John Mnyika ajibu tuhuma za Tundu Lissu kuhusu rushwa, adai tuhuma zenye ushahidi kupelekwe kwenye vikao vya Kikatiba vya Chama

John Mnyika ajibu tuhuma za Tundu Lissu kuhusu rushwa, adai tuhuma zenye ushahidi kupelekwe kwenye vikao vya Kikatiba vya Chama

Ajibu nini wakati hajapelekewa hizo tuhuma rasimi.
Urasmi gani inatakiwa hapo, wakati mtoa shutuma ni Lisu, makamu mwenyekiti wa chadema??

Lisu angekuwa kama mm au wewe tungesema tuhuma siyo rasmi.
 
Urasmi gani inatakiwa hapo, wakati mtoa shutuma ni Lisu, makamu mwenyekiti wa chadema??

Lisu angekuwa kama mm au wewe tungesema tuhuma siyo rasmi.
Kwahiyo unataka Katibu akisikia tuhuma mitandaoni anaita press kujibu.
 
Kwahiyo unataka Katibu akisikia tuhuma mitandaoni anaita press kujibu.
Lisu aliitisha press, hakuandika mitandaoni na makamu mwenyekiti wa chama. Kauli yake haipuuzwi na watanzania bali inavhukuliwa kwa uzito.

. Kama Kuna jambo siyo sawa, Mnyika alipaswa kulitolea ufafanuzi badala ya kujificha kwenye urasmi wa taarifa. Vinginevyo watu wataamini.
 
kwani michango binafsi aloomba makamu mwenyekiti kuchangiwa kupitia platforms za chadeama imeenda kwenye mfuko wa nani na kwa maslahi ya nani?
Acha Uzezeta wa fikra, michango ya Lissu aliyochangiwa na kila Mtanzania ni kwanini iingie kwenye Akaunti za Chama?
 
Acha Uzezeta wa fikra, michango ya Lissu aliyochangiwa na kila Mtanzania ni kwanini iingie kwenye Akaunti za Chama?
relax basi na uwealeze wadau taratibu gentleman :pedroP:

sasa sia aombe kuchangiwa bila kutumia pltfoms za chadema?

hata chadema kwa ujumla wake hungangiwa na wanachama wa ndani na nje ya nchi, wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi wadau wa siasa na marafiki wa chadema. lakini pia hutumika kwa maslahi ya chadema kwa ujumla.

huyo kibaraka aache kutumia platfoms za chadema kujinufaisha binafs:BASED:
 
Hataki tuhuma za jumla jumla, lkn yeye anatoa majibu ya jumla jumla.

Nilitegemea kwa nafasi yake kama katibu mkuu ajibu hoja baada hoja ktk hotuba ya Lisu iliyoleta sintofahamu miongoni mwa wanachama.

Hoja za Lisu ni hisia tu aka mawazo yake hazina ushahidi ndiyo maana hazikufika kwenye vikao sahihi
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amejibu tuhuma za Tundu Lissu, adai tuhuma zenye ushahidi kupelekwe kwenye vikao vya Kikatiba vya Chama

"Ikiwa kuna kiongozi yeyote au mtu yoyote kwa maana ya mwanachama wa CHADEMA anatuhuma dhidi ya yeyote aziwasilishe ili zishughulikiwa kwa mujibu wa Katiba, Itifaki na maandili ya Chama na sikutoa tuhuma za jumla jumla"
View attachment 3177933
Pia, Soma:

CHADEMA hali inazidi kuwa tete. John Mrema asema kama kuna ushahidi wa tuhuma za Rushwa uwasilishwe haraka kwaajili ya hatua za kinidhamu
A good dance must know when to leave the stage. Kama Mbowe ataendelea kusikiliza chawa wake badala ya kusikiliza ukweli basi ataharibu kazi aliyo ifanya kwa guvu na mateso kwa mda mlefu sana. Majuto ni mjukuu.
 
Lisu aliitisha press, hakuandika mitandaoni na makamu mwenyekiti wa chama. Kauli yake haipuuzwi na watanzania bali inavhukuliwa kwa uzito.

. Kama Kuna jambo siyo sawa, Mnyika alipaswa kulitolea ufafanuzi badala ya kujificha kwenye urasmi wa taarifa. Vinginevyo watu wataamini.
Kaambiwa apeleke tuhuma rasimi ofisini na sio mlimani city.
 
Wewe muamala wako wa kazi yako ya Uchawa wa Lumumba kitengo cha JF Dr. Nchimbi huwa anautuma kwenye akaunti za CCM?
relax tu gentleman,

ni muhimu sana kibaraka akajitafakari upya juu ya azma yake ya kuutaka uenyekiti wa chadema hali ya kua ni mbinafs, mchoyo, mpigakelele na mpiga mdomo asie na mipango..

wenye mipango hawana papara, achukue ujumbe wake kwa mwenyekiti wa kanda ya Pwani, itamsaidia sana :pedroP:
 
Kaambiwa apeleke tuhuma rasimi ofisini na sio mlimani city.
Zitafanyiwa kazi akizipeleka? Yawezekana anajua mizengwe iliyomo ndani ndiyo maana Kaona amwage mchele kwenye kuku wengi.
 
Zitafanyiwa kazi akizipeleka? Yawezekana anajua mizengwe iliyomo ndani ndiyo maana Kaona amwage mchele kwenye kuku wengi.
Kwahiyo hao kuku wengi watamsaidia nini, yeye aukubali mfumo wa Chadema alioukuta kama ambavyo Msigwa kaukubali mfumo wa CCM alioukuta.
 
Lissu tunakupenda ila ungekuwa na nia ya dhati ya uutaka uwenyekiti usingetumia njia hiyo na kumtuhumu wenyekiti na kukisema chama hadharani.

Kwa hiyo usije ukapata kura 7 afu ukaanza kusema umeibiwa.

CDM ni Mbowe na Mbowe ni CDM. Mwenyekiti ajaye wa CDM ni LAZIMA apate baraka zote toka kwa Mbowe na wanachama watamchagua bila shaka.

Lissu achana na uwenyekiti kwa sasa, utaporomoka zaidi ya Dr. Slaa - tunakushauri mapemaaa.
 
Kwahiyo hao kuku wengi watamsaidia nini, yeye aukubali mfumo wa Chadema alioukuta kama ambavyo Msigwa kaukubali mfumo wa CCM alioukuta.
Kwahiyo unakubali kuwa ccm = chadema? Na kama ndivyo unaushawishi vipi umma kuachana na ccm ikiwa kinachofanywa ccm ni sawa na kinachofanywa chadema??
 
Back
Top Bottom