John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

Tatizo la ukabila Chadema ni kubwa sana! Heche ni tone tu la maji kwa bahari!
Pole maana ukabila mbona umejaa ndani ya CCM? chama kilicho miliki ya viongozi? wakitoka wao wanaingia wana wao. Ni chadema tu ambako uchaguzi unakuwa wazi na si miliki ya viongozi kama chama magamba!
 
CV ya kawaida sana! Hadi maandamano nayo ni wasifu!

Ulitaka iweje? Huu ulikuwa uchaguzi wa Vijana na umri ni kigezo; sasa kwa umri huo ulitaka awe amefanya nini? Awe ameoa wake wanne? HONGERA KAMANDA HECHE.

Nashauri Chama kifanye haraka kumtambulisha nchi nzima hususan kwa vijana; mijini na vijijini; vyuoni na migodini; vijiweni na hata maofisini. Karibu kamanda - unganisha vijana, unganisha watanzania, tusonge mbele.

KWA MBAAALI KAMA NAANZA KUONA MWANGA VILE.
 
tukamatie mafisadi mura, ni fiita moja kuubwa kuliko ya khagera, nakuwuunga mukono mia kwa mia tata, wewe wa nyumbani hiyo gasi ndhongo
 
Nadhani inakubidi kwanza utafute maana au tafsiri ya neno UDINI, ukisha pata rudi tutajadili maanake napoteza muda wa kujadili mengine muhimu...

Sio kwamba utafute wewe, kwani umeshindwa kufafanua hoja zako sasa unataka watu wakusaidie kujua maana ya udini? Eeeeh! Kumbe unaongea bila kujua maana, unapoteza mda wa watu bure tafadhali kapumzike, ndg yangu!!

Nikusaidie kwa kifupi - UDINI:- Ni tendo au mtazamo au hisia au mlengo wa maamuzi anayofanya mtu juu ya jambo fulani kwa misingi ya dini fulani. Inaweza kuwa katika ajira, sherehe, mikutano, uchaguzi, kupandisha vyeo, au kuteua viongozi n.k.

Haya sasa Linganisha hoja zako na wengine halafu uamue mwenyewe kuendelea au la maana umeelewa bila shaka.
 
Watu wengi sasa wameanza kuulizia wakihitaji kumjua Kamanda Heche. Haya ni maelezo yaliyopatikana siku za nyuma kidogo katika mazungumzo naye. Wakuu mpiganaji huyu anastahili kupewa ushirikiano ili aiongoze BAVICHA kwa maslahi ya nchi na chama chake pia. MPAKA SASA record ya Heche katika uaminifu wake kwa maslahi ya Watanzania wanyonge, ambao chama chake kimejipambanua kuwasemea na kuwapigania, si ya kutiliwa wasiwasi. Kwa maneno na vitendo. Mwingine anaweza kuongeza. Nawasilisha wakuu.

Watu wengi wameanza kuuliza Heche ni mtu gani. Walau haya yamepatikana kutokana na mazungumzo naye siku za nyuma kidogo. Lakini upambanaji wa Heche na uwezo wake katika kusukuma hoja za wananchi (Watanzania) wanyonge, hoja za chama chake na maslahi ya nchi kwa ujumla, MPAKA SASA si wa kutiliwa shaka wakuu. Apewe ushirikiano katika kushirikiana na viongozi wenzake CDM, kwa maendeleo ya nchi yetu. KAZI SI KUCHAGULIWA, KAZI NI KUWAJIBIKA KUTIMIZA MATARAJIO YA WATU KWA WAKATI HUO.

JOHN HECHE SUGUTA

- Kuzaliwa – 1981 – katika kijiji cha Sirari, Tarime
- Shule 1989 – Nyamaharaga Primary
- Sekondari – 1997- Bulima Secondary
- Musoma Allience High School- 2001
- Stashahada ya Ualimu - 2004- 2006 Chuo cha Ualimu Bunda
- Shahada ya Sanaa na Elimu – 2006-2009 Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Nyegezi
Mwanza.

