John Heche: Tukisema msiue watu kwenye uchaguzi tunaonekana wanaharakati, hatuoni shida kuitwa wanaharakati

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche, amesema chama hicho kimeamua kuendelea kudai mabadiliko ya kweli badala ya kufanya siasa kwa ajili ya kuonekana pekee. Heche amesema wanapozungumzia masuala yanayowagusa wananchi na kudai mabadiliko, baadhi ya watu wamekuwa wakiwaita wanaharakati, huku akisisitiza kuwa CHADEMA haitaki siasa ya “kupiga picha za uongo” bila kupigania mabadiliko halisi.

Heche amedai kuwa nchini kumekuwa na matukio ya watu kutekwa, akitaja majina ya Humphrey Polepole, Mdude Nyagali, Jacob Mlay, Deusdedith Soka na Ben Saanane miongoni mwa watu aliowataja katika maelezo yake.

Amesema wanapodai watu wasitekwe na kuhoji matukio hayo, badala ya kuitwa wanasiasa, wamekuwa wakielezwa kuwa ni wanaharakati. “Tukisema msisteke watu, hiyo inaonekana ni harakati. Wanataka tunyamazie hayo ionekane ni siasa,” amesema.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…