1. Katibu Mkuu ambaye ndiye mwenye dhamana ya kupeleka majina ya wabunge viti maalum kwa tume ya uchaguzi hajawahi kupeleka majina hayo.
2. Wabunge walioelekea bungeni kuapishwa hawana baraka za chama.
3. Tume ya uchaguzi haina uhalali wa kisheria kupeleka majina hayo kwa spika.
4. Spika Hana uhalali wa kisheria wa kuwapisha wabunge wa chadema kwa sababu hawajafuata sheria zilizotungwa na Bunge.
5. CHadema hata wasipowafuta uanachama Hawa tayari siyo wabunge wa chadema kwa sababu hawana baraka za chama Kama taratibu zinavyosema, hivyo wanaingia kwenye kundi la wabunge wa chama tawala maana chama kinautaratibu ambao umetokana na sheria za Bunge.
6. Endapo Chadema watawafuta uanachama bado bunge na tume itawakingia kifua kama walivyofanya kwa yule Mbunge wa Mtwara last time ambaye aliitwa na spika akaambiwa ni Mbunge.
7. Endapo Chadema itaenda mahakaman kufungua kesi, kesi watashinda lakini maamuzi ya mahakama hayatafanyiwa kazi kwa sababu bunge limejijengea msingi wa kuwa muhimili usioingiliwa.
8. Pamoja na Chadema watatekeleza wajibu wao Kama formality kwa kuwaondoa uanachama ili waruhusu kupata viongozi wapya watakaoendelea pale wenzao walipoishia.
9. Move hii inavyochezwa inalengo lakutengeneza CCM B ndani ya CCM ambapo watu Chadema wana mkakati wa muda mrefu wakuandaa vijana watakaopata ajira ndani ya serikali na ndani ya CCM kwa kuzingatia uwezo wa vijana hao kujenga hoja.
10. CHadema wanaelekea kukamilisha kazi yao ndani ya ccm, nguvu kubwa inayohitajika nikuimarisha mizizi kwenye dola ili lengo la TANZANIA HURU LIWEZE KUTIMIA.
11. Uhuru ni mchakato mkubwa, mpasuko wa ccm wa miaka ishirini mbele ulianza mwaka 1984, tuendelee kuvumilia na kuandaa watoto wetu kuja kuturejeshea Tanzania yetu.