Uchaguzi 2020 John Mnyika: Hatujateua majina ya wabunge Viti Maalum. Tunafuatilia Ofisi ya Spika na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua

Uchaguzi 2020 John Mnyika: Hatujateua majina ya wabunge Viti Maalum. Tunafuatilia Ofisi ya Spika na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua

Hakuna kitu hapo huyo Mnyika anadanganya watu tu. Hakuna anayrapishwa bila barua.
 
Wanacheza na akili zenu tu.

Ngoma ishaisha hiyo,

Kama mnasubiri jingine endeleeni kusubiri.
 
Exactly wafukuzwe wote hao ibaki cream tupu . Kulinda legacy ya chama , ingawa Ndugai atawalinda kwa maagizo ya Mhutu , ili wapate wajumbe na wenyeviti wa PAC na LAAC , si unamjua Mhutu kwa hela , atawalinda lakini tulishawstimua na wafadhili watapata taarifa na wanafuatilia hivyo Jiwe hatopata hizo hela anazozitaka .
 
1. Katibu Mkuu ambaye ndiye mwenye dhamana ya kupeleka majina ya wabunge viti maalum kwa tume ya uchaguzi hajawahi kupeleka majina hayo.

2. Wabunge walioelekea bungeni kuapishwa hawana baraka za chama.

3. Tume ya uchaguzi haina uhalali wa kisheria kupeleka majina hayo kwa spika.

4. Spika Hana uhalali wa kisheria wa kuwapisha wabunge wa chadema kwa sababu hawajafuata sheria zilizotungwa na Bunge.

5. CHadema hata wasipowafuta uanachama Hawa tayari siyo wabunge wa chadema kwa sababu hawana baraka za chama Kama taratibu zinavyosema, hivyo wanaingia kwenye kundi la wabunge wa chama tawala maana chama kinautaratibu ambao umetokana na sheria za Bunge.

6. Endapo Chadema watawafuta uanachama bado bunge na tume itawakingia kifua kama walivyofanya kwa yule Mbunge wa Mtwara last time ambaye aliitwa na spika akaambiwa ni Mbunge.

7. Endapo Chadema itaenda mahakaman kufungua kesi, kesi watashinda lakini maamuzi ya mahakama hayatafanyiwa kazi kwa sababu bunge limejijengea msingi wa kuwa muhimili usioingiliwa.

8. Pamoja na Chadema watatekeleza wajibu wao Kama formality kwa kuwaondoa uanachama ili waruhusu kupata viongozi wapya watakaoendelea pale wenzao walipoishia.

9. Move hii inavyochezwa inalengo lakutengeneza CCM B ndani ya CCM ambapo watu Chadema wana mkakati wa muda mrefu wakuandaa vijana watakaopata ajira ndani ya serikali na ndani ya CCM kwa kuzingatia uwezo wa vijana hao kujenga hoja.

10. CHadema wanaelekea kukamilisha kazi yao ndani ya ccm, nguvu kubwa inayohitajika nikuimarisha mizizi kwenye dola ili lengo la TANZANIA HURU LIWEZE KUTIMIA.

11. Uhuru ni mchakato mkubwa, mpasuko wa ccm wa miaka ishirini mbele ulianza mwaka 1984, tuendelee kuvumilia na kuandaa watoto wetu kuja kuturejeshea Tanzania yetu.
 
Ndiyo maana nilishajiamlia kuwa sitakaa ninaamini mwanasiasa wala kuwa mwanachama wa chama cha upinzani hata siku moja. Upinzani ni njaa na mbwembwe tu. Nimebaki kuwa Mashabiki tu na mpiga kura huru. Ngoja nichukue ka wine kangu ninywe.
 
Chadema niwashauri mlichukulie hili swala kwa umakini mkubwa mno. Hapo busara itumike. Wamelengwa wabunge vichwa na mkiviachia tu mtayumba kuliko meli iliyogonga edge of a cliff. Ni mpango mkubwa umesuka kuwaua jumla. Take my words as an independent observer.
 
Yani wamejizalilisha Sana very shame kuumia kisa nafasi za wanawake Hawa watu wabinafsi na wachumia tumbo, wao si waligombea waende bungeni sasa kushindwa kwao ndio wanawake eti wasiende, very shame
Mi ndiyo maana niliacha kushabikia hiki chama
Hakina tofauti na CCM
 
Mtashangaa pale mtakapo oneshwa barua ya uteuzi wa majina ya "vitu maalum" ikiwa na hati zote halali. Hii Tanzania watu wanaweza fanya yao mkabaki midomo wazi. Huu ujasiri wa kwenda kuapishwa bila Baraka za Chama, (kama ni kweli hazipo), wanautoa wapi?

Tusubiri tuone
Sidhani kama barua rasmi ipo; ingekuwepo ingekuwa kitu cha kwanza kuzumgumziwa. Aidha barua ingeluwepo, hata kama ya kugushi hili suala lingeanzia NEC kwani ndicho chombo chenye dhamana ya kutangaza majina ya wabunge waliopatikana. Lakini inavyoelekea mambo yamaanzia bumgeni. Watu wamejipeleka wenyewe kwa Spika wakalishwa kiapo. Maadam limeanzia kwa Spika maana yake ni ule ule mkakati uliompokonya Lissu ubunge na kumrejesha Mwambe bungeni! Lengo ni kuwa na watu wanaoitwa ni wapinzani bila kujali wamepatikanaje. The end justifies the means!
 
Naunga mkono hoja ,wafukuzwe kabisa ,Mdee amekaa bungeni miaka 15 lakini bado anaogopa kukaa kitaani ,yaani miaka yote 15 hakujipanga? Sasa kama ameweza Kujenga HEKALU lile Mbweni Mpiji ameshindwa kuwa na mtaji wa biashara wa kuweza kumuendeshea maisha kipindi cha miaka mi5 mpaka aendekeze NJAA?
 
Mi ndiyo maana niliacha kushabikia hiki chama
Hakina tofauti na CCM
Dah kwa issue ka hii ndio wamenichosha kabisa maswala ya wanawake ni sensitive wao wanaleta mitazamo yao kandamizi. Inabidi kuwa na upinzani wenye watu waelewa, viti hvo viko kikatiba na kwa bunge hili la kijani ilikuwa na umuhimu kuwa na mawazo mubadala Sasa wao wanaleta blah blah
 
C`mon this is bullying kwanini CCM wanatumia mbinu mfu zile zile kila siku kwa hio hao ccm ndio wanawajua sana wabunge wanaofaa kutoka chadema sio kama wao walivyojipatia ushindi bila kuchaguliwa?
 
Naunga mkono hoja ,wafukuzwe kabisa ,Mdee amekaa bungeni miaka 15 lakini bado anaogopa kukaa kitaani ,yaani miaka yote 15 hakujipanga? Sasa kama ameweza Kujenga HEKALU lile Mbweni Mpiji ameshindwa kuwa na mtaji wa biashara wa kuweza kumuendeshea maisha kipindi cha miaka mi5 mpaka aendekeze NJAA?
Biashara mchezoii?

Mtu hajawahi kufanya biashara hata ya kuuzA kuku.

Biashara tuachie wenyewe wewe.

Sio kila Mtu anaweza
 
Ni wazi kuna rafu imechezwa kwa kushirikiana na Ndugai!Sasa ili iwe fundisho napendekeza wafutwe uanachama na KM apeleke majina mengine ambayo yamo kwenye orodha ya wagombea viti maalumu!
Anayapeleka kwa nani? Hawawezi kua wabunge bila kuapishwa na Ndugai.
 
Back
Top Bottom