John Mnyika: Kiongozi wa CHADEMA Mzee Ali Mohamed Kibao, adaiwa kushushwa kwenye Basi na kuchukuliwa na watu wasiyojulikana

John Mnyika: Kiongozi wa CHADEMA Mzee Ali Mohamed Kibao, adaiwa kushushwa kwenye Basi na kuchukuliwa na watu wasiyojulikana

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu, John Mnyika kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (Twitter)
---
John Mnyika kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (Twitter) anaripoti:

Nimetaarifiwa usiku huu kuwa Mzee Ali Mohamed Kibao Mtaalamu katika Sekretariati CHADEMA amechukuliwa na watu walijitambulisha kuwa ni polisi(bila uniforms).
Walizuia basi la Tashrif alilokuwa amependa kutoka DSM kwenda Tanga kwa gari za kawaida wakaingia na kumfunga pingu.
Tunaendelea kufuatilia kupata taarifa kamili ikiwemo wamempeleka wapi. Nimetoa taarifa hii ya awali ili iwapo kuna yoyote alikuwepo kwenye basi au ana taarifa zozote kuhusu alipopelekwa atupatie au kutupa ushirikiano wa haraka.

1725653154659.png


Pia soma:
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Amechukuliwa hajatekwa hivyo tutulie vyombo husika vitatupa taarifa kamili
Watasema wao hawahusiki ukisoma Criminal Proceedings inasema kabla Polisi hajakukamata omba kitambulisho pia una haki ya kuambatana na ndugu mpaka kituoni sio wanakuchukua peke yako, siku hizi Polisibubu ni wengi sana Vifaa vya kipolisi vinauzwa tu km Pingu, Bastora, nk kadharika vinauzwa maeneo na wengine wanavikodisha kabisa kwa ajili ya hizo kazi kwa hio sio kila mwenye Pingu na bastora kiungoni bila gwanda kavaa kiraia ni Polisi
 
Back
Top Bottom