Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katika mahojiano yake na Wasafi FM, John Heche alitoa mtazamo wake kuhusu hali ya kisiasa, kuhama vyama, na msimamo wa Chadema kwa waliohama CHADEMA na kwenda Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA)
"Watu waliotoka kwa wingi ambao wamewahi kuwa viongozi kwenye chama hiki ni watu walioenda chama kinaitwa Chauma. Mara nyingi anatoka mtu mmoja, ameshawishiwa na nini... na sababu zinafahamika: watu waliambiwa huwezi kushinda, kulikuwa na ushawishi."
"Mtu amekaa Makao Makuu ya chama kwa miaka 25, hajawahi kuona ubaya wa chama. Kesho chama kimefanya uchaguzi, amekuja mwenyekiti mpya na timu mpya, wewe unaambiwa sasa rudi kule wilayani... unatoka unasema hiki chama ni kibaya. Hivi unaeleweka?"
"Watu walioondoka Chadema walitaka madaraka... ni watu waliotoka baada ya kukosa vyeo."
"Ni kama wewe umeachana na mke wako, unaanza kusema mke wangu kwanza kikojozi, huyu hafai; hukuwahi kusema ukiwa pale."