John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

Nimefurahishwa na uchaguzi wa BAVICHA uliomalizika jana.Ulikuwa uchaguzi mgumu sana kulingana na wagombea wote waliokuwa wanagombea.hakika mshindi aliyepatikana atajua alipambana kiume.John Heche ni mwanaharakati na mpiganaji asiyeyumba,hongera kwa ushindi.
Pamoja na ushindi wako unatakiwa ufanye kitu kimoja,ita wapinzani wako wote mkae pamoja mjenge BAVICHA mpya.Usithubutu kudhani kwamba wewe ni bora kuloko wengine wote la hasha! Ila fahamu katika ushindani ni lazima mmoja apatikane.Na bahati umepatikana wewe.Chukua fursa hii adimu kuwaomba wenzako wote wavunje makundi.Washirikishe kwenye fursa na kamati mbalimbali ndani ya BAVICHA.Ambatana nao kwenye ziara mbalimbali za BAVICHA.Ukifanikisha hilo utakuwa umeimarisha ngome ya Chadema.Utakuwa umejifanyia historia ya kutukuka ndani ya Chadema.Utakuwa kiongozi wa kutiliwa mfano.Utakuwa unaandaliwa kuja kurithi mikoba ya kina Dr Slaa miaka ijayo.HONGERA SANA.....
 
mh Geza ulole hii lugha imekuja kwa ndege!ondoa boriti yako kisha onesha hicho kibanzi kwenye jicho la mwenzio,neno sahihi ni APARTHEID na siyo apertheid.
 
Nimefurahishwa na uchaguzi wa BAVICHA uliomalizika jana.Ulikuwa uchaguzi mgumu sana kulingana na wagombea wote waliokuwa wanagombea.hakika mshindi aliyepatikana atajua alipambana kiume.John Heche ni mwanaharakati na mpiganaji asiyeyumba,hongera kwa ushindi.
Pamoja na ushindi wako unatakiwa ufanye kitu kimoja,ita wapinzani wako wote mkae pamoja mjenge BAVICHA mpya.Usithubutu kudhani kwamba wewe ni bora kuloko wengine wote la hasha! Ila fahamu katika ushindani ni lazima mmoja apatikane.Na bahati umepatikana wewe.Chukua fursa hii adimu kuwaomba wenzako wote wavunje makundi.Washirikishe kwenye fursa na kamati mbalimbali ndani ya BAVICHA.Ambatana nao kwenye ziara mbalimbali za BAVICHA.Ukifanikisha hilo utakuwa umeimarisha ngome ya Chadema.Utakuwa umejifanyia historia ya kutukuka ndani ya Chadema.Utakuwa kiongozi wa kutiliwa mfano.Utakuwa unaandaliwa kuja kurithi mikoba ya kina Dr Slaa miaka ijayo.HONGERA SANA.....

Hacha utoto makundi umeyaona wapi?
 
Hongera sana,
Natuko pamoja.Kumbuka mafisadi wapo kila kona uwe imara na umuombe mungu akupe hekima kama za suleimani

Umenichesha kama Sulemani! sure ila hisije ikawa ile hekima aliyokuwa nayo akiona watu kama avatar yako!!

Nina wasiwasi kidogo kuhusu CV na jinsi watu wanavyoisifia! au watu wanamuongelea Heche lakini siyo CV iliyotolewa hapo?

Mimi kulingana na hiyo CV naona Bwana Heche bado ni Mchanga sana katika Siasa za Tanzania na Dunia kwa ujumla hivyo chama bado kinahitaji kumjenga na kumuhimarisha zaidi. Yeye kama yeye bado sana.

Kama nilivyosema jana wakati nampongeza kuwa uongozi ni kutumikia watu amepata nafasi sasa aonyeshe utumishi wake bila woga naomba niongee kuwa hasisite kuchota hekima na mawazo ya busara kutoka kwenye kisima cha wazee wa Chadema na hasiwe kiongozi wa kuamini kuwa mawazo yake ndio sahihi kuliko mawazo ya mtu yeyote, na awe mwepesi kujifunza kutokana na makosa na kutokana na waliomtangulia.
 
