John Mnyika: Kiongozi wa CHADEMA Mzee Ali Mohamed Kibao, adaiwa kushushwa kwenye Basi na kuchukuliwa na watu wasiyojulikana

Kwanini unapotosha taarifa aliyotoa mnyika? Yeye kaandika amechukuliwa wewe unaandika ametekwa

Hapo mwisho ameomba mwenye taarifa amjulishe kwakua unajua ametekwa nenda kampe taarifa
Vipi mkuu, alichukuliwa au alitekwa?
 
Nikikumbuka mbwembwe za Chadema walivyo mpokea Samia wakati anaingia madarakani na kumpa tuzo juu;nachoka mimi!
Mkuu kuna kanuni ipo hivi, mtu akifanya vizuri mpongeze na akifanya vibaya mkosoe.

Utakua mtu wa aina gani kuponda kila kitu kiwe chema au kibaya wewe ni kuponda tu?
 
Mkuu umeongea vitu vya msingi sana. Hata paka ukimtaitisha sana na akakosa pakutokea basi kazi unavyo.

Ndio ilivyo sasa watu wanaumiza vichwa wanaepukana na hawa watekaji. Sio rahisi kuwazuia watu kukosoa, ndio nature ya binadamu na kuna baadhi yetu wanamkosoa hadi Mungu na bado Mungu hawanyang'anyi pumzi, wanadunda tu.

Kama Mwenyezi Mungu tunayemuimba kwenye wimbo wa Taifa anavumilia kukosolea wao wanajiona kina nani?

Ubaya wa haya mambo ukiongea unakufa na usipoongea pia unakufa. Vingenevyo tukumbushane aliongea nini Akwilina?
 
Hata Magufuli kabla hajafa alijua atakuwa Rais Milele, ndio maana alilazimisha viongozi wa ngazi zote kununua viwanja Chato

Sikushangai wewe mtu duni kujidanganya kama hivyo
Watazania ifike mahali tuseme imetosha. Mimi siki hao majabazi wanajiita polisi au usalama wakiji kunikamata sitakubali kwenda nao popote watamaliza kazi yao hapo walipo nikuta, baada ya mimi kufanya kila niwezalo kujiokowa.
 
Suala la kifo cha mzee Ali binafsi sioni kama linafanana na matukio mengine ya kutekwa .

Hawa watu ni either Wana Usalama wenzake au Wana CHADEMA .Kwa hali ilivyo Mzee wale watu angekuwa hawajui asingekubali kushuka kirahisi na kuongozana nao , na kuna uwezekano mkubwa wale watu anawajua .

Je hawa watu ni kina nani ?
 
muda utaongea hata mimi nawaza ivyo ivyo
 
Sielewi na ndiyo maana nimekuwa kimya. Wapo wanaojua na wataongea katika mfumo rasmi. Acha ujuaji na roporopo. Be warned!
acha kutisha watu,wao wanavyoo tuhumu jeshi wanaushahidi, na sisi pia kwa jicho la tatu tunaona kua wanaumizana wenyewe kwa wenyewe
 
Mtu amejitambulisha kwako ni polisi wanakuhitaji unawezaje kupinga arrest?.

Kama kweli Serikali iko serious, itoe tangazo public kupitia Rais na Waziri wa mambo ya ndani, marufuku kumuarrest mtu bila kuwepo mjumbe au mwanasheria wa mhusika, au hata waambatane na ndugu wa mhusika mpaka kituo cha karibu cha polisi maelezo rasmi yatolewa ndugu/mwanasheria/mjumbe wote wajue.
 
Kwahiyo awakubalie watu wa CHADEMA wampige pingu?

WTF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…