Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, amedai kuwa alishawishiwa kupewa fedha ili akubali chama hicho kiingie kwenye uchaguzi.
Heche ameyasema hayo wakati akihojiwa na Clouds TV, akieleza kuwa chama hicho kinapigania demokrasia na kwamba demokrasia hiyo inapaswa kuanza ndani ya chama chenyewe.
“Sisi tunapigania demokrasia, demokrasia haiwezi kuonekana nje ya chama, lazima ionekane ndani ya chama. Mimi nimeshawishiwa, nihongwe, nimeshawishiwa hata juzi kwenye uchaguzi, tuingize chama kwenye uchaguzi, nipewe fedha nikubali tuingize chama kwenye uchaguzi,” amesema Heche.