Bavicha ndio imefanya uchaguzi makundi yako wapi jamani munaomba Bavicha iwe kama UVCCM duuh
 
Kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza mtoa mada kwa kutupa japo kwa ufupi wasifu wa Kijana wetu Heche, mimi kama mtu mzima kidogo, nina imani kubwa sana na huyu kijana, kiumri namzidi kwa miaka kama minne hivi ila, kiupeo anaweza akawa amenizidi saaana!! Lakini kingine cha dhamani sana alichonacho Heche ni ule moyo wa kuwa tayari kupambani kwa ajili ya watanzania kwa gharama yoyote!! Hii ni lulu ambayo watanzania wengi hasa vijana hawana, nina imani kuwa kwa kipindi chote cha harakati zake za kisiasa lazima aliwahi kuendewa na hawa wavua magamba na kumtaka ama apunguze speed yake katika kutetea wananch,i au ahamie kwao ili aimbe wimbo uleule wa "oh! amani yetu inadhamani tusiivuruge, mara oh! bora kuwa masikini kuliko kukosa amani" lakini naamini kutokana na moyo na wito alionao hakukubali kuuza utume wake kwa chakula cha kidhalimu.

Sasa rai yangu kwake; nataka au naomba ajue kuwa amechaguliwa katika kipindi ambacho taifa lina uhitaji wa hali ya juu wa haki za wananchi kutumia rasilimali zao kwa manufaa yao!! Kwa nini nasema hiyvo , sio kwamba kuna wakati ambao watu hawakuwa na uhitaji huo ila uelewa wa wananchi ulikuwa mdogo sana kutambua kuwa mazingira yao yangeweza kuprovide mahitaji yao ya kila siku! ingawa wapo waliojua hilo walikubali wawe wasaliti kwa taifa lao na watu wao kwa kutotaka kuwajuza walio wengi juu ya neema iliyopo kwenye mazingira yao. Kinyume chake waliendeleza uhaini huo kwa kuwafifisha macho hata walioanza kufunguka macho kidogo na kuanza kuona ili wasithubutu kuuelimisha umma juu ya yaliyopo yenye neema kwao! ila Mungu si Athumani kwa kupitia njia mbalimbali sasa mtanzania wa leo anaelewa haki zake!

Shida iliyopo sasa ambayo Heche unapaswa kuifahamu au tayari umeshaifahamu ni kuwa baada ya umma wa watanzania kuelewa fika juu ya haki zao na utajiri wao jinsi ambovyo kama ungetumika vizuri ungewafaidisha wanalazimishwa, tena kulazimisha sana hata kwa mtutu wa bunduki kuamini kuwa wao ni masikini! na hawapaswi kufikiria zaidi ya hapo wala luhoji kwa nini ni masikini. Huo umma ukisema sawa nyinyi mnafikiri sisi ni masikini na hakuna cha zaidi ya hapo mbona sisi tunaona zaidi ya hapo? Basi tupisheni tuwaonyeshe kwa nini tunasema sisi si masikini!! Umma huo utaambiwa mnataka kuvuruga amani? mnataka kuleta vita? Basi litakalo tokea ni baadhi ya watu katika umma ule kuishia kupoteza viungo vyao kama sio uhai wao kabisa!

Watu wametulizwa si kwa sababu wamechoka sana na kazi za kila siku bali wanasikilizia leo nani atakufa au nani atakuwa kilema kwa sababu tu ya kusema ile ardhi tungeitumia hivyi ingetusaidia.
Kwa hiyo Heche tunakutaka utuongoze katika harakati za kuleta amani ya kweli sio utulivu utokanao na kalipio la dola! yaani tufikie uhuru wa kweli. Nina imani kubwa tena kubwa na wewe hasa nikizingatia kuwa eneo utokalo ni wahanga wa hivi karibuni wa vitendo vya uonevyu dhidi ya wananchi vifanywavyo na Serikali kwa kisingizioa cha kulinda amani.

