Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Ndg. John Heche amezungumza na watanzania jioni ya Tarehe 11 July 2026 nyumbani kwake Tarime mjini ambapo amewashukuru kwa simu na jumbe za pole.
Pia soma:Mnyika afafanua tuhuma za Heche na matumizi ya fedha za ToneTone
Hivi karibuni kiongozi huyo alifiwa na aliyekuwa Dereva wake marehemu Suez Maradufu ambaye Heche amesema amekuwa karibu na marehemu Suez tangu akiwa shuleni na akiwa miaka 16 marehemu Suez alikuwa ni Dereva wa Baba yake.
Heche ameongeza kuwa sio rahisi kujibu jumbe na simu ya kila mtu, kila kiongozi, kila mtanzania ndio maana ameamua kwa pamoja kujibu pole hizo.
Katika hatua nyingine Heche amebainisha kupokea simu nyingi kutoka kwa wanachama wa Chadema na watanzania kwa ujumla wanaotaka kumtumia fedha ili kumpa pole na kumtia moyo kama Kiongozi wa CHADEMA, akiomba wote walioguswa na harakati zake kutuma fedha hizo kwenye akaunti za chama ili kusaidia katika maandalizi ya Mkutano mkuu wa CHADEMA unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.