HARAKATI ZA KISIASA:
- Kujiunga na CHADEMA mwaka 2000
- Mmoja wa Waasisi na waanzilishi wa Tawi la CHADEMA Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Nyegezi Mwanza.
- Katibu wa Tawi la CHADEMA SAUT 2008

- Mgombea Udiwani katika Kata ya Tarime Mjini CHADEMA Uchaguzi Mdogo 2008 kuziba nafasi ya Marehemu Mh. Chacha Zakayo Wangwe na kushinda kiti hicho baada ya kumshinda Mfanyabiashara Tajiri Kanda ya Ziwa mwenye kumiliki Mabasi na Visima vya Mafuta.

- Mgombea Ubunge Kura za M aoni ndani ya CHADEMA Uchaguzi mkuu wa 2010 lakini kura hazikutosha ndani ya CHADEMA
- Mgombea Uenyekiti wa Vijana wa CHADEMA Taifa 2009, Uchaguzi ulioharibika
- Kushiriki katika operesheni mbalimbali za chama, Oparesheni Sangara 2008-2010,
- Mratibu msaidizi wa kampeni za mgombea urais CHADEMA Nchi nzima.
- Kuzunguka nchi nzima kwenye kampeni za mgombea urais CHADEMA
- Kushiriki maandamano ya Arusha kupinga uchaguzi wa umeya
- Kushiriki oparesheni ya kanda ya ziwa kupinga DOWANS na kupanda kwa gharama za maisha.

Kazi alizofanya katika kipindi chake cha udiwani

Kujenga shule ya sekondari kata ya Tarime mjini(nyamisangura sekondari)
- Kusimamia ujenzi wa barabara za Tarime Mjini
- Kusimamia upatikanaji wa maji safi katika kata ya Tarime mjini.
- Kusimamia na kutetea haki za wanyonge
- Kufanya mikutano ya kujenga chama mikoa ya Mara(Musoma mjini,MugumuTarime), Mwanza (Nyamagana na Ilemela,Magu), Shinyanga (Bukombe) na Dar es Salaam.

MALENGO YAKE YA SASA:
Kwani nini aligombea uenyekiti
- Kuifanya BAVICHA kuwa taasisi imara itakayo toa viongozi makini wa chama na taifa kwa ujumla.
- Kuunganisha nguvu za vijana wa taifa hili katika kudai uhuru katika mapambano haya ya awamu ya pili, yanayolenga kusimamia rasilimali za nchi kutumika kwa maslahi ya Watanzania, kwa ajili ya kuwainua kiuchumi na kupunguza umaskini wao. Pia haki na usawa kwa Watanzania wote ili kujenga amani na utulivu wa kweli ulio imara.
- Kupigania ushiriki wa vijana katika siasa za Tanzania na nafasi za uongozi katika taifa
- Kuongoza BAVICHA kuisimamia serekali kuiwajibisha na kuihoji kuhusu maisha (ustawi) ya Watanzania na nchi kwa ujumla.
- Kuandaa tasisi itakayo tetea na kulinda chama na mali zake
- Kuunda taasisi itakayo waandaa vijana kuwa na uzalendo wa kitaifa uliopotea na kupigania maadili
- Kuunda baraza litakalo piga vita ufisadi, wizi na upendeleo kwa nguvu zote
- Kupigania kuunda baraza la vijana la taifa

VIONGOZI WANAOMVUTIA KISIASA
- Mwl Nyerere, Dr Slaa, Mbowe, Zitto
- Nelson Mandela na Franklin Roosevelt
KINACHOMCHUKIZA
- Ufisadi na siasa za udini.
- Kuhusu ufisadi, yeye hupenda kusema “Waafrika Kusini wakati wa ubaguzi wa rangi walikuwa na msemo unaosema “we want aperthaid removed not aperthaid reformed” wakiwa na maana wanataka kuondoa ubaguzi wa rangi sio kuurekebisha ubaguzi wa rangi na sisi vijana wa CHADEMA tunalengo la kuuondoa ufisadi na sio kuurekebisha ufisadi.”

