Pre GE2025 John Mnyika adai kuna hujuma za kuyumbisha harakati za 'No Reforms No Election' kufuatia pingamizi la uteuzi wa vigogo nane CHADEMA

Pre GE2025 John Mnyika adai kuna hujuma za kuyumbisha harakati za 'No Reforms No Election' kufuatia pingamizi la uteuzi wa vigogo nane CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Narusia, hili ni jambo la kulikalia chini na kujadili, kukosekana kwa jitihada za makusudi za kukiunganisha chama ni anguko tunalolitengeneza.

Uzuri wa kuwagawanya watu ili kuwatawala ni kwamba huhitaji tena nguvu ya dola, watapigana wao wenyewe kwa wenyewe.
Mfano; Viongozi wa kikanda, mikoa na wilaya ambao hawakumpigia kura Lissu (asilimia 48% ya viongozi wote) wakiamua kutowahimiza wananchi wao kushiriki uchaguzi au wakiamua kutotoa ushirikiano kwenye mchakato wa uchaguzi for CHADEMA, kuna haja gani ya nguvu ya dola? Mbona tayari kijani wanapenya bila maguvu.

Kama nilivyosema pale mwanzo, tujitafakari bila mihemko.
Hao wajumbe waliopiga kura kwa mbowe kinyume na msimamo wa wapiga kura hawana maana yeyote na hakuna haja ya kuwahofia.
Wanachama wengi wanamuunga mkono Lisu huku site.
 
Narudia, hili ni jambo la kulikalia chini na kujadili, kukosekana kwa jitihada za makusudi za kukiunganisha chama ni anguko tunalolitengeneza.

Uzuri wa kuwagawanya watu ili kuwatawala ni kwamba huhitaji tena nguvu ya dola, watapigana wao wenyewe kwa wenyewe.

Mfano; Viongozi wa kikanda, mikoa na wilaya ambao hawakumpigia kura Lissu (asilimia 48% ya viongozi wote) wakiamua kutowahimiza wananchi wao kushiriki uchaguzi au wakiamua kutotoa ushirikiano kwenye mchakato wa uchaguzi for CHADEMA, kuna haja gani ya nguvu ya dola? Mbona tayari kijani wanapenya bila maguvu.

Kama nilivyosema pale mwanzo, tujitafakari bila mihemko.
Wewe uko na akili mingi, CCM ni dude kubwa sana. Walijua Lissu sio kiongozi hawezi kuunganisha chama CCM walikuwa wanachochea moto kupitia makada wao akina Msigwa. CDM itajifikia kilo cha kawaida
 
Hao wajumbe waliopiga kura kwa mbowe kinyume na msimamo wa wapiga kura hawana maana yeyote na hakuna haja ya kuwahofia.
Wanachama wengi wanamuunga mkono Lisu huku site.
Nashangazwa sana na namna tunavyorahisisha mambo. Kipindi cha uchaguzi ukikosa almost nusu ya viongozi wako wilayani na mikoani, utausimamia vipi uchaguzi ikiwemo shughuli za kampeni na kulinda kura?

Viongozi wa chama, wawe team Lissu au Mbowe ndiyo wana dhamana ya kukisimamia chama huko kwenye maeneo yao. Anyway, ngoja tuone mambo yatakavyokua.
 
Lissu ana kazi kubwa ya kukiunganisha chama. Mara Aidan hachangii hapo ataweza kweli.
 
Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika, amedai kuwa kuna juhudi za kuhamisha mwelekeo kutoka kwenye kampeni ya 'No Reforms, No Election'. Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa X, Mnyika amesisitiza kuwa maamuzi ya Baraza Kuu la CHADEMA yaliyofanyika tarehe 22 Januari 2025 ni halali, kwani yalihusisha wajumbe halali 234 kati ya 412, sawa na asilimia 56.8, kwa mujibu wa Katiba ya chama ibara ya 6.2.2.

Pia, Soma: Team Mbowe wajidhatiti kumkwamisha LISSU , wapinga uteuzi wa Wajumbe watano wa kamati kuu aloufanya Lissu, waandika Barua kwa msajili wa Vyama

Aidha, Mnyika ameeleza kuwa kikao hicho kilifanya uthibitishaji kwa mujibu wa Katiba ibara ya 7.7.12 (c) na (e), na hakukuwa na ajenda ya uchaguzi.

Ameeleza kuwa hatua ya kuwasilisha nakala ya barua kwa Msajili wa Vyama vya Siasa inadhihirisha kuwepo kwa nia ovu inayofanyika kwa siri dhidi ya chama hicho.

Amejibu vizuri. Naamini ana majina ya wajumbe halali waliohudhuria kikao hicho. Yeye ni mtendaji , asiingie katika mtego wa kuona kila anaehoji utendaji wa CDM kuwa ana nia mbaya.

Amandla...
 
Zama za sasa si zile za zamani......... Tuishi Kwa nyakati za sasa tukihusisha zama zile, si kuishi zama zile tukihusisha na zama za sasa. Kuna watu wanalazimsha kisichowezekana. Zama za sasa zina mabadiliko na zinahitaji mabadiliko zaidi.
 
Chadema imeanza rasmi safari ya kujifia kama ilivyokua TLP na CUF. Ni suala la muda tu. Huenda hata uchaguzi mkuu wasishiriki 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
yanaanzaga hivi hivi....tatizo ni Lisu and Heche kutoona umuhimu wa reconciliation kwa uharibufu walioufanya wao kwenye kampeni! Ujuaji mwingi usio na maana ....
 
Back
Top Bottom