Mimi kwa upande wangu kama mtu niliyekuzidi umri yaani kwa maana nyingine kama kaka yako nakupa baraka zote na Mungu akusaidie katika kutekeleza majukumu haya mazito yaliyokuja wakati mgumu wa majonzi ya watanzania kwa kupoteza ndugu kila siku. Utuongoze kuandamana mpaka haki yetu ipatikane hatujali ni wangapi watapoteza maisha lakini hatimaye tutaufikia uhuru wa kwelie na kuheshimiana baina ya mtu na kiongozi mtu na mtu mwingine nk.

Mungu mbariki Henche, Mungu ibariki Chadema, Mungu ibariki Tanzania:
Amen
 
huyu atakuwa na vielement vya magamba, hakuna swala la makundi katika chama kinachotaka kukombowa nchi, makundi yapo kule kwa wale uvccm wanaosema sasani ni zamu yao kula.
 
Umenichesha kama Sulemani! sure ila hisije ikawa ile hekima aliyokuwa nayo akiona watu kama avatar yako!!

Nina wasiwasi kidogo kuhusu CV na jinsi watu wanavyoisifia! au watu wanamuongelea Heche lakini siyo CV iliyotolewa hapo?

Mimi kulingana na hiyo CV naona Bwana Heche bado ni Mchanga sana katika Siasa za Tanzania na Dunia kwa ujumla hivyo chama bado kinahitaji kumjenga na kumuhimarisha zaidi. Yeye kama yeye bado sana.

Kama nilivyosema jana wakati nampongeza kuwa uongozi ni kutumikia watu amepata nafasi sasa aonyeshe utumishi wake bila woga naomba niongee kuwa hasisite kuchota hekima na mawazo ya busara kutoka kwenye kisima cha wazee wa Chadema na hasiwe kiongozi wa kuamini kuwa mawazo yake ndio sahihi kuliko mawazo ya mtu yeyote, na awe mwepesi kujifunza kutokana na makosa na kutokana na waliomtangulia.
Pilau la bure bado halijakuwa tayali kuive? je hata kahawa? ebu uliza jikoni naona njaa inakutafuna sana! hukubakiza hata kiporo? inaonyesha umeongeza bidii sana kufuatilia mambo yasiyokuhusu, au umepandishwa cheo nini? badala ya kulia pilau nje naona sasa unatengewa ndani ya nyumba ya fisadi kabisa! Naona umekazana kweli kutetea ufisadi, endelea hivyohivyo huenda ukakaribisha chumbani kwa fisadi kabisha! si utakuwa umeridhika? kwani wewe una kingine unachokitafuta zaidi ya Pilau na gahawa?
Kwa heri
 
Ninge kujibu ila kwasababu umesema umezaliwa yapata mwaka 1977, basi nakusamehe naamini ni utoto na akili ya makamasi inakusumbua sana au kwa vile ulizaliwa wakati CCM inazaliwa basi ulizaliwa na akili hasi au mtindio wa Ubongo!

Ushahidi kuwa unamtindio wa ubongo ni hayo maneno yako nadhani ubongo wako unafanya kazi kama trigger ya AK47 ni kusukumwa hamna kufikiri.
 
Bila shaka CV inaleta hamasa na matumaini kwa chama na watz kuwa amepatikana kamanda mwingine ambaye tukimpa ushirikiano wa kutosha basi tutazidi kupiga hatua katika kung'oa magamba na kuyazika
 
Umenichesha kama Sulemani! sure ila hisije ikawa ile hekima aliyokuwa nayo akiona watu kama avatar yako!!

Nina wasiwasi kidogo kuhusu CV na jinsi watu wanavyoisifia! au watu wanamuongelea Heche lakini siyo CV iliyotolewa hapo?

Mimi kulingana na hiyo CV naona Bwana Heche bado ni Mchanga sana katika Siasa za Tanzania na Dunia kwa ujumla hivyo chama bado kinahitaji kumjenga na kumuhimarisha zaidi. Yeye kama yeye bado sana.

