John Mnyika: Kiongozi wa CHADEMA Mzee Ali Mohamed Kibao, adaiwa kushushwa kwenye Basi na kuchukuliwa na watu wasiyojulikana

John Mnyika: Kiongozi wa CHADEMA Mzee Ali Mohamed Kibao, adaiwa kushushwa kwenye Basi na kuchukuliwa na watu wasiyojulikana

Kwanini unapotosha taarifa aliyotoa mnyika? Yeye kaandika amechukuliwa wewe unaandika ametekwa

Hapo mwisho ameomba mwenye taarifa amjulishe kwakua unajua ametekwa nenda kampe taarifa
Vipi mkuu, alichukuliwa au alitekwa?
 
Nikikumbuka mbwembwe za Chadema walivyo mpokea Samia wakati anaingia madarakani na kumpa tuzo juu;nachoka mimi!
Mkuu kuna kanuni ipo hivi, mtu akifanya vizuri mpongeze na akifanya vibaya mkosoe.

Utakua mtu wa aina gani kuponda kila kitu kiwe chema au kibaya wewe ni kuponda tu?
 
Vyombo vya usalama viwe makini kidogo na haya mambo, kama kweli kuna utekaji unaohusiana na siasa na tunaufumbia macho kwa sababu labda unatufavor basi tujue tunaeleke kaburini taratibu.

Tutambue mambo ya usalama yanahitaji umakini na busara kubwa sana na sio siasa maana dunia ya leo ina mengi sana tunayoyafahamu na tusiyoyafahamu na yote huwa yanabackfire tukijichanganya.

Hii michezo ikiendelea tutambue hakuna anayekubali uonevu kila siku, Bali tutawajengea watu usugu na kuwafanya waanze kutafuta namna ya kujilinda na hata bargain style itakayofanya wateke ili mbadirishane mateka, lakini pia tutambue huko mitaani hawa watu huishi na viongozi wa kada mbalimbali huku watekwaji nao wakiwa na ndugu zao huko mitaani.
Palestinians imefika mahala hawaogopi tena kufa wala kuumia bali wamebaki na dhamira moja ya kupigana na adui usiku na mchana kwa pamoja, Nasisi sasa tunawalazimisha watu wetu wafike.

Vikundi vingi vya kigaidi na marcenaries wapo na kumilikiwa na mataifa makubwa kwamaslahi ya mataifa husika, Mataifa makubwa moja ya silaha yao kubwa kudestabilize nchi ni pale nchi inapogawanyika na kundi moja kuhisi linaonewa linahitaji msaada, basi kundi hilo husaidiwa mara moja ili kuchafua amani na upande mwingine kwa siri huzidi kuchochea hali pia kupitia watawala, hapo mtajikuta mnapigana hovyo hovyo bila hata kujua mnapigania nini.

Mwenyezi Mungu ametutunuku Amani basi tuilinde Kwa kudumisha umoja.
Mkuu umeongea vitu vya msingi sana. Hata paka ukimtaitisha sana na akakosa pakutokea basi kazi unavyo.

Ndio ilivyo sasa watu wanaumiza vichwa wanaepukana na hawa watekaji. Sio rahisi kuwazuia watu kukosoa, ndio nature ya binadamu na kuna baadhi yetu wanamkosoa hadi Mungu na bado Mungu hawanyang'anyi pumzi, wanadunda tu.

Kama Mwenyezi Mungu tunayemuimba kwenye wimbo wa Taifa anavumilia kukosolea wao wanajiona kina nani?

Ubaya wa haya mambo ukiongea unakufa na usipoongea pia unakufa. Vingenevyo tukumbushane aliongea nini Akwilina?
 
Hata Magufuli kabla hajafa alijua atakuwa Rais Milele, ndio maana alilazimisha viongozi wa ngazi zote kununua viwanja Chato

Sikushangai wewe mtu duni kujidanganya kama hivyo
Watazania ifike mahali tuseme imetosha. Mimi siki hao majabazi wanajiita polisi au usalama wakiji kunikamata sitakubali kwenda nao popote watamaliza kazi yao hapo walipo nikuta, baada ya mimi kufanya kila niwezalo kujiokowa.
 
Suala la kifo cha mzee Ali binafsi sioni kama linafanana na matukio mengine ya kutekwa .

Hawa watu ni either Wana Usalama wenzake au Wana CHADEMA .Kwa hali ilivyo Mzee wale watu angekuwa hawajui asingekubali kushuka kirahisi na kuongozana nao , na kuna uwezekano mkubwa wale watu anawajua .

Je hawa watu ni kina nani ?
 
Suala la kifo cha mzee Ali binafsi sioni kama linafanana na matukio mengine ya kutekwa .

Hawa watu ni either Wana Usalama wenzake au Wana CHADEMA .Kwa hali ilivyo Mzee wale watu angekuwa hawajui asingekubali kushuka kirahisi na kuongozana nao , na kuna uwezekano mkubwa wale watu anawajua .

Je hawa watu ni kina nani ?
muda utaongea hata mimi nawaza ivyo ivyo
 
Sielewi na ndiyo maana nimekuwa kimya. Wapo wanaojua na wataongea katika mfumo rasmi. Acha ujuaji na roporopo. Be warned!
acha kutisha watu,wao wanavyoo tuhumu jeshi wanaushahidi, na sisi pia kwa jicho la tatu tunaona kua wanaumizana wenyewe kwa wenyewe
 
Mtu amejitambulisha kwako ni polisi wanakuhitaji unawezaje kupinga arrest?.

Kama kweli Serikali iko serious, itoe tangazo public kupitia Rais na Waziri wa mambo ya ndani, marufuku kumuarrest mtu bila kuwepo mjumbe au mwanasheria wa mhusika, au hata waambatane na ndugu wa mhusika mpaka kituo cha karibu cha polisi maelezo rasmi yatolewa ndugu/mwanasheria/mjumbe wote wajue.
 
Suala la kifo cha mzee Ali binafsi sioni kama linafanana na matukio mengine ya kutekwa .

Hawa watu ni either Wana Usalama wenzake au Wana CHADEMA .Kwa hali ilivyo Mzee wale watu angekuwa hawajui asingekubali kushuka kirahisi na kuongozana nao , na kuna uwezekano mkubwa wale watu anawajua .

Je hawa watu ni kina nani ?
Kwahiyo awakubalie watu wa CHADEMA wampige pingu?

WTF
 
Back
Top Bottom