- Tanzania hakuna udini, kuna viongozi wachache wanaoficha udhaifu wao wa kiuongozi kwenye kapeti la udini, Watanzania ni wamoja wanashirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii, kisiasa na kimaendeleo kwa pamoja.

WITO
- Vijana wajiunge na CHADEMA kwa wingi kwa sababu CHADEMA ni chama pekee kinachopigania haki za wanyonge, kutetea rasimali za nchi na ndiyo tumaini jipya kwa Watanzania

- Anawaomba Vijana wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kupitia CHADEMA katika chaguzi mbalimbali kuanzia ndani ya chama na za kiserekali vijijini,vitongoji na uchaguzi mkuu ujao

- Anawaomba Watanzania wote kuiunga CHADEMA mkono na kuikataa CCM kwa kuwasababishia watanzania umasikini mkubwa kwa zaidi ya miaka 50.
Nimeshiriki nae Musoma High School kufanya Migomo mwaka 2001 iliyoleta mabadiliko ya kiongozi na kiutendaji
 
Mkuu, this is very good!
Hivi kwanini mtu asiseme tu kwamba jamani habari za kazi, au atumie uhamasishaji unaofuatana na mauddhui ya mkutano/kika. Kwa mfano mtu kama yuko kwenye mkutano wa vijana, basi hata aseme : Vijana Juu! na siyo mambo ya Bwana asifiwe au asalaam Aleikum....

Ni kwa sababu unafikiri Mungu amefungiwa misikitini na Makanisani tu, kama hauna unafiki na dhamira yako ni safi mbele za watu na Mungu na malengo yako ni mema utamtanguliza Mungu katika uongozi wako wa kisiasa. Lakini kama ni Gamba, mla rushwa, fisadi, mwongo,n.k. lazima uongope kumtaja Mungu mbele za watu na utashangaa tu kuona wengine wanamtaja, utafikiri wanakosea kumbe masikini unafiki na dhuruma zako ndo zinakutesa tu.
 
Mungu wa chadema ni Yesu, kama huamini hivyo basi ww huja kolifai kuwa chama hichi, na reference yake ni bible pekee, ndio maana Habib alichinjwa kwakuwa mungu wake ni shetani kama alivyotueleza mh. Mbunge

NONSENSE!!! To hell!!
 
nimeipenda......ingetulia zaidi kama ungetumia nafsi ya kwanza..... I,ME,MY,MINE
 
hongera sana kaka heche tunategemea mengi kutoka kwako.
Goodluck on your New job.
 
Pongezi Mwenyekiti na Tunakutakia Uongozi Mwema. Ushahuri nitakupa ni kuwa karibu na viongozi wa Taifa Dr Slaa, Mbowe na wengine ili ujifunze mengi kutoka kwao na pia jenga vision ya vijana Chadema. Jiandae na jenga BAVICHA Tanzania nzima kuanzia vijijini mpaka miji yote mikubwa. Kama unavyoona kazi kubwa imeshafanywa na viongozi wetu wa Taifa na tunategemea utaendeleza malengo na aspirations za Watanzania wote.

"Leadership is directly go with responsibilities and criticisms. Don't Fear the Challenges"
 
Sio kwamba utafute wewe, kwani umeshindwa kufafanua hoja zako sasa unataka watu wakusaidie kujua maana ya udini? Eeeeh! Kumbe unaongea bila kujua maana, unapoteza mda wa watu bure tafadhali kapumzike, ndg yangu!!