Kama nilivyosema jana wakati nampongeza kuwa uongozi ni kutumikia watu amepata nafasi sasa aonyeshe utumishi wake bila woga naomba niongee kuwa hasisite kuchota hekima na mawazo ya busara kutoka kwenye kisima cha wazee wa Chadema na hasiwe kiongozi wa kuamini kuwa mawazo yake ndio sahihi kuliko mawazo ya mtu yeyote, na awe mwepesi kujifunza kutokana na makosa na kutokana na waliomtangulia.

Sasa mbona wewe pia hujaonesha tofauti ya aina yoyote! Mahali gani ambapo umeongelea CV (umemchambua Heche kwa kuangalia CV yake) tunafanya hivi kwa maslahi ya wananchi, maana kiongozi wa BAVICHA si kitu kidogo kwa namna siasa zetu sasa zinavyochukua mkondo wa kuelekea mapambano ya awamu ya pili kupigania rasilimali za nchi kumuinua kiuchumi Mtanzania (kama alivyotabiri Lumumba).

Hujaonesha uchanga wa Heche, otherwise ndiyo maana ni kiongozi wa vijana
 
Kuchaguliwa kwa John Heche ni pigo kwa Nauye mwenye kueneza siasa za ukabila na udini... nawashukuru sana Vijana Chadema... laiki angalitoka uchagani mngesikia vuvuzela za uchochezi kuwa cdm ni chama cha Wachaga.... leo watasema nini?
Asante mpiganaji Heche... twende mbele, tuikomboe nchi zidi ya mafisadi.
 
watu wengi sasa wameanza kuulizia wakihitaji kumjua kamanda heche. Haya ni maelezo yaliyopatikana siku za nyuma kidogo katika mazungumzo naye. Wakuu mpiganaji huyu anastahili kupewa ushirikiano ili aiongoze bavicha kwa maslahi ya nchi na chama chake pia. Mpaka sasa record ya heche katika uaminifu wake kwa maslahi ya watanzania wanyonge, ambao chama chake kimejipambanua kuwasemea na kuwapigania, si ya kutiliwa wasiwasi. Kwa maneno na vitendo. Mwingine anaweza kuongeza. Nawasilisha wakuu.

Watu wengi wameanza kuuliza heche ni mtu gani. Walau haya yamepatikana kutokana na mazungumzo naye siku za nyuma kidogo. Lakini upambanaji wa heche na uwezo wake katika kusukuma hoja za wananchi (watanzania) wanyonge, hoja za chama chake na maslahi ya nchi kwa ujumla, mpaka sasa si wa kutiliwa shaka wakuu. Apewe ushirikiano katika kushirikiana na viongozi wenzake cdm, kwa maendeleo ya nchi yetu. Kazi si kuchaguliwa, kazi ni kuwajibika kutimiza matarajio ya watu kwa wakati huo.

john heche suguta

- kuzaliwa – 1981 – katika kijiji cha sirari, tarime
- shule 1989 – nyamaharaga primary
- sekondari – 1997- bulima secondary
- musoma allience high school- 2001
- stashahada ya ualimu - 2004- 2006 chuo cha ualimu bunda
- shahada ya sanaa na elimu – 2006-2009 chuo kikuu cha mt. Augustino nyegezi
mwanza.

harakati za kisiasa:
- kujiunga na chadema mwaka 2000
- mmoja wa waasisi na waanzilishi wa tawi la chadema chuo kikuu cha mt. Augustino nyegezi mwanza.
- katibu wa tawi la chadema saut 2008

- mgombea udiwani katika kata ya tarime mjini chadema uchaguzi mdogo 2008 kuziba nafasi ya marehemu mh. Chacha zakayo wangwe na kushinda kiti hicho baada ya kumshinda mfanyabiashara tajiri kanda ya ziwa mwenye kumiliki mabasi na visima vya mafuta.

