Pre GE2025 John Mnyika atiwa msukosuko na Kamati ya Bunge. Nyaraka za mapendekezo yake zakaguliwa kabla ya kuwasilishwa. Baadhi ya nyaraka zimezuiliwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Safari hii tutawabana kisawasawa , nakuhakikishia kwamba hawatopumua , Liwalo na Liwe !
Hamna huo ubavu na hamuwezi kufanya chochote kile. CCM Ndio mungoza njia .hutaki utakwenda tu hata kwa mijeredi labda uhame nchi. Hatuwezi kulea ujingaujinga na kuwabembeleza. Hata kama hamtaki kushiriki uchaguzi basi nyie kaeni pembeni muone kama uchaguzi hautafanyika na mambo kwenda kama kawaida. Maana hata hivyo mshiriki uchaguzi au msishiriki uchaguzi bado CCM itapita na kushinda kwa kishindo kwa kuzoa kula zote za ndio.
 
Tatizo ni Chadema au ni wananchi kusapoti hoja zao? Jambo la msingi ni wewe utuambie umechukua hatua gani
 
10 January 2024
Dodoma, Tanzania

Katibu mkuu CHADEMA kamanda John John Mnyika wa CHADEMA azungumza na waandishi wa habari, baada ya sarakasi za Kamati ya Bunge leo Dodoma


View: https://m.youtube.com/watch?v=6R7J-butAMQ
Katibu mkuu John Mnyika azuiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge la chama kimoja kusoma utangulizi wa mawasilisho wa maoni ya CHADEMA .

CHADEMA imekazia mapendekezo manne na kimeishauri Kamati ya Kudumu ya Bunge ya utawala, sheria na katiba iondoe miswada yote iliyowakilishwa na kusomwa awali mwishoni mwa mwaka 2023 bungeni na serikali.


Katibu mkuu asisitiza tarehe 30 January 2024 amezuiwa kufanya mawasilisho hayo kwa mdomo mbele ya Kamati ya Kudumu.

Hivyo katibu mkuu John John Mnyika wa chama cha siasa cha CHADEMA awataka waandishi wa habari kutumia mawasilisho yake yaliyopo ktk maandishi kuwapa taarifa wananchi na umma mpana bila hofu, maana mawasilisho mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge siyo siri.

Katibu mkuu John John Mnyika awapa shule waandishi wa habari kuelewa hadaa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ambayo inaonesha tayari ina maoni yake mfukoni na zoezi la kuita watu Dodoma linaenda kinyume na 4R za rais Dr. Samia Suluhu Hassan ...

Uthubutu wa kuleta miswada mibovu bungeni na katika Kamati ya Kudumu ya Bunge masuala ya utawala, sheria na katiba haistahili pongezi, kama waandishi wa habari walipohoji kwanini CHADEMA haipongezi kinachoitwa nia njema na uthubutu wa rais.
 
Tatizo ni Chadema au ni wananchi kusapoti hoja zao? Jambo la msingi ni wewe utuambie umechukua hatua gani
Tatizo ni Chadema. Inashangaza unaponiuliza mimi nimechukua hatua gani wakati siyo mwanasiasa. Hata hivyo ningekuwa Kiongozi Chadema ningeweka nguvu zangu kwa wanachama hai kuliko Watanzania wote. Ningejaribu kuelewa kwanini nina wanachama zaidi ya milioni lakini nikiitisha maandamano watu hata elfu kumi hawafiki. Ningejaribu kuwatumia wanachama wangu chini ya miaka 25 kushambulia na kuhujumu CCM hata kama ikibidi kuingiza mamluki ndani ya CCM na vyombo vya dola. Hivyo vitu vichache tu sababu wanaweza kujifunza mengi kupitia harakati za wapigania Uhuru wa nchi za SADC walivyokuwa wanapambana na wakoloni lakini nisingepoteza muda wangu kuendekeza victimhood mentality ndani ya ranks zangu bali ningeweka nguvu kupanda mbegu ya jeuri na imani ya kudai na kuchukua nchi kwa wanachama wangu. Ifike mahali mwananchi akimuona mwanachama wa Chadema bila kusita aamini anataka kuchukua madaraka ya Nchi na siyo tu kusindikiza CCM kwenye siasa. Imani mtakayojenga kwa wanachama wenu itahama kwa wananchi kama upepo.
 
..CCM ndio wamewashindwa Chadema.

..Hawana uwezo wa kushindana nao kwa hoja.

..siasa ni hoja vs hoja. Na CCM uwezo hawana.
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa Msuya alishasema kuwa CHADEMA ni Wajenzi wazuri wa hoja kuliko CCM!
 
Kwaiyo wewe unataka waitishe maandamano?
 
Nilisema hapa jana kuwa ccm/serekali wana nongwa na cdm, na kitendo Cha cdm kwenda kwa wingi kuto maoni yao kutasababisha maoni yote kutofanyiwa kazi. Shida ya serekali ya ccm ni uwepo wa cdm, hiki chama kinaitesa sana ccm.
 
Unashindwa nini kuwa mwanasiasa? Umeona wenzio wameshindwa chukua hatua, uache kucheua hapa.
 
10 January 2024
Dodoma, Tanzania

Dr. Joseph Kizito Mhagama -
Jumla ya washiriki 1,707 wamejiandikisha kwenye ushiriki wa utoaji maoni



View: https://m.youtube.com/watch?v=jzaIBOli9P4
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mh. Dr. Joseph Mhagama (Mbunge CCM) amesema jumla ya washiriki 1,707 wamejiandikisha kwenye ushiriki wa utoaji maoni.

Pia, taasisi za kidini, mashirika manne, vyama vya siasa 18, taasisi na asasi za kiraia 31 zimeshiriki huku wachangiaji binafsi 68 wakitoa maoni yao.

Mh. Dr. Joseph Kizito Mhagama amesema hayo leo Jumatano, Januari 10, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha utoaji wa maoni uliodumu kwa siku nne.

Baada ya hapo, kamati hiyo .....
 
BUNGE LA CHAMA KIMOJA LA KARIPIWA, KWA KUWA NA MAONI YA CCM MFUKONI

Katibu mkuu wa CHADEMA kamanda John Mnyika leo katika viunga vya bunge mjini Dodoma

 
Kikosi Kipana cha Chadema kilichotikisa Kamati ya Bunge na kumchanganya Bwana Joseph Mhangama kiasi cha kuwewesekana na kusababisha Polisi kuongezwa Dodoma leo kwa ajili ya Doria .

 
10 January 2024
Kilombero, Morogoro
Tanzania

ALIYEKUWA MJUMBE KAMATI YA CCM ATOBOA SIRI MBELE YA CHADEMA / ARUDISHA KADI YA UANACHAMA WA CCM


View: https://m.youtube.com/watch?v=p72keZ6L7-U

Mzee wa kata ya Mwaya akubali yeye na wananchi wameguswa sana na sera za CHADEMA hivyo wanajiunga na chama kikuu cha upinzani Tanzania

Mzee ajuta sana yale aliyokuwa anafanya akiwa ndani ya chama dola kongwe CCM ..kwamba alishiriki kuharibu maisha ya wananchi kwa kupitia mbinu 72 na kuzitaja mbinu kadhaa kupigilia msumari wa mwisho 2024 katika sanduku la kisiasa la CCM linaloenda kuchimbiwa futi sita kuwa ni ....
 
Ipo stage mkuu hatujafika ila upewe uhai hata kuuana kitu kidogo.leo wanazikwa watoto wa chadema kwa sababu ya sheria mbovu za uchaguzi zinazopelekea chaguzi za fujo.iko siku watoto wa vion gozi wa ccm watazika pia watoto wao.tukimaliza kuzika wote.tutapoongelea uchaguzi huru watakuwa wanaelewa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…