Pre GE2025 John Mnyika adai kuna hujuma za kuyumbisha harakati za 'No Reforms No Election' kufuatia pingamizi la uteuzi wa vigogo nane CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika, amedai kuwa kuna juhudi za kuhamisha mwelekeo kutoka kwenye kampeni ya 'No Reforms, No Election'. Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa X, Mnyika amesisitiza kuwa maamuzi ya Baraza Kuu la CHADEMA yaliyofanyika tarehe 22 Januari 2025 ni halali, kwani yalihusisha wajumbe halali 234 kati ya 412, sawa na asilimia 56.8, kwa mujibu wa Katiba ya chama ibara ya 6.2.2.

Pia, Soma: Team Mbowe wajidhatiti kumkwamisha LISSU , wapinga uteuzi wa Wajumbe watano wa kamati kuu aloufanya Lissu, waandika Barua kwa msajili wa Vyama

Aidha, Mnyika ameeleza kuwa kikao hicho kilifanya uthibitishaji kwa mujibu wa Katiba ibara ya 7.7.12 (c) na (e), na hakukuwa na ajenda ya uchaguzi.

Ameeleza kuwa hatua ya kuwasilisha nakala ya barua kwa Msajili wa Vyama vya Siasa inadhihirisha kuwepo kwa nia ovu inayofanyika kwa siri dhidi ya chama hicho.

Mnyika si wa kuaminika sana!
 
Chadema imeanza rasmi safari ya kujifia kama ilivyokua TLP na CUF. Ni suala la muda tu. Huenda hata uchaguzi mkuu wasishiriki 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Siasa si ujuaji tu, Bali na ujanja pia. Karne ya Sasa si rahisi mshamba akaongoza taasisi kubwa na kufanikiwa.
 
Chadema imeanza rasmi safari ya kujifia kama ilivyokua TLP na CUF. Ni suala la muda tu. Huenda hata uchaguzi mkuu wasishiriki 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Uchaguzi mkuu kama hawatashiriki sio kwasababu ya hawa wahuni. Usitake kuona unaweza kutupoteza maboya. Tatizo la chaguzi zetu ni tume hii ya rais na katiba inayolinda chama kimoja. Usitegemee kwamba hatujui tofauti ya mambo haya.
 
Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika, amedai kuwa kuna juhudi za kuhamisha mwelekeo kutoka kwenye kampeni ya 'No Reforms, No Election'. Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa X, Mnyika amesisitiza kuwa maamuzi ya Baraza Kuu la CHADEMA yaliyofanyika tarehe 22 Januari 2025 ni halali, kwani yalihusisha wajumbe halali 234 kati ya 412, sawa na asilimia 56.8, kwa mujibu wa Katiba ya chama ibara ya 6.2.2.

Pia, Soma: Team Mbowe wajidhatiti kumkwamisha LISSU , wapinga uteuzi wa Wajumbe watano wa kamati kuu aloufanya Lissu, waandika Barua kwa msajili wa Vyama

Aidha, Mnyika ameeleza kuwa kikao hicho kilifanya uthibitishaji kwa mujibu wa Katiba ibara ya 7.7.12 (c) na (e), na hakukuwa na ajenda ya uchaguzi.

Ameeleza kuwa hatua ya kuwasilisha nakala ya barua kwa Msajili wa Vyama vya Siasa inadhihirisha kuwepo kwa nia ovu inayofanyika kwa siri dhidi ya chama hicho.

Mwamba wa. Kaskazini🤣🤣
 
Tundu Lisu aonyeshe ukomavu na uvumilivu ili kumaliza changamoto za aina hii kama alivyokuwa mtanguizi wake.
Kama kuna wana Chadema wana hoja wasibezwe, wasikilizwe ili chama kiende mbele.
Kuna hoja na nogwa, team Mbowe wakubali uchaguzi umeisha, na mtu wao kashindwa kihalali. Kama kuna hela wamepewa na ccm il Lisu asiwe mwenyekiti, basi waangalie namna ya kuzirudisha.
 
Kampeni za kujazana chuki na kwenda kwenye media kuongeleana bila staha zimeleta mpasuko ndani ya chama, maamuzi ya 56% ya baraza kuu yanaweza kuwa halali, ila siyo jambo la kujivunia.

Jitihada kubwa baada ya uchaguzi zingeenda kwenye kukiunganisha tena chama na wagombea wote kukaa mezani, kuombana msamaha na kutoa maazimio ya pamoja ili kuvunja makundi. Ila Ego na mamluki wa kila upande wamewatia upofu viongozi wetu.

Ukirudi kwenye historia utaona "Ego ndiyo downfall ya wanasiasa wengi duniani", ni wakati wa kuweka hisia pembeni na kujitafakari.
Inaonekana Mbowe na genge lake walijiaminisha cdm ni mali yao, kwa sasa wanashindwa kuushi ukweli uliopo. Kuombana msamaha ni kutaka kuwapa nafasi ya kupenyeza ajenda za hela walizohongwa. Wakae kwa kutulia, muda wa Mbowe ulishaisha, aache chama kijengwe na wengine, ama akaanzishe chama kingine watu wamfuate huko.
 
