John Heche: Wanaonitumia fedha, wazitume kwenye akaunti ya CHADEMA

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Your browser is not able to display this video.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Ndg. John Heche amezungumza na watanzania jioni ya Tarehe 11 July 2026 nyumbani kwake Tarime mjini ambapo amewashukuru kwa simu na jumbe za pole.

Pia soma:Mnyika afafanua tuhuma za Heche na matumizi ya fedha za ToneTone

Hivi karibuni kiongozi huyo alifiwa na aliyekuwa Dereva wake marehemu Suez Maradufu ambaye Heche amesema amekuwa karibu na marehemu Suez tangu akiwa shuleni na akiwa miaka 16 marehemu Suez alikuwa ni Dereva wa Baba yake.

Heche ameongeza kuwa sio rahisi kujibu jumbe na simu ya kila mtu, kila kiongozi, kila mtanzania ndio maana ameamua kwa pamoja kujibu pole hizo.

Katika hatua nyingine Heche amebainisha kupokea simu nyingi kutoka kwa wanachama wa Chadema na watanzania kwa ujumla wanaotaka kumtumia fedha ili kumpa pole na kumtia moyo kama Kiongozi wa CHADEMA, akiomba wote walioguswa na harakati zake kutuma fedha hizo kwenye akaunti za chama ili kusaidia katika maandalizi ya Mkutano mkuu wa CHADEMA unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
 
What if akipokea hizo fedha na kuziwasilisha chadema kutakuwa na changamoto yoyote?
 
Kawajibu kisomi kabisa, hawa CCM wanakula mabilioni ila hawataki hata bunge lijadili ripoti ya CAG yenye taarifa za wizi wa mabilioni lakini cha ajabu wanaanzisha propaganda za wizi chadema huku wakijua hata hakipokei ruzuku tena!!

Hawa jamaa ni zaidi ya mashetani
 
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Heche anajua akipokea binafsi kelele zitaanza tena, kaamua ziende kwa account ya chama kuepusha maneno.

Binafsi sioni tatizo kama angeamua kupokea binafsi, kwasababu waliokuwa tayari kumchangia, walikuwa wakitaka kumchangia Heche kwasababu ya msiba alioupata wa kufiwa na dereva wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…