1. Katibu Mkuu ambaye ndiye mwenye dhamana ya kupeleka majina ya wabunge viti maalum kwa tume ya uchaguzi hajawahi kupeleka majina hayo.
2. Wabunge walioelekea bungeni kuapishwa hawana baraka za chama...
Kwa kweli mii bado niko neutral katika hili la wabunge wa viti maalumu.
Sijapata ushahidi concrete wa kunithibitishia kuwa wana baraka za chama au la. Nitaweza kutoa msimamo wangu binafsi katika hili nitakapokuwa na ukweli halisia.
Ila kwa watanzaninia niseme hivi,
Hawajawa tayari kufanya mageuzi yaani wanaupenda utumwa wao ama kwa kujua au kutokujua kuliko wengi tunavyofikiri.
Kipindi Mrema akiwa mpinzani kweli alijashtuka kuwa anawapigania watu ambao hawajitambui na hata hawajui kutofautisha kati ya haki na batili.
Kwa jinsi hii Mrema aliamua kupiga about turn na kufanya siasa za kinafiki kwa maana ya ku survive binafsi yeye na familia yake.
Wengi tunaweza kumdhihaki lakini kimantiki hatuna uhalali huo baada ya kuwa sisi ni jamii isiyojitambua kabisa kwamba tunataka nini na kwa wakati gani na ni kwa jinsi gani ya kukichukua, ukilinfanisha na mataifa yote yaliyotuzunguka.
Sasa ukija kwa Chedema watu wamejitoa muhanga kuwapifania wananchi kupewa haki yao ya uhuru kamilikatika nyanja zote kwa kuhatarisha maisha yao. Baadhi wamenyang'anywa mali zao na hata kuharibiwa kwa mashamba yao ya mboga, wengine wameuawa bila hata nzi kukamatwa wala kutuhumiwa kuhusika na kifo chao, wengine wamemiminiwa risasi mchana kweupe bila hao wahuni kujulikana, wengine wana zaidi ya kesi tano za kubambikwa mahakamani.
Juzi katika kampeni viongozi walijitoa na kuhatarisha uhai wao maana waliachwa na vyombo vya ulinzi kama swala wasio na kinga, wakuu wa wilaya wamewafuata hadi majumbani na bunduki, wakuu wa polisi walijiapiza hadharani kuwa hawatawaruhusu washinde.
Kibaya zaidi atendo haya yote ya kihalifu bila kufuata utaratibu raia waliyaacha yapite hivi hivi bila kuchukua hatua yoyote hata maandaamano ya amani kuonyesha/ kuashiria kukataa huu uhuni yaliyoitishwa na hao waliokuwa wakiwapigania.
Huu uhalali wa kuwashutumu baada labda ya wao kugundua wanaopiganiwa hawapo tayari mnaupata wapi na kwa kigezo gani?
Katika biblia kulikuwa na maachilio ya watumwa kuachwa huru warudi makwao yaani mwaka wa 49 na hamsini ndio maachilio.
Lakini mtumwa ambae aliona gana haja ya kuachwa na bwana wake ili awe huru, alitakiwa na sheria apelekwe kwa kuhani hekaluni na halafu kisha atobolewe sikio lake kama ishara ya kumfanta mtumwa milele.
Ndivyo ilivyo kwa watanzania. Kwa matendo yao katika utawala wa kiimla wamechagua kwa watumwa.
Kuwapigania ni sawa na kuupaka upepo rangi.