- mgombea ubunge kura za m aoni ndani ya chadema uchaguzi mkuu wa 2010 lakini kura hazikutosha ndani ya chadema
- mgombea uenyekiti wa vijana wa chadema taifa 2009, uchaguzi ulioharibika
- kushiriki katika operesheni mbalimbali za chama, oparesheni sangara 2008-2010,
- mratibu msaidizi wa kampeni za mgombea urais chadema nchi nzima.
- kuzunguka nchi nzima kwenye kampeni za mgombea urais chadema
- kushiriki maandamano ya arusha kupinga uchaguzi wa umeya
- kushiriki oparesheni ya kanda ya ziwa kupinga dowans na kupanda kwa gharama za maisha.

kazi alizofanya katika kipindi chake cha udiwani

kujenga shule ya sekondari kata ya tarime mjini(nyamisangura sekondari)
- kusimamia ujenzi wa barabara za tarime mjini
- kusimamia upatikanaji wa maji safi katika kata ya tarime mjini.
- kusimamia na kutetea haki za wanyonge
- kufanya mikutano ya kujenga chama mikoa ya mara(musoma mjini,mugumutarime), mwanza (nyamagana na ilemela,magu), shinyanga (bukombe) na dar es salaam.

malengo yake ya sasa:
kwani nini aligombea uenyekiti
- kuifanya bavicha kuwa taasisi imara itakayo toa viongozi makini wa chama na taifa kwa ujumla.
- kuunganisha nguvu za vijana wa taifa hili katika kudai uhuru katika mapambano haya ya awamu ya pili, yanayolenga kusimamia rasilimali za nchi kutumika kwa maslahi ya watanzania, kwa ajili ya kuwainua kiuchumi na kupunguza umaskini wao. Pia haki na usawa kwa watanzania wote ili kujenga amani na utulivu wa kweli ulio imara.
- kupigania ushiriki wa vijana katika siasa za tanzania na nafasi za uongozi katika taifa
- kuongoza bavicha kuisimamia serekali kuiwajibisha na kuihoji kuhusu maisha (ustawi) ya watanzania na nchi kwa ujumla.
- kuandaa tasisi itakayo tetea na kulinda chama na mali zake
- kuunda taasisi itakayo waandaa vijana kuwa na uzalendo wa kitaifa uliopotea na kupigania maadili
- kuunda baraza litakalo piga vita ufisadi, wizi na upendeleo kwa nguvu zote
- kupigania kuunda baraza la vijana la taifa

viongozi wanaomvutia kisiasa
- mwl nyerere, dr slaa, mbowe, zitto
- nelson mandela na franklin roosevelt
kinachomchukiza
- ufisadi na siasa za udini.
- kuhusu ufisadi, yeye hupenda kusema "waafrika kusini wakati wa ubaguzi wa rangi walikuwa na msemo unaosema "we want aperthaid removed not aperthaid reformed" wakiwa na maana wanataka kuondoa ubaguzi wa rangi sio kuurekebisha ubaguzi wa rangi na sisi vijana wa chadema tunalengo la kuuondoa ufisadi na sio kuurekebisha ufisadi."

- tanzania hakuna udini, kuna viongozi wachache wanaoficha udhaifu wao wa kiuongozi kwenye kapeti la udini, watanzania ni wamoja wanashirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii, kisiasa na kimaendeleo kwa pamoja.

wito
- vijana wajiunge na chadema kwa wingi kwa sababu chadema ni chama pekee kinachopigania haki za wanyonge, kutetea rasimali za nchi na ndiyo tumaini jipya kwa watanzania

- anawaomba vijana wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chadema katika chaguzi mbalimbali kuanzia ndani ya chama na za kiserekali vijijini,vitongoji na uchaguzi mkuu ujao

- anawaomba watanzania wote kuiunga chadema mkono na kuikataa ccm kwa kuwasababishia watanzania umasikini mkubwa kwa zaidi ya miaka 50.

kumbuka wewe heche ni target ya mafisi wa ahadi wa chama cha magamba. Waliingilia uchaguzi wameshindwa sasa watakufuata wewe na pesa hizo hizo wanazotuibia. Ni mashetani.
Pambana dogo you have the full support of strong soldiers of cdm.
 