Nikusaidie kwa kifupi - UDINI:- Ni tendo au mtazamo au hisia au mlengo wa maamuzi anayofanya mtu juu ya jambo fulani kwa misingi ya dini fulani. Inaweza kuwa katika ajira, sherehe, mikutano, uchaguzi, kupandisha vyeo, au kuteua viongozi n.k.Haya sasa Linganisha hoja zako na wengine halafu uamue mwenyewe kuendelea au la maana umeelewa bila shaka.
Mkuu samahani nilikuwa nimetoka ktk ukumbi huu kwa muda..Sijui kama nimekukwaza. Naam umeisema tafsiri ya Udini vizuri tu kama unavyoelewa wewe ingawa sii sahihi...sasa nikuulize ninapotumia maneno ya kiimani ya dini ktk siasa na hukubaliani nayo Je, huo ni Udini pia?.. nilichosema mimi ni kwamba tusipende sana kutumia imani za dini ktk siasa zinaweza kuharibu mchuzi mzima, kwani alichosema Regia mimi sikubaliani nacho na sidhani kama ni Udini iwe yeye alosema au mimi nisiyekubaliana naye..
Kweli unaweza tumia neno Mungu walati wowote lakini unapompa Mungu mkono juu ya Chama hali mimi sikubaliani na mawazo hayo ni sawa na kutokubaliana kisiasa...
Labda nikujuze kwa kutumia dini zenyewe ingawa haikuwa nia yangu kabisa kwa nini sipendi matumizi ya aya za dini ktk mihadhara ya kisiasa. Kwa mfano Mkristu anapoomba kwa jina la Yesu, hii ni kufuru kwa Waislaam kwa sababu anayeombwa ni Mungu tu na Jesus sii Mungu..Utanisamehe sana kuandika haya lakini hii ndio imani ya Waislaam na wanaposikia maneno kama haya unawaweka ktk wakati mgumu sana kukubaliana nawe hivyo kuharibu kabisa maombi yote! Vivyo hivyo kwa Mkristu, Muislaam anaposema lolote linalohusiana na Muhammad, mkristu hamuelewi isipokuwa anafumba macho na kuweka heshima ya imani ya waislaam ambayo kisiasa inaweza kupingana kabisa na neno la Mungu (biblia).

Kwa hiyo nachosema mimi, tujaribu sana kuyaweka mabo haya nje ya siasa na wala sio Udini isipokuwa kujihadhari na hapa tulipofikia kwani Udini umekuwa adui mwingine wa umaskini wa Mtanzania. Napinga kauli za kiimani zisitumike kisiasa, ila zitumike ktk mazingira ya maisha yetu kama ilivyokuwa zamani. Iwe ktk harusi, misiba, sala za chakula na kadhalika kuliko kutumiwa na viongozi wetu kisiasa ktk kuelezea matukio ya kisiasa..Na kilichotangulia mimi kusema haya ni kutokana na statement ya bibie ambayo mimi sikubaliani nayo kwamba mkono wa Mungu upo Chadema na kawanusuru kutokana na watu waliokuwa na nia mbaya..Je, hawa ni kina nani na wanalindwa na nani kama sii Mungu huyo huyo!...
 
Ninge kujibu ila kwasababu umesema umezaliwa yapata mwaka 1977, basi nakusamehe naamini ni utoto na akili ya makamasi inakusumbua sana au kwa vile ulizaliwa wakati CCM inazaliwa basi ulizaliwa na akili hasi au mtindio wa Ubongo!

Ushahidi kuwa unamtindio wa ubongo ni hayo maneno yako nadhani ubongo wako unafanya kazi kama trigger ya AK47 ni kusukumwa hamna kufikiri.

Umekalia kuti kavu, mkuu lazima udondoke, huna jipya
 
Mkuu samahani nilikuwa nimetoka ktk ukumbi huu kwa muda..Sijui kama nimekukwaza. Naam umeisema tafsiri ya Udini vizuri tu kama unavyoelewa wewe ingawa sii sahihi...sasa nikuulize ninapotumia maneno ya kiimani ya dini ktk siasa na hukubaliani nayo Je, huo ni Udini pia?.. nilichosema mimi ni kwamba tusipende sana kutumia imani za dini ktk siasa zinaweza kuharibu mchuzi mzima, kwani alichosema Regia mimi sikubaliani nacho na sidhani kama ni Udini iwe yeye alosema au mimi nisiyekubaliana naye..
Kweli unaweza tumia neno Mungu walati wowote lakini unapompa Mungu mkono juu ya Chama hali mimi sikubaliani na mawazo hayo ni sawa na kutokubaliana kisiasa...
Labda nikujuze kwa kutumia dini zenyewe ingawa haikuwa nia yangu kabisa kwa nini sipendi matumizi ya aya za dini ktk mihadhara ya kisiasa. Kwa mfano Mkristu anapoomba kwa jina la Yesu, hii ni kufuru kwa Waislaam kwa sababu anayeombwa ni Mungu tu na Jesus sii Mungu..Utanisamehe sana kuandika haya lakini hii ndio imani ya Waislaam na wanaposikia maneno kama haya unawaweka ktk wakati mgumu sana kukubaliana nawe hivyo kuharibu kabisa maombi yote! Vivyo hivyo kwa Mkristu, Muislaam anaposema lolote linalohusiana na Muhammad, mkristu hamuelewi isipokuwa anafumba macho na kuweka heshima ya imani ya waislaam ambayo kisiasa inaweza kupingana kabisa na neno la Mungu (biblia).

