Nyalandu na Mashinji Wamehujumiwa na DJ wao.. Chadema Ni chama Cha hovyo Sana kuwahi kutokea.
How comes unasusa uchaguzi na kuwanyima wananchi haki ya kumpata kiongozi wao wanae mpenda kwa kigezo Cha demokrasia mbovu harafu Wewe kwenye uchaguzi wa chama unakuja kutumia demokrasia mbovu zaidi kupata viongozi wa chama.
Lissu kapita kuwa Makamu mwenyekiti bila hata kunadi sera zake.
Mtu anashindana na kivuli chake angali Chama kina wanachama thousands plus.
Mtu kaongoza chama kwa zaidi ya miaka 15 Sasa harafu huyohuyo anasema hataki watu wakae madarakan kwa miaka mingi.
Mtu anasema chama na wanachama wake Ni matajiri angali Chama hakina hata ofisi zake Wala hakina ofisi zinazoeleweka nchini kote zaidi ya mapango ya nyumba tu.
Mtu anasema Taifa halihitaji ndege harafu yeye na kundi lake wanakodi ndege kwenda kuomba maridhiano na jiwe mwanza.
Watu walioipiga Vijembe serikali ya awamu ya nne chini ya jk kuwa inatumia pesa za serikali hovyo kwa kufanyia Mikutano kwenye Kumbi za kukodi.. Leo hii ndo wamegeuka kuwa wateja wazuri kwenye hizo Kumbi.
Kwakweli kwa uhuni huu Na Unafiki huu CCM itaendelea kubaki madarakani kwa Muda mrefu Sana.
Nilikuwa namuona kijana wangu zitto Kama mtu smart anaeweza Leta revolutions katika upinzani naye siku hizi dishi limeyumba Amekuwa mbwambwajaji na Mnafiki. Mara aite wenzake Washamba Mara Awapongeze Yani hata yeye haelewi msimamo wake Ni upi.
Upinzani wa Tanzania safari bado tunayo Sana tunahitaji maamuzi magumu kufanya mabadiliko siyo huu upuuzi wa kuendelea kumtukuza mtu mmoja kwamba ndo anauwezo wa kuongoza Chama kuliko maelfu ya wanachama waliobaki.
Sent using
Jamii Forums mobile app