Hongera Dogo Heche
Sasa umepewa jukwaa la kuleta maendeleo ya watanzania wote na sio
jukwaa la kuleta ubazazi na ubinafsi na kutenganisha watu kwa ubaguzi.
Sote tunakuamini chaPA kazi mwanangu
Tuko PAMOJA.

Nimekuwa nikifuatilia sana kwa karibu wagombea wote wa BAVICHA ukweli usiofichika na ukiondoa mapenzi hakuna mgombea hata mmoja mwenye sifa ya Bwana HECHE tumemsikia asikisema kwa dhamira ya moyo wake aliyoyaamini, tumemuona akitenda kwa uzalendo na mapenzi ya chama yake tumemuona kwenye majukwaa akifanya kwa ajili ya chama chake tumeona yu tayari mda wowote kupigania na kujitplea kwa ajili ya chama bila kucjhoka na hakuchoka kukitetea chama hata kilipotuhumiwa hakika anafaa kuongoza BAVICHA narudia tena hatuhitaji kutafuna maneno ni mkomavu kuliko wote aliokuwa anapambana nao kwa hiyo tuache porojo za kama nimeenguliwa mapema nk la hasha hizo ni porojo nina uhakika mtu anapoenguliwa kula zake upelekwa upande mwingine kwa hiyo hata kama kuna ambao hawakuenguliwa wangegawana kura hizohizo za HECHE zingebaki palepale ni nani asiyejua kazi ya Heche miongoni mwa wajumbe hao waliopiga kura?

Sina kumbukumbu ya miongoni mwa wagombea wote wameisha simama majukwaani mara nyingi kuipigania chadema kuliko Heche au kwenye vyombo vya Habari wakiipigania CDM kama heche tuache porojo mnyonge mnyongeni haki yake mpeni Bwana Heche anasifa kwa asilimia hizihizo alizopata kuliko wagombea wenzake wote.Hiyo sio nafasi ya ubishoo au ujiko ni ya kuchapa kazi na kazi ya Bwana Heche tumeiona Hakika Heche ni Jembe.
 
Hongereni nyooote mlioshiriki uchaguzi BVICHA.

Mungu awaongoze katika kazi yake ya kusimami haki kwa Watanzania wote. Makundi yooote yavunjwe leo na wala tusingoje kesho katika hili. Nyote washindi kwa washindwa ni wetu; tunawapenda sana na kuwashimu saaana pia.

BAVICHA timu, kazi ianze mara moja. Tuhakikishe ya kwamba ndani ya huo mwezi Juni kunapatikana MWELEKEO WA KISHERIA NDANI YA BUNGE KUHUSU KUPATIKANA KWA KATIBA MPYA YA WANANCHI kabla ya 2015. Ruksa kufanya kila linalowezekaka ili lengo hili litimie haraka nchini

Ndio, tuzunguke nchi nzima vijana kuhamashishana juu y swala hili zito na nyrti la kuandikwa upya kwa ramani na dira ya uongozi nchini.

Nimefurahishwa na uchaguzi wa BAVICHA uliomalizika jana.Ulikuwa uchaguzi mgumu sana kulingana na wagombea wote waliokuwa wanagombea.hakika mshindi aliyepatikana atajua alipambana kiume.John Heche ni mwanaharakati na mpiganaji asiyeyumba,hongera kwa ushindi.
Pamoja na ushindi wako unatakiwa ufanye kitu kimoja,ita wapinzani wako wote mkae pamoja mjenge BAVICHA mpya.Usithubutu kudhani kwamba wewe ni bora kuloko wengine wote la hasha! Ila fahamu katika ushindani ni lazima mmoja apatikane.Na bahati umepatikana wewe.Chukua fursa hii adimu kuwaomba wenzako wote wavunje makundi.Washirikishe kwenye fursa na kamati mbalimbali ndani ya BAVICHA.Ambatana nao kwenye ziara mbalimbali za BAVICHA.Ukifanikisha hilo utakuwa umeimarisha ngome ya Chadema.Utakuwa umejifanyia historia ya kutukuka ndani ya Chadema.Utakuwa kiongozi wa kutiliwa mfano.Utakuwa unaandaliwa kuja kurithi mikoba ya kina Dr Slaa miaka ijayo.HONGERA SANA.....
 
