Pre GE2025 John Mnyika adai kuna hujuma za kuyumbisha harakati za 'No Reforms No Election' kufuatia pingamizi la uteuzi wa vigogo nane CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mnyika si wa kuaminika sana!
 
Sultan Mbowe katulia pembeni anawatuma watwana wake ili kuhalalaisha zile 12b alizopewa na mama Abdul
Huyu Mzee wa hovyo sana, yeye ndo dairekta Lissu na Heche wawe makini sana mzee kile kiti bado anakitaka
 
Chadema imeanza rasmi safari ya kujifia kama ilivyokua TLP na CUF. Ni suala la muda tu. Huenda hata uchaguzi mkuu wasishiriki 🀣🀣🀣🀣🀣🀣
Siasa si ujuaji tu, Bali na ujanja pia. Karne ya Sasa si rahisi mshamba akaongoza taasisi kubwa na kufanikiwa.
 
Chadema imeanza rasmi safari ya kujifia kama ilivyokua TLP na CUF. Ni suala la muda tu. Huenda hata uchaguzi mkuu wasishiriki 🀣🀣🀣🀣🀣🀣
Uchaguzi mkuu kama hawatashiriki sio kwasababu ya hawa wahuni. Usitake kuona unaweza kutupoteza maboya. Tatizo la chaguzi zetu ni tume hii ya rais na katiba inayolinda chama kimoja. Usitegemee kwamba hatujui tofauti ya mambo haya.
 
Mwamba wa. Kaskazini🀣🀣
 
Tundu Lisu aonyeshe ukomavu na uvumilivu ili kumaliza changamoto za aina hii kama alivyokuwa mtanguizi wake.
Kama kuna wana Chadema wana hoja wasibezwe, wasikilizwe ili chama kiende mbele.
Kuna hoja na nogwa, team Mbowe wakubali uchaguzi umeisha, na mtu wao kashindwa kihalali. Kama kuna hela wamepewa na ccm il Lisu asiwe mwenyekiti, basi waangalie namna ya kuzirudisha.
 
Inaonekana Mbowe na genge lake walijiaminisha cdm ni mali yao, kwa sasa wanashindwa kuushi ukweli uliopo. Kuombana msamaha ni kutaka kuwapa nafasi ya kupenyeza ajenda za hela walizohongwa. Wakae kwa kutulia, muda wa Mbowe ulishaisha, aache chama kijengwe na wengine, ama akaanzishe chama kingine watu wamfuate huko.
 
Chadema imeanza rasmi safari ya kujifia kama ilivyokua TLP na CUF. Ni suala la muda tu. Huenda hata uchaguzi mkuu wasishiriki 🀣🀣🀣🀣🀣🀣
Ilipofikia chadema kufa ni ndoto za mchana , chama kwa sasa kina nguvu sana, hakuna wa kudhubutu
 
Wala hakuna haja ya kuwatimua. Watajiondoa wenyewe ni suala la muda tu.
 
Huyo mwana CHADEMA aliyelalamika/pinga uteuzi huo kuwa haukuzingatia matakwa ya kikatiba ameshajibiwa..?

Yeye ametumia vifungu vya katiba kupinga uteuzi huo kwa kudai kuwa akidi ya kuhalalisha uteuzi wa wajumbe uliofanywa na Mwenyekiti haikutimia...

Mimi nilitegemea Katibu mkuu ayaweke wazi malalamiko ya huyo mwana CHADEMA na kisha aweke wazi majibu ya chama kumjibu huyo mwanachama..

Lakini ninachokiona hapa ni kuhusishwa kwa msajili wa vyama vya siasa. Najiuliza huyu kaingiaje tena? Au mlalamikaji huyu alielekezwa na mjasili wa vyama vya siasa kulalamika..?

I don't get this. Hebu tuelekezane jamani..
 
Si bure, Kijani wametumia strategy ya "Divide and conquer"

Chama hakiwezi kufikia malengo kama kuna kundi kubwa la kukisabotage liko ndani ya chama.
Tutawezaje kupambana na kijani kama tayari tunapigana wenyewe kwa wenyewe? hasa katika mwaka wa uchaguzi?

Hebu tuwe serious kidogo na tuweke mihemko pembeni.
 
Iko hivi, kundi la Mbowe naona halikubali kuwa limeshindwa, na hakuna haja ya kuwabembeleza. Uchaguzi umefanyika na wameshindwa kihalali. Tatizo kwenye uchaguzi wetu si umoja ndani ya chama, bali hujuma za wazi toka kwa vyombo vya dola ili kuibeba ccm. Hivyo cdm wawe wamoja, ama vipande tatizo la kwenye chaguzi zetu halina mahusiano na mwenendo wa ndani ya chama.
 
Chadema imeanza rasmi safari ya kujifia kama ilivyokua TLP na CUF. Ni suala la muda tu. Huenda hata uchaguzi mkuu wasishiriki 🀣🀣🀣🀣🀣🀣
Atakufa nnanako, Mamako, na wewe, mtaiacha CHADEMA,kama JIWE MAGUFULI'S alivyoshindwa πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…
 
Narudia, hili ni jambo la kulikalia chini na kujadili, kukosekana kwa jitihada za makusudi za kukiunganisha chama ni anguko tunalolitengeneza.

Uzuri wa kuwagawanya watu ili kuwatawala ni kwamba huhitaji tena nguvu ya dola, watapigana wao wenyewe kwa wenyewe.

Mfano; Viongozi wa kikanda, mikoa na wilaya ambao hawakumpigia kura Lissu (asilimia 48% ya viongozi wote) wakiamua kutowahimiza wananchi wao kushiriki uchaguzi au wakiamua kutotoa ushirikiano kwenye mchakato wa uchaguzi for CHADEMA, kuna haja gani ya nguvu ya dola? Mbona tayari kijani wanapenya bila maguvu.

Kama nilivyosema pale mwanzo, tujitafakari bila mihemko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…