lilotengenezwa na mfumo lilishindwa hata kfika hata nusu ya uwanjaaa ,na mshindwe mna roho mbaya sanaa ,hata hivyo akila kwani umechangiaa anakuuma nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…