Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika, amedai kuwa kuna juhudi za kuhamisha mwelekeo kutoka kwenye kampeni ya 'No Reforms, No Election'. Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa X, Mnyika amesisitiza kuwa maamuzi ya Baraza Kuu la CHADEMA yaliyofanyika tarehe 22 Januari 2025 ni halali, kwani yalihusisha wajumbe halali 234 kati ya 412, sawa na asilimia 56.8, kwa mujibu wa Katiba ya chama ibara ya 6.2.2.
Pia, Soma: Team Mbowe wajidhatiti kumkwamisha LISSU , wapinga uteuzi wa Wajumbe watano wa kamati kuu aloufanya Lissu, waandika Barua kwa msajili wa Vyama
Aidha, Mnyika ameeleza kuwa kikao hicho kilifanya uthibitishaji kwa mujibu wa Katiba ibara ya 7.7.12 (c) na (e), na hakukuwa na ajenda ya uchaguzi.
Ameeleza kuwa hatua ya kuwasilisha nakala ya barua kwa Msajili wa Vyama vya Siasa inadhihirisha kuwepo kwa nia ovu inayofanyika kwa siri dhidi ya chama hicho.