Kwa mazingira yaliyopo Chadema haiwezi kupata viti maalum hata mmoja, kwasababu hawajakidhi viwango vinavyotakiwa, wana mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa jimboni, hii ni sawa na Zitto alivyokuwa anawakilisha chama chake bungeni, alikuwa peke yake, hakuwa na viti maalum hata mmoja wa chama chake.
Hivyo, kutokana na mazingira hayo, Chadema kupata viti maalum haiwezekani kisheria, na kama watapata basi lazima itakuwa ni kwa makubaliano maalum na CCM, hao watakaoteuliwa kwenye hizo nafasi wajiandae kujibu maswali.
Idadi ya kura za urais ni kwaajili ya ruzuku pekee.