Kwa hiyo nachosema mimi, tujaribu sana kuyaweka mabo haya nje ya siasa na wala sio Udini isipokuwa kujihadhari na hapa tulipofikia kwani Udini umekuwa adui mwingine wa umaskini wa Mtanzania. Napinga kauli za kiimani zisitumike kisiasa, ila zitumike ktk mazingira ya maisha yetu kama ilivyokuwa zamani. Iwe ktk harusi, misiba, sala za chakula na kadhalika kuliko kutumiwa na viongozi wetu kisiasa ktk kuelezea matukio ya kisiasa..Na kilichotangulia mimi kusema haya ni kutokana na statement ya bibie ambayo mimi sikubaliani nayo kwamba mkono wa Mungu upo Chadema na kawanusuru kutokana na watu waliokuwa na nia mbaya..Je, hawa ni kina nani na wanalindwa na nani kama sii Mungu huyo huyo!...

..sis binadamu tunafanya mambo yote kulingana na dhamira inavyosema, sioni tatizo kabisa kwa mtu kutaja kile dhamira inachokiamini be it Yesu au hata shetani kwani huyo si ndo unamuamini..? kwa nini kuogopa! tatizo linakuja pale ambapo suala la imani linataka kufanywa kuwa la jumuia..! sivyo hivyo kabisa! suala la imani ni la mtu binafsi! kama yeye anataja Yesu ndio ngao na msaada wake ktk kufanikisha lolote analoamini its ok, wengine hatupaswi kukosoa, subiri au tafuta nawewe jukwaa umtamtaja huyo unayeamini ni msaada wako ktk mambo yote!

Hata shetani anawalinda wanaotenda sawa sawa na anavyotaka! mwizi anapokwenda kuiba na kuua si kweli Mungu anamlinda kufanya uhalifu! so hao wanaotakia wenzao mabaya si lazima wanalindwa na Mungu hata shetani anaweza kuwalinda ili watimize mabaya wanayokusudia! Mh Regia kumtanguliza Mungu kwenye chama chake ni vile anavyoamini yeye... wengine tunajifunza tu kwa kuona kama ni kweli huyo anayemuamini anafanya hayo mazuri ambayo jamii yote inafaidika nayo!
Kwa nini usikie vibaya kumtaja yule unayemuamini lakini..? mbona alipata kutokea mtu anasema dhahiri kuwa ana ulinzi wa majini na mapepo na hata kusema atayatuma kumlinda kiongozi wa nchi! ndio imani yake! mwache! wewe kinakukera nini, subiri au tafuta jukwaa na wewe utaje na kuonesha huyo unayemuani ana msaada gani kwako na hata kwa watu wengine! hili ni suala binafsi! dini ni suala binafsi!
 
Mkuu hujajibu hoja ya mkandara kabisaaaa umejikanyaga kanyaga tuuuu
Hata hivyo wito wangu kwa Mtema awe makini na mitandao ya kijamii kama hii, hapa si mahala pa kukurupuka na kuanza kuweka comments zaako za ajabu ajabu, ashukuru mods walimuokoa maana alisha chemka mbaya,
Iga mfano wa wenzako akina kitila mkumbo, zitto huwezi kuta wanakuja na hoja dhaifu dhaifu hapa
 
Back
Top Bottom