Uchaguzi 2020 John Mnyika: Hatujateua majina ya wabunge Viti Maalum. Tunafuatilia Ofisi ya Spika na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua

Uchaguzi 2020 John Mnyika: Hatujateua majina ya wabunge Viti Maalum. Tunafuatilia Ofisi ya Spika na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua

Niliacha ushabiki wa hivi vyama siku kina Mbowe, Lissu, Lema na Mchungaji Msigwa walipomsafisha Lowassa.

Tunasubiri ACT nao kule Zanzibar waunge juhudi.

Africa bado tuko kwenye level ya kuhangaikia zile issue tatu alizozitaja Nyerere: Chakula (njaa), magonjwa na elimu.

Mpaka tumalize haya ndipo tunaweza kufanya siasa safi na zenye malengo sahihi.
 
Hivi ni yule ambaye tuliambiwa na Kangi kuwa siku zake zinahesabika ni muda mchache tu asingesikika tena na kweli ikafika kipindi akapotea mpaka ikasemekana ameshadhibitiwa!, alirudirudije?

Shikamoo Kigogo
 
Cinema tu za CDM kuondoa aibu mbele ya jamii wakiamini yatapita tu, lakini Mnyika na viongozi wengine wote isipokuwa Lissu watakuwa wanajua sana kilichotokea.

Pole kwa Lissu the message is clear akufukuzae akwambii toka anakufanyia visa tu.
 
Chadema kususia bunge au kutotambua matokeo ya uchaguzi walioushiriki ni

1. Kuwadharau raia wa Tanzania 1.8m walio amka mapema Nov 28, 2020 kuwapigia kura. Kama ambavyo Lissu na Kabwe wamefanya. Kwa upande wa ACT ambayo siitofautishi na Maalim Seif ni kama Maalim hajataka kujifunza makosa aliyoyafanya 2015 kususia uchaguzi ambapo kwa hesabu za haraka kosa hilo limegharimu kwa kupata asilimia 19 ya kura visiwani tofauti na miaka iliyopita.

2. Kususia Bunge kwa CDM kungeikosesha sauti bungeni na ndio ungekuwa mwisho wake kama wangebaki kushikilia mawazo ya Lissu ambayo kisiasa yanakiua chama. Pia Chadema wangepoteza haki yao ya gawio la ruzuku kutoka Bungeni kwa miaka mitano mfululizo. Hii ingeathiri sana shughuli za chama nchi nzima na pia viongozi wa chama kukosa nguvu ya kimaamuzi hasa Mbowe. ( Huu ni mradi wake huo ndio ukweli) amewekeza sana so kufuata mawazo ya kina Lissu kungeiua biashara yake ambayo kwa namna yoyote Mbowe hawezi kuiacha (akakimbilia ughaibuni) ... Wakati Lissa anamahali pa kushikilia hana uchungu na uwekezaji wa Mbowe and Co. Na ndio sababu Mbowe alikuwa kimya anatafakari atoke vipi mtegoni.

Lissu alikitumia Chadema kumchafua Magufuli kwa kutumia tiketi ya urais (kwa ufadhili wa ulaya ....sina ushahidi ila natumia common sense) ambao kwa hakika alijua haupati ....ili adhima yake ya kuichafua serikali itimie rejea kampeni zake hakukuwa na kuzungumzia sera zaidi ya matusi kwa rais ya serikali yake... Na kwa kuthibitisha ufadhili wake ulitoka wapi umoja wa ulaya kupitia ubalozi wa Ujerumani ulimpa kinga ya kidiplomsia aweze kukimbia nchi.

3. Namshauri Maalim na Zitto kuepa Lissu's trap wakubali kushiriki serikali ya umoja wa kitaifa kule Zanzibar ili wasifutike kisiasa na ikiwezekana waipiku CDM ili wao wawe leading opposition party. Siasa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine uki fail mbinu ya huku unahamia plan B kung'ang'ania mawazo ya Lissu, Fatma Karume na Lema ni kujimaliza. Kabudi alijua nini anachoongea na hakuna cha Sanction wala mdogo wake toka ulaya maana nguvu hiyo imemalizwa na CDM kukubali kurudi Bungeni.

Hongera Mbowe na Kongole viti maalum kwa kukwepa mtego wa Lissu.
 
Hana analoweza kufanya Njaa imewazidi nguvu... kama Halima ameshindwa yeye nani?
Watafukuzwa uanachama ili kukijengea chama uaminifu kwa wananchi. Vinginevyo tofauti na hili CHADEMA ndo kimekufa rasmi.
 
Akihojiwa na shirika la utangazaji la BBC

Mnyika anasema kwa mujibu wa taratibu na sheria mwenye mamlaka ya kureuwa majina ni baraza kuu la chama na katibu wa xhama ndie mwenye mamlaka ya kuandika barua kwa tume kuwasilisha majina ya wabunge wa viti maalum.

Yanayoendelea Dodoma inabidi tume na spika waseme hayo majina wamepelekewa nan nani toka CHADEMA
 
Jameni acheni utani,millioni 200 ya mafao bila bla blah kila baada ya miaka mitano ni raha nye!
 
Atasubiri waseme na hapo wametegwa wakiwafuta uanachama wataonekana wanaonea jinsia ya kike wao watulie tu
 
Naona chama wakbidhiwe Bawacha maana wanajielewa kuliko katibu mkuu wao
 
Akihojiwa na shirika la utangazaji la BBC

Mnyika anasema kwa mujibu wa taratibu na sheria mwenye mamlaka ya kureuwa majina ni baraza kuu la chama na katibu wa xhama ndie mwenye mamlaka ya kuandika barua kwa tume kuwasilisha majina ya wabunge wa viti maalum.

Yanayoendelea Dodoma inabidi tume na spika waseme hayo majina wamepelekewa nan nani toka CHADEMA
Duh hii kali sana....
 

Wafukuzeni basi mbona akina Silinde&Co mliwatimua kwenye mazingira hayahaya.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
"Nikishukuru chama changu cha Chadema kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe ambao kupitia wao sisi tumepata nafasi ya kukiwakilisha chama chetu, viti hivi siyo hisani ila ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata"- Halima Mdee

Hiyo ni kauli ya Mdee
Mnyika na Lisu inawezekana bado ni wageni ndani ya chama
CCM ni hatari,Trump aje kupata shule haaa haaa
 
Kamanda tupe mrejesho
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema, chama hicho hakijateua majina ya wabunge wa viti maalum “ niliandika barua NEC kuwajulisha. Tunafuatilia yanayojiri Ofisi ya Spika wa Bunge na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua.”

---UPDATE---
Akihojiwa na shirika la utangazaji la BBC

Mnyika anasema kwa mujibu wa taratibu na sheria mwenye mamlaka ya kuteua majina ni baraza kuu la chama na katibu wa chama ndiye mwenye mamlaka ya kuandika barua kwa tume kuwasilisha majina ya wabunge wa viti maalum.

Yanayoendelea Dodoma inabidi tume na spika waseme hayo majina wamepelekewa nan nani toka CHADEMA




Halima Madee na Ester Bulaya kujifanya makamanda kumbe makamanda njaa tu. Hongera CHADEMA kwa msimamo usioyumba. Kesho Kamati Kuu ikae kufukuza wote hao.
 
Back
Top Bottom