Upo hapa unalaumu wananchi hawaingia barabarani wakati watu wanaojiita wanasiasa wa upinzani wanashindwa kuratibu wanachama wao hai waliowasajili kidijitali kuingia barabarani. Watu wasio smart na strategic kama nyie mnasubiri chuki za wananchi zifanye kazi zenu wanasiasa. Sikiliza, kwa hoja na mtazamo wako hata Samia anaweza kulalamikia vijana wa hovyo wa Nchi hii kwa kutoleta maendeleo. Si wapo Serikali kuu na kwenye halmashauri, si ni sehemu ya decision making ya Nchi kwanini wanashindwa kuleta maendeleo? Huwezi kutulalamikia sisi wananchi wakati mfumo uliopo kwasasa kazi ya kumuulika na kuwajibisha Chama tawala wamekabidhiwa vyama vya upinzani kama mnataka tufanye sisi wananchi basi tufute hivi vyama vya siasa.