Hongera Heche, unganisha vijana na usijifungie milango kwani vijana watz wa leo wanabalehe wanapozaliwa, huna haja ya kufichaficha masuala ya msingi na nina hakika utatunza heshima yako kama kijana
 
*Aahidi CHADEMA kuchukua dola 2015
*Rushwa, kujuana vyatawala uchaguzi

Na Edmund Mihale

HATIMAYE uchaguzi wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) ulimazika jana kwa kumpata Bw. John Heche kuwa
Mwenyekiti wa umoja huo.

Pamoja na kupatika kwa kiongozi huyo, uchaguzi huo uligubikwa na mizengwe mbalimbali ikiwemo rushwa na mambo ya 'kujuana' yaliyooneshwa wazi na viongozi wa chama hicho.

Kwa mujibu wa uchuguzi uliofanywa na Majira juzi usiku, uchaguzi huo ulifanyika huku kukiwa na makundi matatu, makundi hayo ni yale yanayomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe na lile lisilomuunga mkono mtu yeyote katika chama hicho.

Uchunguzi huo ulibaini kuwa kundi linalomuunga mkono, Bw. Mbowe ndilo lilokuwa na nguvu zaidi na ndilo lilochukua kiti hicho kutokana na mwanzilishi wa chama hicho, Bw. Edwin Mtei kuliunga mkono kwa asilimia mia.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Baraza la Wazee kilidokeza kuwa, maamuzi ya kufanya uchunguzi wa wagombea yalifikiwa baada ya kugopa kivuli cha Bw. Zitto ambaye ameonekana kuungwa mkono na vijana wengi ndani ya chama hicho.

Kilisema kuwa baada ya kubaini uwezekano wa kundi hilo kushinda, baraza la wazee lilikubaliana kutafuta mambo yatakayowamaliza wagombea hao ili wasipitishwe katika kugombea kiti hicho.

"Ndugu yangu napenda kusema kuwa chama hiki sasa kinaenda pabaya walitafuta kila njia ya kuwamaliza vijana na njia waliyoipata ni kuwatutafutia tuhuma zitakazowafanya waondoke katika kuwania nafasi hiyo...lakini tulipigana na ikashindikana," alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

Alieleza kuwa tuhuma hizo ni kundi hilo kutaka kuunganisha nguvu katika uchaguzi huo ili kumpigia kura mtu moja jambo ambalo kamati ya wazee ilipingana na suala hilo ikidai kuwa ni jambo linalowagawa vijana ndani ya chama.

Chanzo hicho kilisema kuwa katika uchaguzi wowote makundi lazima yawepo ndo maana mgombea hawezi kupata kura kwa asilimia mia moja hata akiwa pekee yake.

Alisema tuhuma nyingine zilizofanya kuenguliwa kwa wagombea hao ni kupokea wajumbe kutoka Zanzibar jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote lakini kutokana na mizengwe iliyoandaliwa na kamati hiyo ilibidi watu hao waadhibiwe.

Alisema kuwa tuhuma nyingine ilikuwa ni kupiga kampeni kabla ya muda uliopangwa na tume hiyo hali iliyosababisha kuenguliwa dakika za mwisho katika uchaguzi huo.

"Tuhuma nyingine iliyoelezwa ni wagombea hao kutaka kupindua chama hicho kwa kuhamisha agenda za chama hicho na wengine walihofiwa kuwa ni usalama wa taifa," kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo Mjumbe huyo wa baraza la wazee alisema kwa upande wa Bw. Heche nako kulikuwa na tuhuma za kupokea wajumbe ambao kamati haikutaja kuwa wanatoka katika mkoa upi lakini alijitetea kuwa ni ndugu zake.

