ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Malecela ametoa kauli kuhusu sakata la makubaliano ya uwekezaji wa bandari nchini na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya Dubai Port World (DPW).
Malecela ametoa kauli hiyo leo Jumapili Juni 25, 2023 baada ya kuulizwa swali kuhusiana na uwekezaji huo unaohusisha Serikali hizo mbili.
Malecela amesema haoni shida ya uwekezaji huo na amewashangaa wanaopinga akisema ndio demokrasia inavyowaruhusu.
"Kwanza wako wachache wanaopinga na sioni hoja yao," amesema Malecela ambaye ni Waziri Mkuu wa saba wa Tanzania akipokea nafasi hiyo kutoka kwa Jaji Joseph Warioba.
Leo, Malecela amekutana na waandishi wa habari nyumbani kwake eneo la Kilimani jijini Dodoma akielezea kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaotanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwananchi