Pre GE2025 John Mnyika atiwa msukosuko na Kamati ya Bunge. Nyaraka za mapendekezo yake zakaguliwa kabla ya kuwasilishwa. Baadhi ya nyaraka zimezuiliwa!

Pre GE2025 John Mnyika atiwa msukosuko na Kamati ya Bunge. Nyaraka za mapendekezo yake zakaguliwa kabla ya kuwasilishwa. Baadhi ya nyaraka zimezuiliwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chadema inahitaji viongozi wanaoweza kushawishi wananchi kuingia barabarani kudai katiba na sheria nzuri za uchaguzi.
Kama wananchi hawajapata sababu ya kupinga yasiyofaa, hakuna atakaweza kuwaamsha. Ila wajibu sio wa chama cha siasa tu, ni wangu na wako pia.
 
Haufiki bila Chadema kuwa wakali. Tupo mahali TEC na viongozi wa Kilutheli wanakuwa tishio kwa CCM kuliko Chadema. Siyo sawa.
Acha tabia ya kulaumu CHADEMA kwa mambo ambayo na wewe una nafasi ya kucheza nafasi yako..!

Mfano, unawataka CHADEMA kuwa wakali. Mimi nasema, na wewe uwe mkali pia..

Na wewe ufanye utaratibu wa kuongoza maandamano ktk eneo lako kutaka mabadiliko (reforms) za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutawala..

Usiitegemee CHADEMA tu kukuletea mabadiliko unayoyataka. Kila mtu ana wajibu wa kucheza nafasi yake ktk kuleta mabadiliko ktk jamii na nchi hii..!!
 
Kama wananchi hawajapata sababu ya kupinga yasiyofaa, hakuna atakaweza kuwaamsha. Ila wajibu sio wa chama cha siasa tu, ni wangu na wako pia.
Sawa tuweke wananchi pembeni. Je wanachama hai wa Chadema?
 
Viongozi wa Chadema mngeachia ngazi. Ni wazi CCM wanawadharau na hamna cha kuwafanya sababu hamna hata nguvu ya kuitisha maandamano . Hatuwezi kuwa na chama kikuu cha upinzani sifa yake kuu nikulalamika na kuonewa bila kurudisha mapigo kwa mtesi wake.
Kwan ninan umemuajiri awe mpinzani Chief. Unaweza wewe kufanya kile unachohic chadema au ACT wameshindwa Mzee.
 
Video ndefu kabisa / Uncut / unedited video clip. Live Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge alivyokuwa anaingilia uwasilishaji wa maoni

HALI ILIVYOKUWA MBELE YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE, KAMANDA MNYIKA AKITOA WASILISHO LA MAONI YA CHADEMA

View: https://m.youtube.com/watch?v=bKf7xpsl0VI

Huyu Mwenyekiti wa hii kamati ya bunge ni nani maana mpiga picha hata hakuwa anamwonesha sura yake?

By the way, mimi hata sijaona sababu ya Mwenyekiti huyu kumkatiza katiza (interrupt) mara kwa mara John Mnyika kutoa maoni ya chama chake..

Kwa sababu kila mtu anaelewa kuwa, maoni ni maoni tu. Mtu au kamati hailazimishwi kuyakubali au kuyakataa...

Kwa kuwa ni maoni tu, hata pale mchangiaji anapokuwa irrelevant, hiyo huwa ni kwa hasara ya mchangiaji mwenyewe kuutumia muda wake vibaya kwa hasara yake..

Labda ktk hili, wanajua kuwa wataonwa ni wajinga na wapumbavu kukataa mambo ambayo ni dhahiri shairi..

Lakini pia katika scenario hii, CHADEMA wakiwakilishwa na Katibu Mkuu wao ndugu John John Mnyika, wana hoja nzito ambazo hawa CCM hawataki zisikike kwa umma. Hii ndiyo sababu ya mahangaiko yote ya Mwenyekiti huyu kumzuia Mnyika asiseme yapaswayo kusema..!!

All in all, nimempenda bure John Mnyika kwani pamoja na dhamira mbaya ya Mwenyekiti wa kamati hii na wajumbe wake baadhi waliojipanga kum - frustrate ili ashindwe kuwasilisha vyema, bado Mnyika alikuwa very calm na akafanikiwa kuwasilisha hoja zake japo si zote...
 
..Hicho ndicho alichokutana nacho Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika alipokwenda Bungeni kuwasilisha mapendekezo ya chama chake.