Chadema imeanza rasmi safari ya kujifia kama ilivyokua TLP na CUF. Ni suala la muda tu. Huenda hata uchaguzi mkuu wasishiriki 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Ilipofikia chadema kufa ni ndoto za mchana , chama kwa sasa kina nguvu sana, hakuna wa kudhubutu
 
Ningekuwa Lissu ningewatimua mamluki wa Mbowe wote ndani ya chama ili nikinyooshe chama

Kuishi kiccm ndani ya chadema ni ujinga Sana

Lissu safisha nyumba kwanza mpini umeshika wewe leta watu potential ndani ya chama achana na Wala pesa Abdul na Samia!!
Wala hakuna haja ya kuwatimua. Watajiondoa wenyewe ni suala la muda tu.
 
Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika, amedai kuwa kuna juhudi za kuhamisha mwelekeo kutoka kwenye kampeni ya 'No Reforms, No Election'. Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa X, Mnyika amesisitiza kuwa maamuzi ya Baraza Kuu la CHADEMA yaliyofanyika tarehe 22 Januari 2025 ni halali, kwani yalihusisha wajumbe halali 234 kati ya 412, sawa na asilimia 56.8, kwa mujibu wa Katiba ya chama ibara ya 6.2.2.

Pia, Soma: Team Mbowe wajidhatiti kumkwamisha LISSU , wapinga uteuzi wa Wajumbe watano wa kamati kuu aloufanya Lissu, waandika Barua kwa msajili wa Vyama

Aidha, Mnyika ameeleza kuwa kikao hicho kilifanya uthibitishaji kwa mujibu wa Katiba ibara ya 7.7.12 (c) na (e), na hakukuwa na ajenda ya uchaguzi.

Ameeleza kuwa hatua ya kuwasilisha nakala ya barua kwa Msajili wa Vyama vya Siasa inadhihirisha kuwepo kwa nia ovu inayofanyika kwa siri dhidi ya chama hicho.

Huyo mwana CHADEMA aliyelalamika/pinga uteuzi huo kuwa haukuzingatia matakwa ya kikatiba ameshajibiwa..?

Yeye ametumia vifungu vya katiba kupinga uteuzi huo kwa kudai kuwa akidi ya kuhalalisha uteuzi wa wajumbe uliofanywa na Mwenyekiti haikutimia...

Mimi nilitegemea Katibu mkuu ayaweke wazi malalamiko ya huyo mwana CHADEMA na kisha aweke wazi majibu ya chama kumjibu huyo mwanachama..

Lakini ninachokiona hapa ni kuhusishwa kwa msajili wa vyama vya siasa. Najiuliza huyu kaingiaje tena? Au mlalamikaji huyu alielekezwa na mjasili wa vyama vya siasa kulalamika..?

I don't get this. Hebu tuelekezane jamani..
 
Inaonekana Mbowe na genge lake walijiaminisha cdm ni mali yao, kwa sasa wanashindwa kuushi ukweli uliopo. Kuombana msamaha ni kutaka kuwapa nafasi ya kupenyeza ajenda za hela walizohongwa. Wakae kwa kutulia, muda wa Mbowe ulishaisha, aache chama kijengwe na wengine, ama akaanzishe chama kingine watu wamfuate huko.
Si bure, Kijani wametumia strategy ya "Divide and conquer"

Chama hakiwezi kufikia malengo kama kuna kundi kubwa la kukisabotage liko ndani ya chama.
Tutawezaje kupambana na kijani kama tayari tunapigana wenyewe kwa wenyewe? hasa katika mwaka wa uchaguzi?

Hebu tuwe serious kidogo na tuweke mihemko pembeni.
 
Iko hivi, kundi la Mbowe naona halikubali kuwa limeshindwa, na hakuna haja ya kuwabembeleza. Uchaguzi umefanyika na wameshindwa kihalali. Tatizo kwenye uchaguzi wetu si umoja ndani ya chama, bali hujuma za wazi toka kwa vyombo vya dola ili kuibeba ccm. Hivyo cdm wawe wamoja, ama vipande tatizo la kwenye chaguzi zetu halina mahusiano na mwenendo wa ndani ya chama.
 
Chadema imeanza rasmi safari ya kujifia kama ilivyokua TLP na CUF. Ni suala la muda tu. Huenda hata uchaguzi mkuu wasishiriki 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Atakufa nnanako, Mamako, na wewe, mtaiacha CHADEMA,kama JIWE MAGUFULI'S alivyoshindwa 🤣🤣🤣😅🤣😅
 
Iko hivi, kundi la Mbowe naona halikubali kuwa limeshindwa, na hakuna haja ya kuwabembeleza. Uchaguzi umefanyika na wameshindwa kihalali. Tatizo kwenye uchaguzi wetu si umoja ndani ya chama, bali hujuma za wazi toka kwa vyombo vya dola ili kuibeba ccm. Hivyo cdm wawe wamoja, ama vipande tatizo la kwenye chaguzi zetu halina mahusiano na mwenendo wa ndani ya chama.
Narudia, hili ni jambo la kulikalia chini na kujadili, kukosekana kwa jitihada za makusudi za kukiunganisha chama ni anguko tunalolitengeneza.

Uzuri wa kuwagawanya watu ili kuwatawala ni kwamba huhitaji tena nguvu ya dola, watapigana wao wenyewe kwa wenyewe.

Mfano; Viongozi wa kikanda, mikoa na wilaya ambao hawakumpigia kura Lissu (asilimia 48% ya viongozi wote) wakiamua kutowahimiza wananchi wao kushiriki uchaguzi au wakiamua kutotoa ushirikiano kwenye mchakato wa uchaguzi for CHADEMA, kuna haja gani ya nguvu ya dola? Mbona tayari kijani wanapenya bila maguvu.

Kama nilivyosema pale mwanzo, tujitafakari bila mihemko.
 
Back
Top Bottom