John Mnyika ajibu tuhuma za Tundu Lissu kuhusu rushwa, adai tuhuma zenye ushahidi kupelekwe kwenye vikao vya Kikatiba vya Chama

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amejibu tuhuma za Tundu Lissu, adai tuhuma zenye ushahidi kupelekwe kwenye vikao vya Kikatiba vya Chama

"Ikiwa kuna kiongozi yeyote au mtu yoyote kwa maana ya mwanachama wa CHADEMA anatuhuma dhidi ya yeyote aziwasilishe ili zishughulikiwa kwa mujibu wa Katiba, Itifaki na maandili ya Chama na sikutoa tuhuma za jumla jumla"

Pia, Soma:

CHADEMA hali inazidi kuwa tete. John Mrema asema kama kuna ushahidi wa tuhuma za Rushwa uwasilishwe haraka kwaajili ya hatua za kinidhamu
 
View attachment 3177933
Pia, Soma:

CHADEMA hali inazidi kuwa tete. John Mrema asema kama kuna ushahidi wa tuhuma za Rushwa uwasilishwe haraka kwaajili ya hatua za kinidhamu
Uko sahihi
 
Siasa tupu hana jipya kwangu sionagi tofauti ya ccm na chadema wote wana majibu yale yale kuna uhaba wa mtendaji genius sio kama hao waliopo.
Hataki tuhuma za jumla jumla, lkn yeye anatoa majibu ya jumla jumla.

Nilitegemea kwa nafasi yake kama katibu mkuu ajibu hoja baada hoja ktk hotuba ya Lisu iliyoleta sintofahamu miongoni mwa wanachama.
 
Kama Makamu asiye na ofisi na nyenzo nyingine za kiutendaji,
ameweza kubaini kwamba uchaguzi wenu wa ndani ulikuwa una hela nyingi,zisizo na maelezo kwanini Katibu Mkuu hufahamu hili?...Mnyika nakufahamu.,upstairs sina shaka nawe..usiingie kwenye huu MTEGO
 
Lissu hajui haha matakwa ya katiba halafu ndio aongoze chama na nchi?
 
Hoja za jumla jumla hazijibiki. Unamjibu vipi mtu anayesema CDM kumejaa rushwa bila kuwataja wala rushwa wanaohusika? Mtu akisema pesa za Chadema zinaingia katika akaunti binafsi, unamjibu vipi kama hajataja ni akaunti ya nani inayopokelea pesa? Na tukumbuke kuwa CDM inakaguliwa na suala kama hilo lingeibuliwa na CAG maana ni grassroots mismanagement ya fedha za chama.

Nakumbuka Lijualikali alivyolia Bungeni akielezea jinsi Mbowe alivyojinunulia mashamba Kilombero. Spika akaagiza Takukuru iangalie na Lijualikali akaahidi kutoa ushirikiano. Yako wapi?

Amandla...
 
Hataki tuhuma za jumla jumla, lkn yeye anatoa majibu ya jumla jumla.

Nilitegemea kwa nafasi yake kama katibu mkuu ajibu hoja baada hoja ktk hotuba ya Lisu iliyoleta sintofahamu miongoni mwa wanachama.
Sintofahamu ipi imeletwa kwenye hotuba ya lissu labda wenye ubongo mdogo ndo wanaona Kuna sintofahamu.
 
Hana content kabisa tayari unaona iko upande gani katika siasa kwa viongozi kama hao hi Tanzania bado sana, hatuna mbadala wa dhati wa CCM.
 
1. Chama kinamtegemea mtu na marafiki wa mtu kutafuta fedha. Lisu anasema kuwe na mfumo pamoja marafiki wa chama wa kutafuta fedha za kuendeshwa shughuli za chama.

2. Kutokuwepo kwa ukomo wa nafasi ya mwenyekiti kulikozua na kukomaza uchawa ndani ya chadema . Lisu anasema ukomo uwekwe ili kuondoa uchawa.
3. Mashambulizi kuelekezwa kwa Lisu mara tu alipotangaza Nia yake ya kugombea uenyekiti.

Haya yalipaswa kuelezwa na katibu mkuu Mnyika. Inakuwaje yapo wakati hiki ni chama mbada wa ccm tulitege mea kiwe kisafi na kiendeshwe kwa misingi yote ya demokrasia??
 
Kweli kabisa. Ni kama alikuwa ana muwakilisha mtu fulani pale.
 
Mtu akisema pesa za Chadema zinaingia katika akaunti binafsi, unamjibu vipi kama hajataja ni akaunti ya nani inayopokelea pesa?
Yericko Nyerere Nyerere mwanachama mtiifu na kiongozi wa chadema amesema Mbowe ndiye mwenye hela, Mbowe ndiyo sponsor na Mbowe ndiye ana marafiki wanaotoa pesa. Mpk hapa ushajua akaunti inayopokea pesa ni ya nani.
 
1. Chama kinamtegemea mtu na marafiki wa mtu kutafuta fedha. Lisu anasema kuwe na mfumo pamoja marafiki wa chama wa kutafuta fedha za kuendeshwa shughuli za chama.

2. Kutokuwepo kwa ukomo wa nafasi ya mwenyekiti kulikozua na kukomaza uchawa ndani ya chadema . Lisu anasema ukomo uwekwe ili kuondoa uchawa.
3. Mashambulizi kuelekezwa kwa Lisu mara tu alipotangaza Nia yake ya kugombea uenyekiti.

Haya yalipaswa kuelezwa na katibu mkuu Mnyika. Inakuwaje yapo wakati hiki ni chama mbada wa ccm tulitege mea kiwe kisafi na kiendeshwe kwa misingi yote ya demokrasia??
Chadema imeshindwa kutenganisha chama kama independent entity kutoka kwa personality chama sio mtu au kabila kinapashwa kiwe na mfumo wa kujiendesha bila kutegemea mtu yoyote awe maarufu au kiongozi..kwa hill CCM inawazidi mbali CCM uwe nani au nani huwezi kua juu ya chama malengo ya chama kupewa kipaombele hata uweke nani CCM wata sapoti huyu mtu ilimradi wanapata Utawal nguvu Mamlaka ya dola.
 
Back
Top Bottom