"CHADEMA tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anapokosea tunataka awajibishwe, sisi leo mtu anakosea wakati wa mchakato wa uchaguzi lakini tunasema tunafanya uchunguzi je akipata madaraka tunamchukulia hatua gani kwani atakuwa tayari amepata madaraka," kilisema chanzo.

Chanzo hicho kiliendelea kuhoji ni kwa nini mgombea huyo aachwe na kuchukua madaraka huku akiwa na tuhuma hivyo akataka haki itendeke kwa wote.

Naye Tumaini Makene anaripoti kuwa;

Kamati ndogo maalum, kwa ajili ya uchunguzi wa uchaguzi huo iliyoundwa na kamati kuu ya chama hicho ilibaini kuwepo kwa vitendo vichafu ikiwemo baadhi ya wagombea kutaka kuundwa makundi ili kudanganya wapiga kura kwa nia ya kutaka ashinde mtu wanayemtaka kwa hila zao.

Akizungumza na majira jana akiwa katika uchovu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, pamoja na kutotaka kuzungumzia tuhuma hizo za rushwa kwa undani akisema "mengine yanahitaji maamuzi ya juu", alisema kuwa wagombea hao watatu walioenguliwa baada ya kuthibitisha kuwa wamekwenda kinyume na katiba na kanuni za chama, kifungu cha 10, wamekiri pia kuwa wao walijihusisha kutengeneza agenda ya BAVICHA.

"Sasa hilo ni suala kubwa agenda ya BAVICHA ni suala la mkutano na haliwezi kuwa la wao watatu lakini walibainika kujihusisha na kundi la Bw. Habib Machange ambapo ilibidi chama kiingie gharama ikiwemo wajumbe wa kamati hizo kufanya kazi tangu saa saba usiku wa juzi mpaka asubuhi jana na baadhi ya wajumbe walishindwa kurejea kwao," alisema Dkt. Slaa.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Majira ilibainika kuwa mmoja wa wabunge wa chama hicho alijihusisha na kusimamia vikao vya usiku wa manane vilivyokuwa vikitumika kuwalubuni wajumbe kugawa fedha, kuwanunulia pombe usiku wa kuamkia uchaguzi akitaka kuweka mtandao unaodaiwa kuwa na lengo la kusambaratisha chama hicho.

Mbunge huyo machachari kutoka Kanda ya ziwa ametajwa pia kutoa udhamini wa mmoja wa mgombea aliyeenguliwa kwa lengo hilo ambapo imeelezwa kuwa suala lake pamoja na vituko vingine vitafikishwa mbele ya Kamati Kuu kwa maamuzi zaidi.

Alipoulizwa juu ya tuhuma kwa mbunge huyo (jina tunalo), Dkt. Slaa hakuwa tayari kulizungumzia na kusema kuwa liko ngazi ya juu ya kamati kuu.

Wakati hayo yakiendelea Bw. Heche alisema yuko tayari kufanya kazi katika nafasi hiyo akishirikiana na wenzake ili BAVICHA iwe sauti ya kupigania maslahi ya wananchi wanyonge.

Akizungumza na majira jana, Bw. Heche alisema kuwa BAVICHA itasimama kwa maslahi ya nchi na chama hicho kwa jitihada za kuchukua dola kwa ridhaa ya wananchi.

Bw. Heche alipata kura 147 sawa na asimilia 56 ya kura zote zilizopigwa 267 ambapo kura tatu ziliharibika.

Walioenguliwa katika uchaguzi huo ni Greyson Nyakarungu, Mwampamba na Bernard Saanane.
 
Kuchaguliwa kwa John Heche ni pigo kwa Nauye mwenye kueneza siasa za ukabila na udini... nawashukuru sana Vijana Chadema... laiki angalitoka uchagani mngesikia vuvuzela za uchochezi kuwa cdm ni chama cha Wachaga.... leo watasema nini?
Asante mpiganaji Heche... twende mbele, tuikomboe nchi zidi ya mafisadi.

Tatizo la ukabila Chadema ni kubwa sana! Heche ni tone tu la maji kwa bahari!
 
Back
Top Bottom