..Msikilize hapa chini akieleza kilichomtokea alipofika Bungeni.

View: https://www.youtube.com/watch?v=A7tp2deYb-w

Nchi hizi imeishakuwa ya ya uchakachuaji. Fikiria tuna rais ambaye anajua kuwa hukuchaguliwa na wananchi, tuna wabunge waliopitishwa na mwendawazimu mmoja, hivyo hata yanayotokea Zanzibar kwenye kombe la mapinduzi ni.matikeinya kubwa na jamii ya watu wanoamini na kusimamia uongo na uchakachuaji
 
Kwan ninan umemuajiri awe mpinzani Chief. Unaweza wewe kufanya kile unachohic chadema au ACT wameshindwa Mzee.
Swali lako linaonesha huelewi concept nzima ya vyama vya siasa na demokrasia. Asante kwa kuchangia kwenye post yangu.
 
Acha tabia ya kulaumu CHADEMA kwa mambo ambayo na wewe una nafasi ya kucheza nafasi yako..!

Mfano, unawataka CHADEMA kuwa wakali. Mimi nasema, na wewe uwe mkali pia..

Na wewe ufanye utaratibu wa kuongoza maandamano ktk eneo lako kutaka mabadiliko (reforms) za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutawala..

Usiitegemee CHADEMA tu kukuletea mabadiliko unayoyataka. Kila mtu ana wajibu wa kucheza nafasi yake ktk kuleta mabadiliko ktk jamii na nchi hii..!!
Ni wazo zuri lakini halina mashiko. Sheria zilizopo na wanazojitahidi kuzirekebisha wanataka mabadiliko ya uongozi yafanyikie kupitia vyama vya siasa hawataki hata wagombea binafsi. Sioni haja ya mimi kufanya hiyo kazi wakati kuna nafasi ya kutumi platform ya Chadema kufanya hivyo na inawezakana kama viongozi wa Chadema wakiwachia wengine wenye udhubutu na ari kupambana na CCM. Mtajitahidi kubadilisha hoja lakini viongozi wa Chadema lazima waanze kuulizwa na kujihoji wanakosea wapi hadi inafika CCM hawaogopi uwepo wao wala hawaoni kama wanaweza kuchukua madaraka ya Nchi.
 
Swali lako linaonesha huelewi concept nzima ya vyama vya siasa na demokrasia. Asante kwa kuchangia kwenye post yangu.
Bro mtu akikaa mbele yako kama kiongoz wako nguvu zake ni wewe so kabla hujamlaumu kwa lolote mtu wa kwanza wa kujilaumu ni wewe. Je umefanya mangap ili kufikia hicho unachotaka kifanyike. Wewe kiongoz wa upinzan mkuu anawekwa ndani miez 8 mmekaa kimya unategemea nini. Hili ni tatizo la wananchi sio upinzan. Hapo kenya watu wenyewe ndio wapinzan wa matendo kinzan ya serIkali. Akina raila wanaelekeza tu nini kifanyike watu wanafuata coz wanajua hawana mjomba wa kumlilia. Sasa wewe mwanaume mzima uko nyuma ya laptop unawalaumu watu kwa madhaifu yako shame.
 
Haufiki bila Chadema kuwa wakali. Tupo mahali TEC na viongozi wa Kilutheli wanakuwa tishio kwa CCM kuliko Chadema. Siyo sawa.

1. Badala ya kuweka jina la chama pale ungeweka vyama vya upinzani.

2. Vinginevyo Kuna vi misemo vya mgema akisifiwa, na maskini akipata ... ambavyo vina ukakasi.

3. UKAWA ilitikisa; Kenya wanatembea kwa coalitions; sisi tuna ka kulogwa sugu.

Proved; ila imhotep akawaambie na wenzake.
 
..Hicho ndicho alichokutana nacho Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika alipokwenda Bungeni kuwasilisha mapendekezo ya chama chake.

..Msikilize hapa chini akieleza kilichomtokea alipofika Bungeni.

View: https://www.youtube.com/watch?v=A7tp2deYb-w

Sasa watu wa Serikali wanapata shida gani Kwa sababu Chadema wanaleta maoni ,Sasa maoni si unayaookea na kuyasikiliza harafu Uamzi unabakia ni WA kamati ku damp au kuchukua shida Iko wapi?
 
Back
Top Bottom